Mwanausalama Tanzania aaibika kutumia nguvu na mwanausalama wa Obama kumlinda mwandishi

Mwanausalama Tanzania aaibika kutumia nguvu na mwanausalama wa Obama kumlinda mwandishi

Jamani huu ugomvi hautuhusu, huu ugomvi ni wa Mume na wake zake, sie hautuhus; Uhuru, wanausalama Vs Serikali ya CCM, sie unatuhusu nini?? Waache wao wenyewe waumane kwanza wasijekutusingizia bure..
 
Ndivyo mnavyofundishwa katika utendaji wenu? Haya ni maneno mazito sana kuhusu maafisa wa usalama wetu.
Jasusi
Mbona haya ya kutumia nguvu huku USA yapo mengi sana unataka tukuwekee data za kiasi police department zinalipa watu kwa makosa ya kutumia nguvu na unyasaji? Mkuu angalia sana kuandika vitu kwa kudakia hao waandishi lugha mgogoro hapo palikosekana mkalimani!
 
Last edited by a moderator:
Hiyo mipoliCCM,ishazoea kufanya madudu ya aina hiyo,si mnakumbuka namna Kamanda Kamuhanda,alivyoamrisha mauajiya mwandishi Mwangosi,ambapo hadi sasa huyo Kamuhanda hakupandishwa kizimbani kujibu tuhuma za mauaji,na badala yake,bosi wake JK,amempandisha cheo,kwa utumishi uliotukuka wa kumwua Mwangosi!

Kwa hiyo hata wale wanaofikiri ile kauli ya Pinda,ya kusema PIGA TU TENA WAPIGWE SANA KWA KUWA TUMECHOKA.

Hiyo siyo kauli ya Pinda as an individual,bali huo ndio msimamo wa serikali nzima ya CCM.

Kumbuka JK,alipotoa siri kwenye mkutano mkuu wa CCM,uliopita,alipowaasa wanaCCM wenzake,wapunguze kuwatumia poliCCM,kuwabeba kwenye shughuli zao za kisiasa!!
mmechokonowa wee angalau mpate lilooenda tofaut katika mapokezi obama atimaye mmekutana na hili,kuhitilafiana ni jambo la kawaida katika utendaji,maana naona mmeanza na kejeli,ohh wamefundishwa kutumia vitu vyenye ncha kali,haya yanausiana vipi na masuala ya wanausalama kuitilafiana??michadema utaijua tu,nilitegemea utahoji labda mbona viongozi wa upinzani hawakualikwa kuteta na obama,unakuja kuhoji upuuzi apa.
 
Kumbe ndio maana hawa jamaa huwa wanaamua jukumu la usalama wa raisi wao libaki kwao ni si kwa nchi wanayoitembelea.
 
Jasusi
Mbona haya ya kutumia nguvu huku USA yapo mengi sana unataka tukuwekee data za kiasi police department zinalipa watu kwa makosa ya kutumia nguvu na unyasaji? Mkuu angalia sana kuandika vitu kwa kudakia hao waandishi lugha mgogoro hapo palikosekana mkalimani!

Kumbe marekani wakimkosea raia "WANAMLIPA"!?? huku bongo thubutu yako...
 
Last edited by a moderator:
"Ndivyo mnavyofundishwa katika utendaji wenu"? jibu ni ndiyo ndivyo wanavyofundishwa.
 
Huyo askari wetu alijibu nini baada ya kuulizwa kwa kimombo ikiwa hayo ndiyo wanayofundishwa katika utendaji wao?

Isije ikawa lugha ilikorofishwa akajibu yes Sir.

Ana bahati kweli huyo Mmarekani alikuwepo karibu .............. la sivyo angepata ule mkong'oto wa Pinda wa kufa mtu!!


Mmarekani alikuwa anaavoid kama vyombo vya habari vingeinasa hiyo ingekuwaje??
 
Vijana wa buku 7 siwaoni hapa, ninaiman angekuwa ni mwandishi wa gazeti la TANZANIA DAIMA sijui nini kingetokea hapo, lakini ni wao kwa wao shaka hakuna hii ni aibu ya hali ya juu kabisa ( ndo hivyo mnavyofundishwa?) Naona wanaumbuana wao kwa wao.
 
Candid Scope in as much as sisupport matumizi ya nguvu, sidhani pia kama Marekani na wenyewe wanaheshimu demokrasia na haki za binadamu kama unavyotaka kuonesha umma wa watanzania.

