pappilon
JF-Expert Member
- Jan 27, 2015
- 3,192
- 3,559
Mkuu Kuna wanawake pasua kichwa acha kabisa...Kuna bro wangu kazaa na mwanamke wa singida...siku moja kampa 1M kwa ajili ya kutafuta chumba na kulipia maana alisema amechoka kukaa kwao..huwezi amini kesho yake yule mwanamke anampigia jamaa simu anamwambia amtumie 10k ya dalali...jamaa akamwambia hyo 10k toa hapo kwenye 1M ..mwanamke alitokomea kusikojulikana alikuja kuwasiloana na jamaa baada ya miezi sita tena akawa anaomba hela ya matumizi.Imagine mwanaume upo bar unakula bata kama kawaida na kuwalipia marafiki waliokuzunguka pia,lakini kuna sehemu umetelekeza Mtoto damu yako kabisa na hujui anakula nini,anavaa nini anaishije?
Kweli kabisa unaweza kwenda kitandani ukalala usingizi kabisa na huku umetelekeza damu yako!?,wanaume wa kweli tunapatikana mikoa ya kaskazini ni nadra sana kukuta mwanaume wa kanda hii anatelekeza damu yake!
Mwanaume usikubali kwa gharama yeyote kupoteza damu yako bila kujali changamoto za wanawake wakorofi,
Mwanamke akikukazia usichukue mtoto na una uhakika ni damu yako kuwa mpole baada ya miaka mitano pora Mtoto tokomea (jokes)
Mkuu hakuna mtu anapenda telekeza damu yake ila wakati mwingine watu wanaamua tu kukaa kimya kutokana na makwazo ya waliozaa nao.