Mwanaume auliwa kwa kukatwa mapanga nyumbani kwa mpenzi wake, yadaiwa alikuwa akitembea na mke wa mtu

Mwanaume auliwa kwa kukatwa mapanga nyumbani kwa mpenzi wake, yadaiwa alikuwa akitembea na mke wa mtu

Waafrica ni watu makatili sana. Unaanzaje kuuwa kisa mwanamke? wapo tele wamejaa mitani unajikamatia tu mwengine. Hapo anaenda kuozea jela tu huyo tena.
 
Kuna watu walivyo na roho ngumu utashangaa walivyosoma habari hii tu ikadisa🙄🤔
 
Kufungwa jela sababu ya mwanamke ni ujinga uliopitiliza.
 
Mwanaume una akili kweli unaenda kwa mwanamke tena nyumbani kwake tena kitanda cha mumewe kabisa Ina maana vichaka hamuvioni hizi ni dharau na vifo vya kujitakia kabisa
 
Wanawake wengi sana tujitahidi kuwa na wake wengi ili ukiachwa huwazi sana
 
Mwanaume mmoja aliyetambulika kwa jina la Kibwana Musa mkazi wa Kijiji cha Kiziwa Kata ya kiroka wilayani Morogoro, amekutwa ameuawa alfajili ya kuamkia leo Juni 22, 2022 kwa kukatwa panga nyumbani kwa mwanamke anayedaiwa kuwa ni mpenzi wake.

Akizungumzia tukio hilo, Mwenyekiti wa kijiji hicho, Mbena Loki amesema Musa aliuawa na mtu aliyedaiwa kuwa ni mume wa mwanamke huyo aliyemtaja kwa jina la Farida Ally.

Mwenyekiti huyo amesema taarifa za kuuawa kwa mwanaume huyo zilianza kusambaa asubuhi na uongozi wa Kijiji ulifika eneo la tukio na kumkamata mwanamke huyo na kumpeleka kituo kidogo cha Polisi Mkuyuni kwa ajili ya usalama wake.

“Taarifa nilizonazo ni kwamba, kwa muda mrefu huyo mwanamke aliachana na mume wake (ambaye ni mtuhumiwa), hivyo alianzisha uhusiano wa mapenzi na marehemu, hata hivyo, mtuhumiwa alikuwa akiendelea kumfuatilia huyu mwanamke," amesema Loki.

“Leo kaamua kumvizia na kumkuta ndani na kuamua kumuua mwanaume mwenzake kwa kumkata mapanga," alisema.

Mtuhumiwa baada ya kufanya mauaji hayo alikimbia na jitihada za kumsaka zinaendelea.
Baadhi ya wanaume wanapomwacha mwanamke wanataka mwanamke huyo aje kumpigia magoti kuomba msamaha, na kujishusha kwa mwanamke, ili mwanaume aonekane mjanja.
Sasa anapotokea mwanaume kuzima matarajio hayo chuki inajitokeza dhidi ya mwanaume huyo aliyejitokeza kumfariji mwanamke aliyeachwa.
Hii inamaana kuwa, kuachwa kwa mwanamke kulikotokana na ugomvi kati yao kusichukuliwe kuwa KWELI bali ni geresha tu.
 
Back
Top Bottom