Mwandishi wa kampuni ya Mwananchi Communications (MCL), Azory Gwanda apotea. Ni siku 10 na hajulikani alipo

Mwandishi wa kampuni ya Mwananchi Communications (MCL), Azory Gwanda apotea. Ni siku 10 na hajulikani alipo

A country of Democracy & Freedom of speech!
 
Huyo mwandishi wa habari ana kazi gani Kibiti? Kwa maelezo ya mkewe amekuwa anachukuliwa na 'watu' huko Kibiti, sasa swali alikuwa anachukuliwa na nani na alikuwa anapelekwa wapi na kwa kazi gani? KIBITI?

Gazeti la Mwananchi nalo lilikuwa na kazi gani KIBITI?
Kama jeshi lilikuwepo na watoto weng kutekwa na kuwazuia na kuzuia ndugu wazazi kuandamana,kuweka vikao wala kueleza isia zao zaidi kuzui vyombo vya habar kujiingiza katika habar za kibiti ni sahihi,wanaficha nini?
 
Tuzidi kumuomba Mungu asipatikane kwenye Viroba ufukweni mwa bahari..
 
haya mambo ya kutekana tekana yanaichafua sana hii serikali ya Magufuli.
 
Tuwe na utamaduni wa kusoma namba za magari unapohisi jambo lisilo la kawaida. Yaani gari inafika shambani na mmeo ndani ya gari hujisumbui kujua yupo na akina nani, anaulizia funguo za nyumbani ulipoficha unamuelekeza mbele ya watu usiowajua. Hili ni tatizo la wengi. Tujifunze tubadilike.
 
Kwenye gazeti la mtandaoni la The Washington post, kuna habari inayosema mwanahabari Azory Gwanda, 42, wa gazeti la Mwananchi amepotea tangu November 21, 2017 baada ya kutekwa nyumbani kwake huko Kibiti.

Gwanda amekuwa akiripoti taarifa za mauaji ya raia na mabaya kuwahi kutokea huko Kibiti.

Francis Nanai, mkurugenzi wa gazeti la Mwananchi anasema mawasiliano ya mwisho na mwanahabari wao yalikuwa Novembemba 20, na tangu hapo simu zake zote zimekuwa hazipatikani.

Chanzo: Journalist reported missing in Tanzania
 
Alikuwa akiripoti habari gani/matukio gani? kama ni yale ya kutomfurahisha mfalme...kuna walakini
 
Alikuwa akifuatilia habari gani na kwani waanze kuripoti watu wa bara mbali na siyo huku ?
 
Alikuwa akifuatilia habari gani na kwani waanze kuripoti watu wa bara mbali na siyo huku ?
Mkuuu,kwamba umeamza kuiona hiyo habari kwenye Washington post kabla ya taarifa ya mwananchi?.nilichoona mimi kwanza ni taarifa ya mwananchi.
 
Kibiti kuna mengi mazito bado yanaendelea ila hairuhisiwi kuyasimulia wala kuyaripoti. Sasa huyu mwandishi alifanya kazi yake kiuweledi, akasahau kuwa hii ni awamu ya maagizo.
 
Back
Top Bottom