Jiji la Mwanza ni jiji la pili kwa ukubwa na kwa uchumi nchini Tanzania, mfumo wa uchumi wa Mwanza unategemea zaidi private sector, mashirika na taasisi binafsi.
Watu wamekuwa wakijiuliza kama Mwanza ni jiji kubwa kiuchumi na kibiashara kwa nini mapato ya halmashauri ni madogo kulinganisha na mji kama Dodoma?, jibu ni kwamba jiji la Mwanza ni jiji la kipebali mfumo mkubwa wa uchumi haumilikiwi na serikali, mfano vitega uchumi vya halmashauri/serikali ni vichache kulinganisha na Dodoma au miji mingine so halmashuri haina huwezo wa kuvuna mazao mengi sehemu ambayo hawalima vya kutosha, huwekezaji wa serikali kwa jiji kama Dodoma ni mkubwa na ndio maana ata makisio yao ya ukusanyaji wa mapato unakuwa tofauti kati ya sehemu moja na sehemu nyingine, mapato makubwa ya halmashauri ina maanisha serikali imeweka nguvu kubwa huko.
NB: Mapato makubwa ya halmashauri hayamaanishi kuwa uchumi wa mji huo ni mkubwa la asha, kiwango cha uchumi kinapimwa na GDP ndo maana Dodoma na Arusha zimeachwa mbali sana kiuchumi na Mwanza kwa kuangakia vigezo vya kiuchumi.