Mwanaume wa kiislamu aliye tayari kuwa rafiki, mchumba hatimaye mume

Mwanaume wa kiislamu aliye tayari kuwa rafiki, mchumba hatimaye mume

Ah kazi tena mwanawane inakuwaje...njoo nikupe bajaj na boxer mkaanze maisha. Vijana kama nyie mnaotaka kuikimbia zinaa inabidi tuwawezeshe
Haaa haaa haaa asante mkuu, ngoja nimuulize mrembo kama atakubali.
 
Ndugu zangu waislam mnakwama wapi sasa!

Aaliyyah hii imekaa vizuri, mfungo ukiisha kazi ni moja tu, vijana ma-ostaath naamini wapo wa kutosha kabisa🤣
 
Allah akujaalie upate mume mwema mchamungu ameen

Zidisha dua, Allah atakupa aliye sahihi kwako.

Mimi nilimpata mke wangu kupitia facebook! ALLAH anaunganisha nyoyo hata kama mkiwa mbalimbali baina ya mashariki na magharibi
 
Usijichanganye ukapata mwanamke ama mwanaume wa kufanya nae maisha kupitia mitandaoni majuto yake ni makubwa sana. Bora upate mwenza kupitia njia mbadala kama kwenye msiba, kwenye vyombo vya usafiri wa umma ama kwenye vilabu vya Wanzuki na Kangara ama kwenye nyumba za ibada msikitini, kanisa la RC, Sabato, anglicana na KKKT. Onyo usije oa ama olewa na wapendwa toka kwa Mwingira, Kakobe, Gwajima, Lusekelo, Kuhani Mussa, Mwamposa na majambazi wengine wanaoibia watu kupitia haya makanisa ya mabati.
 
Sio kweli
 
Hakuna mke hapo, mbaguaji ataleta shida kwa watoto kipindi wanataka kuoa/kuolewa na dini tofauti
Mkuu umelewa au, hebu rudia kusoma comnent yako na kisha uandike tena.
 
Asalam aleykum

Nimekuwa single kwa mda mrefu nimeona sasa ni muda sahihi kuwa na familia Sihitaji Mtu wa kusumbuana nae tena

Nahitaji mwanaume wa kuanzisha nae familia mwenye uhitaji navigezo ninavyohitaji naamini Kuna wanaume wema wenye uhitaji

Sifa za mwanaume.
-Muislam awe anafanya ibada kama hafanyi awe tayari kufanya ibada
-miaka 31 Hadi 35
-mwanaume anaejua na anauishi uanaume wake
-awe na utayari wa kuwa na familia
-awe na shughuli halali akiwa muajiriwa itapendeza zaidi

Sifa zangu
-Mjasiriàmali pia elimu kidato cha nne
-miaka 27 mwaka huu Dec natimiza 28
-ninafanya ibada
-sinamtoto
-sijawahi kuolewa pia

Nyongeza
Nahitaji Mtu serious na mwenye uelewa kuwa mume ni nataka kuwa mke mzuri na mwema na mama mzuri wa watoto wangu tuishi wa kuzingatia wajibu wa Kila mmoja kwa mwenzie
Nawakaribisha PM wenye vigezo kama hauna naomba usije
Nawatakia Ramadhani kareem
Dah umri tu umenikosesha mke
 
Mwaka mmoja umenifanya nikose mke mwema

Nina miaka 36. Upo tayari?
 
Back
Top Bottom