Mwanza: Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Mbowe na wenzake wanyakuliwa na Polisi usiku wa manane, haijulikani wako kituo gani

Msipende kukuza vitu, mbona hawa watuhumiwa walikuja kwangu na tukanywa chai wote kabla ya kupewa vichapo?
 
Mdude mdomo wake mchafu umefanya watawala wakaanza kuwa madikteta tena

Hali ya uhuru ilikua isharudi vizuri tu yule mdude akamtukana na kumkejeli mama,

Mama ashakasirika ameamua kuwabadilikia

Asante sana mdude mdomo wako umetufanya turudi zama za mwendazake za kuonewa.
 
Unafikiri majukumu au umuhimu wa katiba ni nini hasa?

Sera ni kauli za ujumla zinahitaji commitment na rasilimali kutekelezeka. Kama hakuna namna ya kuwabana wahusika serikalini mtaendelea kupigwa blabla wakati rasilimali wanazielekeza kwingine kwenye maslahi yao hasa.

Bila shaka unajua duniani kote hasa kwenye nchi zenye kuzingatia demokrasia, viongozi wakuu kuanzia Rais huapishwa kulinda katiba kabla hawajakabidhiwa madaraka na wakikiuka vipengele vya katiba hufunguliwa mashtaka hata kuondolewa ofisini kwa njia mbalimbali kwa mujibu wa katiba zao.

Uko sahihi kabisa, Magufuli alikuwa akivunja katiba waziwazi na hakukuwa na mwenye ubavu wa kumuuliza kitu kwa sababu kwa mujibu wa katiba tuliyo nayo amri ya Rais haihojiwi; inatekelezwa tu - ana absolute power. Ukienda kinyume na matakwa yake anaweza kukuchukulia hatua yoyote hata kinyume cha sheria na asiulizwe. Hilo ndilo tatizo kubwa sana la kujadiliwa.

Kwa katiba ya Afrika ya Kusini, Rais mstaafu Zuma yuko jela kwa mujibu wa sheria na bado anakabiliwa na kesi nzito ya ufisadi. Wafuasi wake walioandamana na kuiba wamedhibitiwa na vyombo vya dola na wengi wako ndani wanasubiri hatua za kisheria. Chama tawala cha ANC kinahaha jinsi ya kushughulikia umasikini wa weusi wengi na ufisadi wa viongozi wao serikalini.

Kinahojiwa waziwazi na vyombo vya habari vya ndani na nje ya nchi. Hiyo ndiyo katiba makini. Ya Tanzania kila kitu kiko chini ya Rais na kinategemea utashi, fadhila na huruma yake. Vyombo vya habari vinaelekezwa na Ikulu mambo ya kutangazwa na yasiyotakiwa. Rais asipokuwa mtu wa maana nchi inaenda mrama na hakuna wa kumfanya kitu.
 
Ni kosa kukusanyika na kufanya makongamano ya Chadema,Huko Mwanza na kwingineko walikamatwa watu wengi kwa kuvunja sheria.

Mahakama ndio chombo cha kutafsiri sheria,Je ni lini watu hawa wasioitakia nchi yetu iwe na Amani watafikishwa Mahakamani?

Nguvu ikitumika kubwa vivyo hivo na haki itendeke.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…