Mwanaume mbembeleze mwanamke baada ya ugomvi, mtatuua kwa stress

Usemalo nilakweli kabisaaa..
Tatizo nyinyi wadada wa dot.com hamjui/kujifunza namna yakuzima ugomvii mnataka kujifananisha na mwanaume, hapo ndipo kisanga huanzia..

Mwanaume hafananishwi na kitu chochote kile sawa na mwanamke vilevile..
Jueni nafasi zenu si kushindana..
Umeanza vizuri ila ulivyomalizia woga ndo umeharibu!

Kila mmoja ana wajibu wa kuhakikisha mahusiano yanakuwa ya amani,furaha na upendo!

Halafu kila mmoja anamjua mtuwe aloko naye kwenye mahusiano, kama wako ni pasua kichwa ulimpenda mwenyewe! Hao wa dot com wapo wapi eti!

Na ujue kuna wanawake na wasichana, na kuna wanawake wenye akili za kisichana sasa kazi kwako!
 
Khaaaah!!
Eti huu ndio urijali[emoji134][emoji134]
Bora niwe na asie rijali tu nijue moja.
Yeah, kuishi na mwanamke kwa akili kuna mengi humo katikakati. I wouldn't say I'm so sorry directly, lakini kwa matendo yangu utajua nimeomba msamaha na najutia nilichofanya, lakini eti "samahani mke wangu, nisamehe"..teh nah nah!!
 
Mama si afadhali wewe unaongelea hata ulie na malengo nae, wenzio ni wanandoa kabisaaaa na wananuniana na wanajisifia kununa(tena wanaume[emoji134])

Wengine anakosea yeye halafu anataka uombe msamaha wewe.
Inawezekana vipi lakini mtu mnanuniana na mnalala kitanda kimoja?

Mie naonaga kama maigizo vile dear
 
Khaaaah!!
Eti huu ndio urijali[emoji134][emoji134]
Bora niwe na asie rijali tu nijue moja.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]kabisaaa bora tuwe na wanaume wasio marijali tu kwa kweli yaani nikubali kuteseka kwenye ndoa eti ili mradi tu nionekane nimeolewa na mwanaume rijali, nahi karungi.
 
Kuna wanawake wenye gubu kari hatakusemesha hadi mwezi uishe hata ufichi chupi yake......hasa wanawake wa mikoani wanamisimamo mikali sanaa hawana smile au jokes akiamuwa ameamuwa tu
Sasa hao ndo wanaendana na wanaume wao wa mikoani
 
Easier said than done! Tafakari maisha yako na ndugu wa damu yalivyo, yachukue yaishi ndani ya nyumba na mtu mliyekutana ukubwani, ain't easy my dear!
Nope
Kipi kikubwaa cha kukununisha siku ama wiki!

Hakuna kitu kigumu kama kukaa saa kadhaa bila amani!

Nina ndugu watatu sikumbuki tumegombana lini, tukigombana huwa tunaishia kucheka tuu kama ikiwa worse simu inapigwa kwa baba kabla hujafika kwako mnaanza kucheka tuu!

Maybe mie ni muoga wa ugomvi ila kununa siku nzima nitakufwa
 
Mimi niliambiwa kwenye kikome na babu nikubembekeze kwa kukupiga na mkuyenge au mgegedo wa nguvu!!!!!
Kwenye mahusiano ya boyfriend na girlfriend au mahusiano yoyote yale lazima kunakuwepo na kuhitilafiana kwa hapa na pale

Linapokuja suala la kugombana ya wawili hao kinachofuata ni kusuluhishana mambo yaishe mapenzi yaendelee

Kunapotokea ugomvi wa kimahusiano sio siri sisi wanawake huwa tunaumia sana,na huwa tunapenda mahusiano yazidi kuwepo hasa kama uliyenaye ni yule wa moyo wako

Katika hali hiyo tunategemea mwanaume amuonyeshe mpenzi wake pamoja na kugombana bado anampenda na anampenda sana

Hapa tunamtegemea mwanaume baada ya kugombana,baada ya SAA moja mwanaume atakuwa na jukumu la kuweka mahusiano sawa,kwa kumtumia text za hapa na pale,za kumbembeleza mwanamke hata kama mwanamke ndo alikuwa na makosa,haijalishi nani kaanzisha ugomvi ila mwanaume ana jukumu kubwa la kuweka mahusiano sawa

Kwa sasa hali imebadilika sana kwa hawa wanaume,mnagombana,mnamaliza hata siku mbili hakutumii text,wala kukupigia sim,na kama mwanamke ataendelea kupiga kimya,kinachofuata ni mwanaume kuanza kuweka picha kwenye mitandao ya kijamii ambazo hazieleweki,mara aweke za mwanamke fulani,mara aweke za wanawake na status kibao,au akae online muda mrefu ambapo si kawaida yake

Unabaki unajiuliza ina maana mahusiano yameisha,mbona sielewi,mapicha picha ya nini tena

Ukweli ndo huu,tunapogombana na ukamaliza masaa 2 bila kutuma sms au kupiga sim hata kuulizia kitu fulani,yaani huwa tunaumia sana

