Mwanza: Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Mbowe na wenzake wanyakuliwa na Polisi usiku wa manane, haijulikani wako kituo gani

Mwanza: Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Mbowe na wenzake wanyakuliwa na Polisi usiku wa manane, haijulikani wako kituo gani

View attachment 1861764

View attachment 1861765
View attachment 1861766

Usiku majira ya saa tisa, Polisi walivamia Hoteli aliyokuwa amefikia Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa na wageni wengine pamoja na wenyeji wao.

Waliochukuliwa:
1. Freeman Mbowe
2. John Pambalu
3. John Heche
4. Rose Mayemba
5. Masenya(Mwenyekiti BAVICHA Ilemela)
6. Steven Odipo
7. Dr. Rwaitama
8. Seti (Dereva kanda ya Victoria)
9. Apollo (Afisa Habari Taifa)
10. Frank Novatus (CHASO)
11. Mwakiaba (Mwenyekiti Nyamagana)
12. Benja (BAVICHA Kinondoni)

Mpaka sasa haijajulikana wamechukuliwa kwa kosa gani.

=====

My Take.
Uonevu, uvunjifu wa haki za kiraia, kutoheshimu katiba ya nchi unaendelea kwa kasi katika serikali ya Samia Suluhu Hassan.
Anyway, Aluta continua, uonevu huu utaisha oneday, dawa tutaipata tu.

Nimkumbusha Samia kuwa alikuwepo mtu katika nchi hii anaitwa Magufuli, tulimuita Chuma, Jiwe—Leo yuko wapi?

====

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)

Taarifa Kwa UMMA

Mwenyekiti wa Chama Taifa Mhe..Freeman Mbowe alivamiwa na Jeshi la Polisi hotelini alipokuwa ( Kingdom Hotel) majira ya saa nane na nusu usiku na kumkamata pamoja na viongozi wengine waliokuwa naye.

Viongozi wengine walipelekwa Kituo cha Kati cha Polisi Mwanza,Ila Mwenyekiti Mbowe haijulikani alipelekwa wapi na mpaka Muda huu hakuna taarifa zozote za mahali alipo.
Waliokamatwa ni wafuatao;

1. Mhe .Freeman Mbow
2. Mhe.John Pambalu
3. Mhe. John Heche
4.Mhe. Rose mayemba
5. Masenya( Mwenyekiti Bavicha ilemela)
6. Steven Odipo
7.Dr. Azavel Lwaitama
8. Seti ( Dereva Kanda ya Victoria)
9. Apolinary Appolo (Afisa habari Taifa)
10. Frank Novatus (Chaso Mwanza)
11. Mwakiaba (Mwenyekiti Nyamagana)
12. Benjamin Kambarage ( M.kiti Bavicha kinondoni)

Tunalitaka Jeshi la Polisi kujitokeza na kusema alipo Mwenyekiti wa Taifa na sababu za kumkamata zilikuwa nini.

Tunalaani ukandamizaji huu wa Haki za Watanzania Kwa nguvu zote , na hizi NI dalili za wazi kuwa Udikteta uliokuwepo enzi za utawala wa Rais Magufuli bado unaendelea .

Tutatoa taarifa kadiri ya Muda na jinsi tutakavyozipokea .

====

UPDATES:

=====

Jeshi la polisi mkoani Mwanza limefunga barabara ya Bwiru maarufu kona ya Bwiru jirani na ukumbi uliopangwa kufanyia kongamano la Chadema la kudai Katiba, hakuna kinachoendelea kwa sasa polisi wametanda barabara nzima wakiwa na magari na silaha za moto
Yote haya kuzuia watu kujadili Katiba Mpya? Seriously?

Amandla...
 
Akili zenu sijui kama mnawaza sawa sawa.

Hata akitoka Samia, mnadhani ndio mwisho wa matatizo ?

Hamjawajua CCM nyie.

