Nimerudi tena baada ya kuona upuuzi umepungua Kwa asilimia kubwa....na shukrani zimuendee
adriz ambaye alitoa hoja kadhaa ambazo zimesaidia kuweka Hali ya hewa kuwa nzuri.
Vile vile nitoe kongole Kwa mkuu
Tsh na mkuu
Kalunya Kwa kujadiliana vizur Kwa ustaarabu mkubwa much respect brothers......siku zote kwenye mijadala ya Dini hatafutwi mshindi Ila tunashare maudhui ya Dini zetu na kisha kila mtu anachakata hizo taarifa kivyake....
Kuna hoja kadhaa ningependa kuzijadili kidogo......binadamu yoyote huamasishwa na mambo mawili Tu....ambayo ni karoti na fimbo...Kwa maana akifanya jema atapata zawadi na akifanya baya ataadhibiwa...hayo ndo mambo ambayo yanaweza mfanya binadamu akabadili Tabia yake na mwenendo wake.
Ndo maana Mwenyezi Mungu ameahidi pepo Kwa wataofanya matendo mema na Moto Kwa ambao wataofanya mambo maovu.....haya mambo mawili ndio yanayo tufanya kufuata maamrisho yake na kuacha makatazo yake....sasa nije kwenye hoja ya wanawake WA peponi ambao wanaitwa Mahurulaini...ambao baadhi ya watu wametoa hoja kuwa waislamu wamebadilishwa akili zao kwa kuahidiwa wanawake mabikra! Iko hivi....Mwenyezi Mungu hapendi zinaa hata kidogo,kwahiyo anajua waja wake wapo ambao wanazini....anachotueleza Allah (Mwenyezi Mungu) ni kuwa tusibabaike na hawa wanawake WA dunia hii Kwa kuzini Bali tuache zinaa kwani ametuandalia wanawake Bora huko peponi ambao wametakaswa na machafu yote,kwahiyo kama hawa wanawake wanatuzuzua basi kuna ambao ni Bora kuliko hao Kwa wale ambao watajitakasa na kufuata maamrisho ya Mwenyezi Mungu,hapo imetumika kanuni ya karoti na fimbo.
Tuache pombe na kamari ambazo ni miongoni mwa kazi za shetani,ambazo zina hasara Kwa wengi na faida Kwa wachache....tuongee ukweli mpo wengi mnao bet humu lkn je ninani anaefaidika zaidi kama sio ambao wanamiliki hayo makampuni? Na ulevi unawasababishia watu wamsahau Mola wao na kuacha swala....sasa wanaambiwa waumini kuwa kama ishu ni pombe Tu! Basi huko peponi kuna pombe ya kutosha ambayo haileweshi wala kupoteza akili za watu na zenye Radha nzuri Kwa wanywao,Kwa maana nyingine tunaambiwa tusimuasi Mwenyezi Mungu Bali tuwe na subira tutayapata hayo yanayo pendwa na nafsi zetu tena yakiwa katika ubora wa Hali ya juu kabisa....hapa Mwenyezi Mungu anajua akili na utashi WA waja wake ndio maana ametumia kanuni ya karoti na fimbo.
Tuje kwenye hoja ya Ugaidi....Uislamu ndio Vita kuu ya tatu ya dunia, wasio Kuwa waislamu wanashtushwa na ukuaji mkubwa wa Dini hii hapa duniani....hivyo wanatafuta kila namna ya kuichafua lkn kamwe hawataweza kwani tayari ilishasemwa katika Maandiko juu ya watu wengi kuingia ktk Uislamu....kwahiyo jinsi wanavyo sambaza propaganda mbaya ndivyo jinsi watu wengi wanavyo usoma Uislamu na kujua ukweli wake....hata Ile ishu ya
Osama alipolipua Kule America ilileta ilileta attention kubwa ya watu na kutaka kujua je Uislamu ni Ugaidi au laa...kinyume chake watu wengi waliujua Uislamu na wakasilimu baada ya kujua ukweli Mashallah.....na ndo hivyo hivyo Kwa huyu bwege,atayafanya watu tena wafunue Qur'an na kuangali je kuna Aya za shetani? Trust me watajionea yaliyomo na kusilimu Kwa wingi.
Hoja je Uislamu ni Dini ya Amani,ni kweli Dini hii ni ya Amani.....na labda nigusie je Uislamu ni nini? Uislamu ni unyenyekevu mbele ya Mwenyezi Mungu mmoja Kwa kufuata maamrisho yake n kuacha makatazo yake....na ndio maana manabii wote walikuwa waislamu, na Dini hii ni kongwe Sana,kuanzia Adam,Nuhu,Yesu mpaka Muhammad,wote hawa waliamrisha KUABUDIWA Kwa Mungu Mmoja Tu na si vinginevyo....kwahiyo Uislamu sio kanzu,kofia na kobazi laa!
Salaam yetu ni ''Amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yako'' hata Yesu nae alisalimia hivyo hivyo na manabii wengine wote na ndio salamu ya peponi hiyo,ukibahatika kuingia utaitumia Sana hiyo.....sasa matumizi ya upanga yamekuja kuondoa udhalimu ambao walikuwa wanafanyiwa waislamu baada ya kuachana na miungu ya kipagani na kuamua kumwabudu Mungu Mmoja,ili haki ipatikane na waislamu wawe salama ilibidi upanga utumike....lkn hawakulazimishwa watu kuingia katika Dini...hata Qur'an imesema hakuna mtu Kulazimishwa kuingia katika Dini na ndivyo ilivyo siku zote.
Nimeona nigusie kidogo mambo hayo baada ya kuona kuna hoja zililetwa hapo.