Mwandishi wa Habari Luqman Maloto afungua kesi dhidi ya DCI na DPP kisa Tundu Lissu, Azory Gwanda na Ben Saanane

..nashauri uwasiliane na waliofungua kesi ili kuangalia uwezekano wa kujumuisha wahanga wengine kama Dr.Ulimboka.
Si huyu aliye leta mada namwambia au unakuwa msemaji wake
 
Hizo unaweza kufungua wewe kumsaidia Maloto ila ametaja baadhi huenda na hao labda wapo kwenye list yake.

Aliyemuua Mwangosi anajulikana na alipandishwa mahakamani.

Aliyemteka Dr Ulimboka mbona Said Kubenea alimuweka wazi ni mtu wa Magogoni? Na hata Dr mwenyewe alimtambua.

Dr Jwan na Dr Mvungi ni issue za kesi/Ducuments ndiyo zilizowaondoa.
Inaelekea hao sio watanzania ni warundi
 
Mwanahabari Luqman Maloto, amefungua kesi ya jinai No. 5/2023 dhidi ya DCI na DPP Mahakama Kuu, Dar es Salaam, akiiomba itamke ofisi hizo zimeshindwa kuchunguza matukio yaliyofanywa na wasiojulikana ikiwemo kushambuliwa Tundu Lissu, kupotea Azory Gwanda na Ben Saanane.

Chanzo: MwanaHalisi
Awamu hii ya kulipa visasi itakuja kujutia unafiki wa kujifanya ni wajuvi wa siasa na demokrasia.

Kuanzia nywele hadi kucha zitavuliwa kinga ya kung'olewa bila ganzi na kushitakiwa kwa makosa mbalimbali yakiwemo uhujumu uchumi, uhaini na uvunjifu wa haki za biandamu ambazo zinafunikwa kwa sasa sababu ya rushwa
 
Mwanahabari Luqman Maloto, amefungua kesi ya jinai No. 5/2023 dhidi ya DCI na DPP Mahakama Kuu, Dar es Salaam, akiiomba itamke ofisi hizo zimeshindwa kuchunguza matukio yaliyofanywa na wasiojulikana ikiwemo kushambuliwa Tundu Lissu, kupotea Azory Gwanda na Ben Saanane.

Chanzo: MwanaHalisi
Hamna kitu hapo! Ni mbinu za kuziba mdomo wataoongelea madudu ya wahusika na kuwalinda. Kwa kisingizio "kesi iko mahakamani".
 
Matukio ya kupotea, kushambuliwa, kuteswa na kuuawa kwa baadhi ya watu wakiwemo wanahabari, wanasiasa na wasanii, sasa yamekabidhiwa mahakamani baada ya mamlaka zenye dhamana ya upelelezi kushindwa kutoa taarifa za upelelezi wa matukio hayo.

Matukio hayo yamefikishwa mahakamani na mwanahabari na mwanaharakati wa haki za binadamu, Luqman Maloto aliyefungua shauri la maombi ya jinai Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam dhidi Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) na Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP).

Katika shauri hilo namba 5 la mwaka 2023, Maloto pamoja na mambo mengine anaiomba mahakama hiyo itamke DCI anawajibika kwa maisha ya watu aliowataja ambao wamo waliopotea, walioshambuliwa na kuteswa na waliouawa kwa kuwa wajibu wake ni kulinda maisha ya Watanzania.

Maloto amewataja waathirika hao ni pamoja mwanahabari Azory Gwanda na wanasiasa Ben Saanane, Simon Kanguye, Daniel John, Tundu Lissu, Mdude Mpaluka Nyagali maarufu kama Mdude, Leopord Lwajabe, Akwilina Akwilini, Ibrahim Mshana maarufu kama Roma Mkatoliki na Allan Kiluvya.

Pia anaiomba mahakama hiyo itamke DCI ameshindwa ama kwa kutokuwa na uwezo au kwa makusudi kufanya upelelezi kuhusu madhila yaliyowakuta watu hao kutokana na kushindwa kutoa taarifa kwa umma na kwa familia za waathirika hao kuhusu madhila yaliyowapata.

