Mwanaume jenga utamaduni wa kurudi nyumbani na mfuko wa sokoni

Mwanaume jenga utamaduni wa kurudi nyumbani na mfuko wa sokoni

Mwisho utaanza kuosha vyombo na chupi za mkeo ili uheshimiwe kumbe anakulia gepu tu
Kila sehemu kuna tamaduni zake, mwaka 2000 nilikwenda Tanga kimajukumu, katika pitapita ufukweni nilikutana na jamaa yangu aliyekuwa Station Master wa TAZARA X akiwa na kapu la samaki kwenye baiskeli analipeleka nyumbani, ujuavyo watu wa Tanga walivyo wakarimu akanitaka nikapafahamu kwake, on our way tulipita zaidi ya sehemu 6 akinunua viungo na mahitaji mengine na zoezi hilo lilituchukua zaidi ya saa nzima
 
Maisha ni kupanga ukiweza fanya, lakini unaweza mpa mama pesa akafanya yote.
 
Jukumu la kwenda sokoni ni la mke. Acha kuingilia majukumu ya mkeo. Mpe hela ataamua akanunue nini kama mama house. Mambo yanayohusu jikoni usiingilie kabisa.... Usijifanye romantic kupitiliza.. utaharibu.
Mtoa mada hujamuelewa hajamaanisha urudi na rundo la mahitaji..Amemaanisha urudi na chochote kitu ndio maana kuna mmojq hapo kasema hata mkate mkate sio mbaya.
 
Vipi nikiacha/nikitoa hela wakanunue wao wenyewe.
zingatia neno ukirudi utakimbiliwa kupokewa, hiyo hela ukiwaachia ukirudi hawakukimbilii maana hauna cha kupokelewa

halafu mitoto itajua mama ndiye mnunuzi wa vitu, bila kuzingatia baba ndie mtoa hela, ila ukirudi navyo mwenyewe, watoto hawatosahau kuwa baba alikuwa hodari analeta vitu nyumbani kila akirudi
 
Ukiwa umeoa / nyumbani una familia hakikisha kila unaporudi home unarudi na mfuko umejaa vitu vya sokoni.

Ukijenga huo utamaduni itakuongezea heshima kwenye nyumba yako hata kabla haujaingia ndani ya nyumba yako utaona mke au watoto wanakukimbilia kukupokea.
Hizi ni zangu hizi. Nikitoka wakati wa kurudi ni lazima nimebeba kitu mkononi. Hili nilijifunza kutoka kwa dingi yangu.
 
Ukiwa umeoa / nyumbani una familia hakikisha kila unaporudi home unarudi na mfuko umejaa vitu vya sokoni.

Ukijenga huo utamaduni itakuongezea heshima kwenye nyumba yako hata kabla haujaingia ndani ya nyumba yako utaona mke au watoto wanakukimbilia kukupokea.
"Mbwa hambwekei anayempa chakula"
 
Wanawake wa bongo hata urudi na gunia dharau zipo palepale...unaweza unaambiwa leo ndo umeona uje na furushi lako huku..wake zako wa nje mmegombana Nini?
 
Ukiacha pesa kuna tatizo gani? Labda vya watoto...sasa wengine tunanunua vitu kwa wingi na pesa tunatoa kwa wingi then inatulia,kununua ni ukiamua tu .
 
Back
Top Bottom