Sikuwepo Marekani lakini tulifanikiwa kuona jinsi polisi wa Marekani walivyowapiga na kuwaumiza waandamanaji wa wall street kule kwao:

Police beat back Occupy Wall Street protesters, dozens arrested - YouTube

Ilibidi uwaulize na wao, is this how they are taught to deal with protesters?!

Obama jana anashauri wamisri kuheshimu freedom of assembly, vipi Marekani kule kwao kwanini waliwapiga wall street demonstrators?
 
nafikiri kwa tendo hillo ni wazi ulimwengu utakuwa umethibishwa kwamba serikali yetu na vyombo vya dora hawawatendei haki raia. WAtaumbuka sasa ccm kuja kufika 2015,
 
Hata mimi natamani angemdunda huyo mwanausalama wa Marekani halafu akasema anatekeleza maelekezo ya pinda, maana amechoka kutumia akili, ni nguvu tu.
Lol!, lakini nyie!...am dyin!...lol!
 
ha ha ha loh ilikuwa aibu iliyoje yaani wana usalama wetu yaani wameshazoea kutumia nguvu ilikuwa haina haja ya kumzuia cz alikuwepo kwenye list tote hayo ili aonekane wajifunze wanausalama wetu kuangalia wenzao wanavyofanya kazi
 
"...NO NO Sir! We are not TEACHED that way. You know, you know we are AMRIzed to KICK if they NOT HEAR, we KICK ONLY, because us TIRED NOW..."
Kama nawaona vl...and them are supposed to be trusted with "PUBLIC SAFETY"??!!!
 
Hii ni nzuri sana, You just cannot get it better! Hebu fikiria, mwandishi aliyenyanyaswa ni wa Gazeti la UHURU, ambalo huwa linashabikia sana matumizi ya nguvu na mabavu ya vyombo vya dola dhidi ya vyama vya upinzania. nina uhakika Celina ni mmojawapo wa wale ambao huwa wanapiga vigelegele pale wananchi wanaohudhuria mikutano au maandamano ya vyama vya upinzani wanafanyiwa unyama na Polisi na wanausalama. na pia Gazeti la UHURU lilishangilia sana kauli ya Pinda ya "PIGA, PIGA...". Sasa nadhani tumepata fundisho zuri sana kwamba hawa wapiga debe wa serikali wamepata "a taste of thier own medicine". ile "Sukari" ambayo huwa wanapewa vyama vya upinzani, sasa wameionja wenyewe, angalau kidooogo!

Lakini perfection ya issue hii ni kwamba aliyeripoti ni Gazeti la Serikali!!! How marvellous! so Symmetrical! so beautiful! simply outrageous!! Jamani rahaa???

Lakini baada ya kusema hayo napenda kumpa pole dada Celina na kwa kweli hii ni aibu kwetu sisi sote. "hivi ndivyo mnavyofundishwa" itusaidie kutambua kwamba umefika wakati wa kusuka upya vyombo vyetu vya usalama. ni ipi falsafa ya vyombo hivi? kulinda walio madarakani kwa gharama yoyote? kulinda maslahi ya taifa? ni jeshi la ulinzi tu ambalo lilisukwa upya, na kwa kweli limekuwa JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA kwa muda mrefu sana, ingawa matukio ya Mtwara yanaonesha kwamba nalo limeanza kupata kutu kutokana corruption iliyopo sasa hivi katika taifa letu. Tunachohitaji ni kufumua na kusuka upya vyombo vyetu ili viwe kweli vyombo vya usalama wa taifa.

kama inatokea upo mahali usipotakiwa, Mbwa aliyefundishwa, anahakikisha kuwa uko chini ya ulinzi na wala hafanyi kitu zaidi, mradi utulie ulipo, anasubiri maelekezo zaidi. mbwa asiyefundishwa atakuvamia na kukurarua. high security sio maana yake mkwara mkali, vitisho, maguvu. high security ni high professionalism, kutumia zaidi akili kujua yupi ni hatari na yupi si hatari. wanausalama wetu wanafundishwa "PIGA, UA, MWAGIA MAJI YA KUWASHA..." umefika wakati wafundishwe kutumia ziadi akili, na kuwa focused kwenye maslahi ya taifa letu na si kulinda kikundi cha mafisadi walioko serikalini kwa sasa
 
Back
Top Bottom