Mwanza: Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Mbowe na wenzake wanyakuliwa na Polisi usiku wa manane, haijulikani wako kituo gani

Mwanza: Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Mbowe na wenzake wanyakuliwa na Polisi usiku wa manane, haijulikani wako kituo gani

Nimeona taarifa kuwa Rose Mayemba, katoka Mkoa wa Njombe mpaka Mwanza na kafikia hotel aliyofikia Mbowe, hii inatia shaka, kuna nini? SAA 9 usiku!
Naona wivu umekujaaa sana kisa Mbowe kwani hujui kuwa Mbowe ameoa na anafamilia yake?

Katafute vijana wenzako watakupa unacho kihitaji kutoka kwa mh Mbowe.
 
Wapuuzi tuu hao mtaani maisha Magumu govt inajaribu kuweka mambo sawa hata kama kutakuwa na maumivu kidogo for a while Ili baadae mambo yanyoke ndio mambo mengine ya Katiba yafuate wanaleta dharau

Si mlisema Mmeingia Uchumi wa Kati au zilikuwa Mbwe mbwe tu za Lumumba.
Uchumi gani unaotaka unyooke huu wa kutegemea tozo za miamala.

Vipi zile raslimali mnazosema sisi matajiri tuna raslimali za kutosha sasa inakuaje mtegemee uchumi wa tozo za miamala.
 
View attachment 1861764

View attachment 1861765
View attachment 1861766

Usiku majira ya saa tisa, Polisi walivamia Hoteli aliyokuwa amefikia Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa na wageni wengine pamoja na wenyeji wao.

Waliochukuliwa:
1. Freeman Mbowe
2. John Pambalu
3. John Heche
4. Rose Mayemba
5. Masenya(Mwenyekiti BAVICHA Ilemela)
6. Steven Odipo
7. Dr. Rwaitama
8. Seti (Dereva kanda ya Victoria)
9. Apollo (Afisa Habari Taifa)
10. Frank Novatus (CHASO)
11. Mwakiaba (Mwenyekiti Nyamagana)
12. Benja (BAVICHA Kinondoni)

Mpaka sasa haijajulikana wamechukuliwa kwa kosa gani.

=====

My Take.
Uonevu, uvunjifu wa haki za kiraia, kutoheshimu katiba ya nchi unaendelea kwa kasi katika serikali ya Samia Suluhu Hassan.
Anyway, Aluta continua, uonevu huu utaisha oneday, dawa tutaipata tu.

Nimkumbusha Samia kuwa alikuwepo mtu katika nchi hii anaitwa Magufuli, tulimuita Chuma, Jiwe—Leo yuko wapi?

====

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)

Taarifa Kwa UMMA

Mwenyekiti wa Chama Taifa Mhe..Freeman Mbowe alivamiwa na Jeshi la Polisi hotelini alipokuwa ( Kingdom Hotel) majira ya saa nane na nusu usiku na kumkamata pamoja na viongozi wengine waliokuwa naye.

Viongozi wengine walipelekwa Kituo cha Kati cha Polisi Mwanza,Ila Mwenyekiti Mbowe haijulikani alipelekwa wapi na mpaka Muda huu hakuna taarifa zozote za mahali alipo.
Waliokamatwa ni wafuatao;

1. Mhe .Freeman Mbow
2. Mhe.John Pambalu
3. Mhe. John Heche
4.Mhe. Rose mayemba
5. Masenya( Mwenyekiti Bavicha ilemela)
6. Steven Odipo
7.Dr. Azavel Lwaitama
8. Seti ( Dereva Kanda ya Victoria)
9. Apolinary Appolo (Afisa habari Taifa)
10. Frank Novatus (Chaso Mwanza)
11. Mwakiaba (Mwenyekiti Nyamagana)
12. Benjamin Kambarage ( M.kiti Bavicha kinondoni)

Tunalitaka Jeshi la Polisi kujitokeza na kusema alipo Mwenyekiti wa Taifa na sababu za kumkamata zilikuwa nini.

Tunalaani ukandamizaji huu wa Haki za Watanzania Kwa nguvu zote , na hizi NI dalili za wazi kuwa Udikteta uliokuwepo enzi za utawala wa Rais Magufuli bado unaendelea .

Tutatoa taarifa kadiri ya Muda na jinsi tutakavyozipokea .
Hakuna mwenye akili anaweza kufanya uwekezaji wa maana ktk nchi isiyoheshimu misingi ya haki za binadamu na katiba iliyopo.

SSH na wanaomshauri hawatafika mbali,Jiwe hakuweza huyu ndo kabisa kashindwa mapema kweli
 
Si mlisema Mmeingia Uchumi wa Kati au zilikuwa Mbwe mbwe tu za Lumumba.
Uchumi gani unaotaka unyooke huu wa kutegemea tozo za miamala.

Vipi zile raslimali mnazosema sisi matajiri tuna raslimali za kutosha sasa inakuaje mtegemee uchumi wa tozo za miamala.
Biashara na uwekezaji ulikuwa umedorora kutokana na sera ambazo sio rafiki kama kubambikia kodi,kesi na kupora wafanyabiashara Sasa hizi mambo ndio zinarekebishwa na tayari wafanyabiashara wamerudisha confidence kwa Serikali.
 
Wasimbe hawo wa DJ.
Jaribu kutathimini prominent figure wote wa jinsia ya like waliopo chama Cha nyumbu wa ufipa hybrid ya masaai Mara.
Hakuna mwenye ndoa.
Unaonekana tangu baada ya kifo cha mumeo bado una msongo wa mawazo.

Wewe ni mjane ambaye unahitaji msaada maana hata huna sifa ya kupata urithi kutoka kwa marehemu.
 
Si mlisema Mmeingia Uchumi wa Kati au zilikuwa Mbwe mbwe tu za Lumumba.
Uchumi gani unaotaka unyooke huu wa kutegemea tozo za miamala.

Vipi zile raslimali mnazosema sisi matajiri tuna raslimali za kutosha sasa inakuaje mtegemee uchumi wa tozo za miamala.
Kuwa na rasilimali ni jambo moja na kuzifanya zilete tija ni ishu tofauti, ukweli ni kwamba ni Mataji wa rasilimali japo ndio hivyo hazijawa na tija hadi sasa ila hatua zinazidi kuchukuliwa
 
Back
Top Bottom