Nimeona ile stori ya Mwananchi mwenzangu wa Kigoma aliyoandika kuhusu Shule ya Sekondari Buhanda iliyopo Kigoma Mjini kuwa na upungufu wa madawati, ni kweli shule hiyo na nyingine kadhaa hazina madawati na ni changamoto ambayo ipo kwenye shule kadhaa.
Nishee stori moja, kuna Mwandishi wa Habari mkongwe hapa kwetu Kigoma naye alipoona Mwanaye anayesoma katika Shule ya Msingi Mwilamvya iliyopo Halmashauri ya Mji Kasulu akikaa chini darasani kwa zaidi ya mwaka mmoja, akaamua kufanya jambo.
Mwandishi huyo akaamua kumnunulia dawati mwanaye na kulipeleka shule, akaweka chata la jina lake kwenye dawati kwamba “Dawati hili ni kwa hisani ya Familia ya….” kama yanavyofanya mashirika na taasisi mbalimbali wanapotoa msaada shuleni.
Shule ilipokea dawati hilo na kwa muda sasa linatumiwa na mtoto husika pamoja na Wanafunzi wengine wawili, jumla wanakuwa watatu wanaolitumia.
Wanafunzi wengine kadhaa wanaendelea kusoma wakiwa wamekaa chini katika shule hiyo.
Najiuliza hivi kweli Dunia ya sasa Mwaka 2026 ambapo Wanafunzi wanatakiwa kujifunza kuhusu teknolojia mbalimbali, sisi Kigoma tuna Wanafunzi ambao hawana madawati na wanasoma kwa kukaa chini?
Kama hata Shule ya Serikali inashindwa kuwa na madawati, tunategemea shule hiyo inaweza kuwa na Walimu wanaoweza kuwainua kielimu Wanafunzi wao?
Nishee stori moja