Mwandishi mkongwe Abdallah Majura, ahoji kuhusu redio kujadili michezo asubuhi

Wale wanafanya biashara siku wakiona Habari za Siasa ndio zina wasikilizaji wengi Radio zitahamia huko.
Kinachoangaliwa ni Wapi pana walaj wengi na sio weledi wa kazi.
Mkuu

Ukiangalia kwa kina kinachoanza sio walaji kuwa wengi bali ni radio au watangazaji kuanzisha hicho kitu. Wasikilizaji ni bendera fuata upepo, wao wanafuata kile ambacho redio zinataka.

Mfano, tuliambiwa kuwa hiphop hailipi kuliko afromusic (kubana pua), lakini hilo halikua jambo la kweli bali ni radio na mamogul flani walitaka biashara ya muziki huo wa kubana pua ndio iwe kubwa na ikawa. Walitangaza sana (promo), wakawanyong'onyeza wanahiphop basi ikawa, matokeo wakasema kuwa soko ndio linahitaji hivyo, kumbe ukweli ni wao ndio walihitaji hivyo.

Vivyo hivyo kwenye michezo nk, ni redio ndio zinazoamua na sio kuwa wananchi (soko) ndio linaamua. Bahati mbaya redio zenyewe zinaigana, kwa hiyo moja kubwa ikianzisha utamaduni flani basi zilizobaaki zote zinafuata humohumo
 

Watu wanaangali michezo sababu serikali imeshindwa kuwapa ajira na kuandaa mazingira rafiki ya kujiajiri. Mtu kama hana kazi atafanya chochote kile kupoteza muda.
 
Wakati wa kikwete watu walijadili siasa alipokuja Magu mijadala ya kisiasa ilikaa kimtego sana ukijichanganya tu chombo kinakula burn Kali watu wakaona wachange gia kwenda kwenye mpira (four four two viwanjani) na ndio wamebaki huko mazima
Sio kwa kupenda
 

Majura na yeye asituzengue ,mambo yanabadilika ,anadhani bado tupo mwaka 1947 yupo RTD kipindi cha michezo saa mbili kasoro usiku? Hajui kwamba kuna wengine wametoka kazini shift za usiku na hiyo asubuhi wapo nyumbani ,sio wote asubuhi wapo makazini.

Radio zipo nyingi na hiyo asubuhi kuna redio tu nyingi hazina vipindi vya michezo ,ni option kusikilza michezo ,hawalazimishi...Yeye si anaredio pia?
 
Radio zimekuwa mawakala wa kampuni za kubet.
 
Burn❌
Ban✅
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…