sajo
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 3,474
- 6,195
MkuuWale wanafanya biashara siku wakiona Habari za Siasa ndio zina wasikilizaji wengi Radio zitahamia huko.
Kinachoangaliwa ni Wapi pana walaj wengi na sio weledi wa kazi.
Ukiangalia kwa kina kinachoanza sio walaji kuwa wengi bali ni radio au watangazaji kuanzisha hicho kitu. Wasikilizaji ni bendera fuata upepo, wao wanafuata kile ambacho redio zinataka.
Mfano, tuliambiwa kuwa hiphop hailipi kuliko afromusic (kubana pua), lakini hilo halikua jambo la kweli bali ni radio na mamogul flani walitaka biashara ya muziki huo wa kubana pua ndio iwe kubwa na ikawa. Walitangaza sana (promo), wakawanyong'onyeza wanahiphop basi ikawa, matokeo wakasema kuwa soko ndio linahitaji hivyo, kumbe ukweli ni wao ndio walihitaji hivyo.
Vivyo hivyo kwenye michezo nk, ni redio ndio zinazoamua na sio kuwa wananchi (soko) ndio linaamua. Bahati mbaya redio zenyewe zinaigana, kwa hiyo moja kubwa ikianzisha utamaduni flani basi zilizobaaki zote zinafuata humohumo