Na kama tangu ugomvi yamepita masaa 5 hujatuma sms, huwa tunahisi kuchanganyikiwa,sms inaingia unadhani ni baby kumbe za watu wengine au mitandao maumivu huwa yanatuzidi

Nyie wanaume acheni kuwatesa wawapendao,hamjui tu tunavyoumia

Ndo maana muda mwingine unasema bora usiwe kwenye mahusiano

Tubembelezeni basi baada ya ugomvi,hata kama sisi ndo wakosaji au hata kama ni nyie wakosaji
 
Kuna rafiki yangu mmoja anawaambiaga wanaume wenzie ukiona mmegombana na mkeo akakununia wewe nenda kakaze mifuniko yote ya ndoo ndani kwenu yaani hakikisha umekaza kwa nguvu hadi anashindwa kufungua

Au mfichie vitu vyake vya muhimu na hakikisha umeficha sehemu ambayo hawezi kuviona yaani kwa namna yoyote ile akikosa msaada lazima atakuja tu kukuongelesha kukuomba umsaidie

Sasa alivyosema hivyo angalau nikaona kuwa huyo ni mwanaume kweli hata kama hawezi kukufuata kukubembeleza basi atatafuta tu namna ya wewe kuja kumuongelesha yaani angalau ataonyesha jitihada za kutaka msuluhishe na mwanamke ukiona hivyo unajiongeza

Kuliko yule mwanaume ambaye mkigombana unakuwa ndo umempata nafasi ya kwenda kulala nje ya nyumba yenu miezi na mchepuko na usipomsemesha ndo nitolee hiyo yaani hata yeye haonyeshi jitihada yoyote ya kutaka umuongeleshe aise kuna midume ina gubu halafu mtoto wa kiume kususa au kununa haipendezi jamani looh
upo mwanaharakati!
 
Wanaume wa kuwambeleza kila wakati waliisha awamu ya Kikwete. Siku hizi ukiendekeza utoto unapata unachostahili.
 
Kwenye mahusiano na maisha ya kawaida neno NAOMBA UNISAMEHE huwa lina maana sana. Hata ukilitamka kwa kumaanisha unahisi kabisa thamani yake.

Kwenye mahusiano pakiwa na tofauti lazima mmoja ajishushe ndo maisha yanaenda kwa furaha. Umekosea basi tambua nafasi yako katika mahusiano omba msamaha wala haitogharimu chochote!
Tatizo ni pale kila siku anayejishusha ni yule yule hata kwa kosa lisilo lake.
 
Kwenye mahusiano ya boyfriend na girlfriend au mahusiano yoyote yale lazima kunakuwepo na kuhitilafiana kwa hapa na pale

Linapokuja suala la kugombana ya wawili hao kinachofuata ni kusuluhishana mambo yaishe mapenzi yaendelee

Kunapotokea ugomvi wa kimahusiano sio siri sisi wanawake huwa tunaumia sana,na huwa tunapenda mahusiano yazidi kuwepo hasa kama uliyenaye ni yule wa moyo wako

Katika hali hiyo tunategemea mwanaume amuonyeshe mpenzi wake pamoja na kugombana bado anampenda na anampenda sana

Hapa tunamtegemea mwanaume baada ya kugombana,baada ya SAA moja mwanaume atakuwa na jukumu la kuweka mahusiano sawa,kwa kumtumia text za hapa na pale,za kumbembeleza mwanamke hata kama mwanamke ndo alikuwa na makosa,haijalishi nani kaanzisha ugomvi ila mwanaume ana jukumu kubwa la kuweka mahusiano sawa

Kwa sasa hali imebadilika sana kwa hawa wanaume,mnagombana,mnamaliza hata siku mbili hakutumii text,wala kukupigia sim,na kama mwanamke ataendelea kupiga kimya,kinachofuata ni mwanaume kuanza kuweka picha kwenye mitandao ya kijamii ambazo hazieleweki,mara aweke za mwanamke fulani,mara aweke za wanawake na status kibao,au akae online muda mrefu ambapo si kawaida yake

Unabaki unajiuliza ina maana mahusiano yameisha,mbona sielewi,mapicha picha ya nini tena

Ukweli ndo huu,tunapogombana na ukamaliza masaa 2 bila kutuma sms au kupiga sim hata kuulizia kitu fulani,yaani huwa tunaumia sana

Na kama tangu ugomvi yamepita masaa 5 hujatuma sms, huwa tunahisi kuchanganyikiwa,sms inaingia unadhani ni baby kumbe za watu wengine au mitandao maumivu huwa yanatuzidi

Nyie wanaume acheni kuwatesa wawapendao,hamjui tu tunavyoumia

Ndo maana muda mwingine unasema bora usiwe kwenye mahusiano

Tubembelezeni basi baada ya ugomvi,hata kama sisi ndo wakosaji au hata kama ni nyie wakosaji
Kwa hiyo umesikia ss ndo tuna mioyo ya chuma ambao hatutaki kubembelezwa, ujinga ufanye ww halafu nikubembeleze Tena, badae unajisifu kwa shoga zako jamaa Hana usemi kwangu , hata nifanyaje hawezi chomoka, utakua ni upuuzi wa hali ya juu
 
Back
Top Bottom