Subirini mkiwekewa MWIGULU au MPANGO tena ndio mtaanza kukimbia kama DIGI DIGI.
Wewe si unalipwa kwa kuchunga ng'ombe wa mwigulu. Unadhani yanayoendelea tz hayatakuhusu. Pole zako.
 
Hivi DJ mbona amekuja kasi sana kipindi hiki cha Mama, anamwonea mama! Anamchukulia poa siyo? Mbowe aache vurugu! Nchi inataka amani na mshikamano!
Amefanya vurugu gani?

Kuwa na kongamano ni dhambi katika nchi ya Tanzânia?

Kwanini ccm wanafanya mikutano lakni hakuna matamko wala kukamatwa je ndio wanaostahiki?

Pingeni vitu kwa hoja na sio kwamabunduki.
 
Hivi DJ mbona amekuja kasi sana kipindi hiki cha Mama, anamwonea mama! Anamchukulia poa siyo? Mbowe aache vurugu! Nchi inataka amani na mshikamano!
Tutumie akili kidogo..Hivi mnyonyaji na mnyonyaji kati yao ni nani usababisha vurugu?!
Je,kudai Katiba Mpya ni vurugu?
Ni sheria ipi inavunjwa pale mwananchi anaposema Katiba au Sheria hii ni mbaya!!
 
2030 nilikuwa natamani January achukue, ila kwa tabia hizi chafu za CDM walizoonesha ndani ya miezi 4 tu ya Samia ni bora achukue Mwigulu aendelee kuwanyoosha watu, watu gani hawana uvumilivu na hawajui hata timing ya kufanya harakati zao. Kwa hili Samia inabidi awaachie polisi na vyombo vya usalama vifanye kazi yao, asiwaingilie. Hawa CDM hawana adabu kabisa na siasa za kistaarabu hawawezi.
CDM wenyewe walitimginya Mambo mama alikuwa mstaarabu na msikivu wakaanza kumchokonoa chokonoa mara wamnyoe sijui nywele gani ka mtangulizi wake, na hawataki subira mbona kipindi Cha magufuli walikuwa wapole hivo, so mama akatafsiri Wana mudharau hawa CDM hufanya viongoz wake so harsh Sana aisee, but hapo mwigulu kuwa Rais aisee atamzidi uovu Magufuli kama viroba vya binadamu wenzake alisema ni wahamiaji haramu Sasa si ndo tutazidi kuumia kuliko jiwe.
 
mwanamke aki react anakuwa mbaya Sana ngoja tuone
CDM walionyesha dharau kwa Samia, imagine aliwafutia Hadi case na dini na akaambia wawe na subira na Tena mikutano ilikuwa inaruhusiwa Sasa wao kumwona mama Yuko fair wakaanza ukaidi na kumdharau kisa mama, Sasa na mama kaamua awanyooshe kidogo.
 
Mbowe alikuwa zake dubai, baada ya kifo tu cha yule jamaa amerudi kwa kasi mno na mikutano kila kona na episodes zisizoisha.....CDM itisheni maandamano ili tozo ziondolewe au itisheni maandano kutusaidia kudai Fao la kujitoa...hapa tutawasaidia kuandamana lakini haya mambo yenu ya Katiba mpya bakini nayo huko huko...

Muda si mrefu TL naye atarudi halafu wataanza kumlaumu mama baada ya kumshukuru wako huru sasa ndani ya nchi yao...TL aliomba ahakikishiwe ulinzi, bila shaka JPM alimhakikishia ulinzi akaja kushiriki uchaguzi baada ya uchaguzi inaonekana ulinzi aliohakikishiwa ukawa haupo tena akaondoka..
Hyo agenda ya katiba ingekuwa na support ya wananchi wangeandamana, Sasa wananchi tu tumevurugwa na makodi mengi mara tozo mara ajira then utuambie katiba unafikiria tutakuelewa. In short CDM waje na agenda zinazogusa wananchi ka tozo, afya na ajira uone ka watakosa support hyo katiba ni janja Yao ya kutaka madaraka
 
Back
Top Bottom