Hivyo anaiomba mahakama hiyo itamke kwamba kuchelewa au kushindwa kukamilishwa kwa upelelezi dhidi yao hakuongozwi na kanuni yoyote na itoe amri dhidi ya DCI kuwasilisha mahakamani hapo taarifa yenye maelezo ya kina kuhusu kupotea, kuuawa na kuteswa kwao, kwa uchunguzi zaidi. Shauri limepangwa kusikilizwa na Jaji John Nkwabi na litatajwa Februari 8 mwaka huu.

Chanzo: Mwananchi
 
Naona bashite akihojiwa ktk mambo mengi kuhusu kupotea kwa watu na kupigwa marisasi kwa 'mtu'
Haki na ikatendeke na wahusika wapate stahiki yao kama walivyofanya kwa hao wengine, ukiua kwa upanga sharti nawe ufe kwa upanga!
 
Kuna wananchi wangapi wanakufa kwa kuuwawa hovyo, nani anafungua kesi kuitaka serikali ikiri kwamba wameshindwa kufuatilia?
 
Mwanahabari Luqman Maloto, amefungua kesi ya jinai No. 5/2023 dhidi ya DCI na DPP Mahakama Kuu, Dar es Salaam, akiiomba itamke ofisi hizo zimeshindwa kuchunguza matukio yaliyofanywa na wasiojulikana ikiwemo kushambuliwa Tundu Lissu, kupotea Azory Gwanda na Ben Saanane.

Chanzo: MwanaHalisi

======

HABARI ZAIDI..

Matukio ya kupotea, kushambuliwa, kuteswa na kuuawa kwa baadhi ya watu wakiwemo wanahabari, wanasiasa na wasanii, sasa yamekabidhiwa mahakamani baada ya mamlaka zenye dhamana ya upelelezi kushindwa kutoa taarifa za upelelezi wa matukio hayo.

Matukio hayo yamefikishwa mahakamani na mwanahabari na mwanaharakati wa haki za binadamu, Luqman Maloto aliyefungua shauri la maombi ya jinai Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam dhidi Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) na Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP).

Katika shauri hilo namba 5 la mwaka 2023, Maloto pamoja na mambo mengine anaiomba mahakama hiyo itamke DCI anawajibika kwa maisha ya watu aliowataja ambao wamo waliopotea, walioshambuliwa na kuteswa na waliouawa kwa kuwa wajibu wake ni kulinda maisha ya Watanzania.

Maloto amewataja waathirika hao ni pamoja mwanahabari Azory Gwanda na wanasiasa Ben Saanane, Simon Kanguye, Daniel John, Tundu Lissu, Mdude Mpaluka Nyagali maarufu kama Mdude, Leopord Lwajabe, Akwilina Akwilini, Ibrahim Mshana maarufu kama Roma Mkatoliki na Allan Kiluvya.

Pia anaiomba mahakama hiyo itamke DCI ameshindwa ama kwa kutokuwa na uwezo au kwa makusudi kufanya upelelezi kuhusu madhila yaliyowakuta watu hao kutokana na kushindwa kutoa taarifa kwa umma na kwa familia za waathirika hao kuhusu madhila yaliyowapata.

Hivyo anaiomba mahakama hiyo itamke kwamba kuchelewa au kushindwa kukamilishwa kwa upelelezi dhidi yao hakuongozwi na kanuni yoyote na itoe amri dhidi ya DCI kuwasilisha mahakamani hapo taarifa yenye maelezo ya kina kuhusu kupotea, kuuawa na kuteswa kwao, kwa uchunguzi zaidi. Shauri limepangwa kusikilizwa na Jaji John Nkwabi na litatajwa Februari 8 mwaka huu.

Chanzo: Mwananchi
Why now
 
Alichosema Luqman ndio hicho alichosema jana Rais Samia
 
Back
Top Bottom