Mwanza: Mwanamke amuua mama mkwe wake kwa sumu

Mwanza: Mwanamke amuua mama mkwe wake kwa sumu

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,107
Reaction score
160,001
Jeshi la polisi linamshikilia mwanadada NEEMA MWAMBUSI USWEGE(29) mkoani Mwanza kwa kosa la kumlisha mama mkwe wake sumu kwenye chakula na kumsababishia umauti.

Inadaiwa kuwa mama wa JAMES BULAYA (38) bi ANETH MANYIRIZU umemkuta umauti huo tarehe 13/1/2022 saa 12:00 mchana alipopelekwa hospitali baada ya kutapika damu nyingi nakupoteza uhai, bi ANETH MANYIRIZU amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 79 katika hosipitali inayodaiwa siyo ya Serikali.

Hata hvyo uchunguzi wa polisi umethibitisha kuwa NEEMA MWAMBUSI USWEGE ndiye muhusika mkuu kwani watoto wake walitoa maelezo kuwa mama ndiye alimpikia chakula bibi yao na kuwakataza wasije wakathubutu kula chakula kile.

Watu wa jirani wametoa maelezo kuwa ugomvi wao na mumewe ulikuwa ukijirudia mara kwa mara huku mwanamke alikuwa akimjibu mumewe kuwa yeye kwake siyo kituo cha kulelea wazee tofauti na hivyo atarudi kwao Mbeya.

Bwana JAMES ni mfanyabishara mkubwa wa dagaa tz na nje ya nchi amesikitishwa kwa tukio hilo la kufiwa mama yake ambaye ndiye mzazi pekee aliyekuwa amebaki
 
Mauaji yenye sababu za ndoa ndoa yanaendelea.

Mke kaona mama mkwe anamletea kiwingu kwenye ndoa yake kaamua kumuwekea sumu.

Mimi kinachonishangaza vifo vingi vyenye sababu ya kindoa ndoa majina ni ya wakristo tu. Mfano hapo jina neema badala ya kuwa fatuma ama asha

Je waislamu wametuzidi ujanja wapi?

Wao mbona hawaondoani duniani kama sisi.
 
Mume alishapewa onyo akalimezea. Naye anawajibika kwa mauaji haya kwa kiwango fulani.
 
Mauaji yenye sababu za ndoa ndoa yanaendelea.

Mke kaona mama mkwe anamletea kiwingu kwenye ndoa yake kaamua kumuwekea sumu.

Mimi kinachonishangaza vifo vingi vyenye sababu ya kindoa ndoa majina ni ya wakristo tu. Mfano hapo jina neema badala ya kuwa fatuma ama asha

Je waislamu wametuzidi ujanja wapi?

Wao mbona hawaondoani duniani kama sisi.
Wao wanatumia virus wenye uwezo wa kuuwa bila kuacha alama... jocking😅
 
Angekua mchaga kafanya hivyo story zingekua mingi?

Kanda ya ziwa mnasemaje?
Afu tukio hilo ni kuhusu relationship ko haliwezi kuwa story.

Angekuwa mchaga kafanya story zingekuwa mingi Kwa sababu inguhusisha maswala ya pesa na Mali.
 
Mauaji yenye sababu za ndoa ndoa yanaendelea.

Mke kaona mama mkwe anamletea kiwingu kwenye ndoa yake kaamua kumuwekea sumu.

Mimi kinachonishangaza vifo vingi vyenye sababu ya kindoa ndoa majina ni ya wakristo tu. Mfano hapo jina neema badala ya kuwa fatuma ama asha

Je waislamu wametuzidi ujanja wapi?

Wao mbona hawaondoani duniani kama sisi.
Ndoa za Kiislam kwa maoni yangu ni the best practice of matrimonial life.
Hata ukienda mahakamani mashauri mengi ya talaka ni ya ndoa za Kikristo
 
Yaan ni ukatili wa hali ya juu mama wa mume ni sawa na mama mzazi kabisa kaka ilitakiwa mke ajishushe tu ampotezee na amjali maana watu wakizeeka ni wasumbufu unamchukulia kama mtoto tu
Sasa hapo mume hatompenda tena
Kaharibu maisha yake kwa hasira
Halafu mama mwenyewe mzee tu wala hakuwa na madhara.
Angemlea tu bibi wa watu
 
Back
Top Bottom