Mwanaume jitahidi kujua msimamo wako kiimani na usimame nao kabla hujaingia kwenye ndoa

Mwanaume jitahidi kujua msimamo wako kiimani na usimame nao kabla hujaingia kwenye ndoa

Katika ya wokovu Baba wa kiroho ni mtu anayekuongoza (Guiding) kwenye njia sahihi kiimani kuelekea hatima yako (Purpose) kupitia maelekezo kamili kutoka kwa Mungu. Najua unajua
Sijui, ndio maana nimeuliza, kwahiyo hii ni Kwa Walokole?
 
kwa wakristo wanaume wengi hawashiki dini ndo maana hao mababa wa kiroho wanazingatiwa, na wanawake wanashika dini haswa, mwanaume wa kawaida hawezi kuendana na hayo mapigo.
Ndugu kushika yote yahitaji moyo. Maana muda mwingi wanaume tunakuwa kwenye kutafuta ukirudi unakuwa umechoka hata muda wa kusikiliza story za mkeo unakosa unaishia kulala katikati ya story zake.

Kuna mwalimu mmoja wa masomo ya kiroho alizungumza kitu ambacho ni kigumu sana kwetu.
Jamaaa alisema wanaume mkirudi kwenye shughuli zenu za kila siku hakikisha unabakisha nguvu za kusikiliza mkeo alienda wapi akanunua nini akakanyagwa mguuni saa ngapi. Maana hivyo ndio vitu wanapenda kuwasimulia wamme zao, wanapenda kusikilizwa.

Mwanaume ukishindwa kutenga muda wa kumsikiliza akija kanisani akakutani na mimi, mimi nampa sikio lote aongee hata masaa manne. Atakuja leo atakuja kesho na kesho kutwa mwishowe anaanza kuona akija kwangu ndio ndio sehemu pekee anapata amani maana anayatoa mambo yake yote hapo.
Na hapo ndio mwanzo wa kuanza kuhamisha vipaombele vya mumewe kwenda kwa baba ake wa imani.
Na hapo ndio utaanza kuona mnabishana, mke anakataa anachoambiwa na mumewe muda mwingine anaweza hata kukupa haki yako ya ndoa akwambie anawahi kwa mwalimu mafundisho.

Haya maswala changamoto sana.
 
Nilitaka kucomment kabla ya kusoma ila baada ya kusoma nimepata wazo zuri. Kiukweli awa wababa wa kiroho sio poa sasa hivi na wanawake wanavyomezeshwa ndivyo wanavyokula, ni muhimu sana kuwa na msimamo wa kiimani.
 
Nilitaka kucomment kabla ya kusoma ila baada ya kusoma nimepata wazo zuri. Kiukweli awa wababa wa kiroho sio poa sasa hivi na wanawake wanavyomezeshwa ndivyo wanavyokula, ni muhimu sana kuwa na msimamo wa kiimani.
Huo ndo ukweli
 
Back
Top Bottom