Mwandishi wa Habari wa The Citizen afukuzwa kazi. Kaponzwa na Maoni yake katika mitandao ya kijamii?

Mwandishi wa Habari wa The Citizen afukuzwa kazi. Kaponzwa na Maoni yake katika mitandao ya kijamii?

Hivi unaelewa maana ya public notice?

Ni mjinga pekee anaweza kudhani kampuni itatoa public notice ikijisikia.

Punguza kelele, kumbe hata barua ya kuachishwa kazi hujaiona ila tayari unajua ni ya tarehe gani? Kwa hiyo niamini ramli zako hapa au public notice na tweet ya mwandishi tulizowekewa hapa? Umekalia stori za kufikirika na kurudia rudia post badala utuletee hiyo barua ya termination tuone ni ya lini? Na habari za public notice imewekwa hadharani lini ni wao ndo wameona waiweke siku waliyoiweka sababu wanazijua wao, tupunguze ramli..
 
Mwandishi wa Habari wa The Citizen amesimamishwa kazi. Wengi wanahisi ni kutokana na posts zake katika social media.

View attachment 1396883
Unasema wengi wanasema amefukuzwa kazi kwa sababu ya makala zake. Unaanzisha uzi kwa habari ambayo wala huna uhakika nayo. Huo ni uzushi. Peleleza habari kwanza, upate ukweli wake, ndipo uilete mtandaoni ikiambatana na maoni yako jinsi unavyouona ukweli huo. Hivi sasa unafanya watu waanze kutoa maoni kutokana na hisia zako tu; wengine wakitukana serikali, n.k. Huo ni umbeya.
 
Swali jepesi la kujiuliza, kama alifukuzwa tar 20, kwa nini tangazo halikutolewa tar 20? Uma unakuja kujulishwa tar 23, je huoni kama anaweza kuingia transactions tar 21, 22 na 23 asubuhi kwa kutumia jina la Mwananchi Communication?
Mkuu, unaongea kwa uhakika kabisa kwamba wewe huwa haupitwi na tangazo lolote na kwamba tangazo lolote la tarehe 20 ni lazima tu kwako utalipata tarehe hiyo hiyo? Unapouliza kwa nini hakukutolewa tarehe hiyo, una uhakika kabisa hakukutolewa?
 
Mkuu, unaongea kwa uhakika kabisa kwamba wewe huwa haupitwi na tangazo lolote na kwamba tangazo lolote la tarehe 20 ni lazima tu kwako utalipata tarehe hiyo hiyo? Unapouliza kwa nini hakukutolewa tarehe hiyo, una uhakika kabisa hakukutolewa?

Una taarifa inayoonesha tangazo lilitolewa tar 20?

Maana tuliyonayo humu ni ya Tar 23 saa 6 mchana.
 
kwa misimamo ya huyo mwandishi unadhani kweli tatizo ni hiyo tweet moja tu?fikiria zaidi mkuu. twit hiyo ikupe msukumo zaidi wa kujua twit zake zingine. kabla hujaita watu genge la wajuaji omba kujua,wakati wewe umeona hiyo twit pekee hao wajuaji wameona zaidi ya tweet
Inaweza kuwa kweli kafukuzwa kwa ajili hiyo ila pia tusiamini kuwa ni sababu hiyo pekee iliyomfukuzisha kazi yeye pia ni binadamu yawezekana kuwa kafanya kosa jingine ila anatafuta pa kutokea
 
Naamini khalifa alijianda kwa hili....alijua litatokea kupitia vikao vya tathmini ya mwezi...robo ya mwaka..nusu mwaka au barua za onyo kabisa na pale the citizen wageni walikuwa wengi just three years back

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hyo mtu akisema ukweli mna muona ni ccm?.
mimi magufuli uwa simkubali..
Lakini katika maneno ya siku ile kuhusu corona sijaona kosa lolote.
Mtu kasema "HAKUNA VIFO VILIVYOTOKEA KWA CORONA TANZANIA "

mtu anakuja anapanic.
sasa ulitaka aseme" WATU 100 WAMEFARIKI TANZANIA KWA CORONA WAKATI SIO KWELI".
ni kwamba mnaombea watu wafe au ni nini?.
Mjue nawashangaa.HAMPENDI UHALISIA..
Wewe unafanya nini hapa si uende Chanel 10 au Uhuru ukatoe maoni yako?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hilo tangazo la mwananchi halioneshi kuwa alikuwa mfanyakazi wao linasema alikuwa "contributor" (mchangiaji) wa baadhi ya makala zao na kwa sasa hawataruhusu makala zake.
"Contributor" isingenoga ila MWANDISHI
 
"Contributor" isingenoga ila MWANDISHI
Ilikuwa haina haja ya kuandika uongo. Tafsiri ya "contributor" ni mchangiaji (kimaandishi).

Tatizo siyo tafsiri Bali kusema kafukuzwa kazi. Tuseme eisi tunaochangia kimaandishi hapa JF tukikataliwa na uongozi wa JF (ban) kuweka maandiko yetu ina maana tumefukuzwa kazi na JF?

Tuwe wakweli.
 
Mkurugenzi mkuu wa hiyo media hana confidence na ni opportunist sana.

1585020791414.png
 
Ilikuwa haina haja ya kuandika uongo. Tafsiri ya "contributor" ni mchangiaji (kimaandishi).

Tatizo siyo tafsiri Bali kusema kafukuzwa kazi. Tuseme eisi tunaochangia kimaandishi hapa JF tukikataliwa na uongozi wa JF (ban) kuweka maandiko yetu ina maana tumefukuzwa kazi na JF?

Tuwe wakweli.
Haya ulitaka Kichwa cha Habari kisomeke "Mchangiaji wa magazeti alimwa "Ban" "
 
Back
Top Bottom