Mwanaume jenga utamaduni wa kurudi nyumbani na mfuko wa sokoni

Mwanaume jenga utamaduni wa kurudi nyumbani na mfuko wa sokoni

Mtoa mada hujamuelewa hajamaanisha urudi na rundo la mahitaji..Amemaanisha urudi na chochote kitu ndio maana kuna mmojq hapo kasema hata mkate mkate sio mbaya.
Hakuna kitu kama hicho. Hizo kazi za mama. Mwanaume rudi na hela.
 
Ukiwa umeoa / nyumbani una familia hakikisha kila unaporudi home unarudi na mfuko umejaa vitu vya sokoni.

Ukijenga huo utamaduni itakuongezea heshima kwenye nyumba yako hata kabla haujaingia ndani ya nyumba yako utaona mke au watoto wanakukimbilia kukupokea.
Kweli aisee kwa sisi tulio na familia huu ushauri nimeuchukua
 
Ila kurudi nyumbani bila kitu mkononi inauma!!
Sometimes michongo haijakubali hata maembe ya buku mbili hakuna.

Nakumbuka Nikirudi na mazaga zaga naingia ndani kwa mbwembwe naliita Dume langu la mwanzo liende kwenye gari kubeba mizigo najisikia raha sana.

Likishaenda tu Mama yao naye anawafata hapo nimebaki kwenye kochi nakunywa maji ya baridi.

Raha za ndoa sio ghali ni basi tu
 
Jukumu la kwenda sokoni ni la mke. Acha kuingilia majukumu ya mkeo. Mpe hela ataamua akanunue nini kama mama house. Mambo yanayohusu jikoni usiingilie kabisa.... Usijifanye romantic kupitiliza.. utaharibu.
Hii inafanyika siku moja moja. Unaweza ukawa umeacha hela ya nyama. Lakini si vibaya jioni ukarudi na Samaki hata watano tu. It has an impact
 
Ukiwa umeoa / nyumbani una familia hakikisha kila unaporudi home unarudi na mfuko umejaa vitu vya sokoni.

Ukijenga huo utamaduni itakuongezea heshima kwenye nyumba yako hata kabla haujaingia ndani ya nyumba yako utaona mke au watoto wanakukimbilia kukupokea.
Point kubwa sana hii.. Big up!!
 
Wanawake wenyewe hawa hawaridhiki ukifanya hivo siku ukiwa hujaleta utaletewa zogo
 
Ukiwa umeoa / nyumbani una familia hakikisha kila unaporudi home unarudi na mfuko umejaa vitu vya sokoni.

Ukijenga huo utamaduni itakuongezea heshima kwenye nyumba yako hata kabla haujaingia ndani ya nyumba yako utaona mke au watoto wanakukimbilia kukupokea.
Hakuna kikao cha wanaume tulicho kaa tukakubaliana hilo jambo
 
Mbona hiyo ndio culture yangu. Lazima nikirudi waje kufungua "buti", ikishindikana Hata Jojo na big G.

Yaani unafika Getini hujapiga honi dogo anafungua geti , ukiwa unapita utadhani natumian remote madogo wamekariri muunguruma wa ndiga ya kijapani.

Mwisho wa mwezi ndio mazagazaga yote muhimu yanaletwa, inabakia vya kujazilia tu Kwa kweli inapendeza.
 
Back
Top Bottom