Mwanza: Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Mbowe na wenzake wanyakuliwa na Polisi usiku wa manane, haijulikani wako kituo gani

Mwanza: Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Mbowe na wenzake wanyakuliwa na Polisi usiku wa manane, haijulikani wako kituo gani

View attachment 1861764

View attachment 1861765
View attachment 1861766

Usiku majira ya saa tisa, Polisi walivamia Hoteli aliyokuwa amefikia Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa na wageni wengine pamoja na wenyeji wao.

Waliochukuliwa:
1. Freeman Mbowe
2. John Pambalu
3. John Heche
4. Rose Mayemba
5. Masenya(Mwenyekiti BAVICHA Ilemela)
6. Steven Odipo
7. Dr. Rwaitama
8. Seti (Dereva kanda ya Victoria)
9. Apollo (Afisa Habari Taifa)
10. Frank Novatus (CHASO)
11. Mwakiaba (Mwenyekiti Nyamagana)
12. Benja (BAVICHA Kinondoni)

Mpaka sasa haijajulikana wamechukuliwa kwa kosa gani.

=====

My Take.
Uonevu, uvunjifu wa haki za kiraia, kutoheshimu katiba ya nchi unaendelea kwa kasi katika serikali ya Samia Suluhu Hassan.
Anyway, Aluta continua, uonevu huu utaisha oneday, dawa tutaipata tu.

Nimkumbusha Samia kuwa alikuwepo mtu katika nchi hii anaitwa Magufuli, tulimuita Chuma, Jiwe—Leo yuko wapi?

====

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)

Taarifa Kwa UMMA

Mwenyekiti wa Chama Taifa Mhe..Freeman Mbowe alivamiwa na Jeshi la Polisi hotelini alipokuwa ( Kingdom Hotel) majira ya saa nane na nusu usiku na kumkamata pamoja na viongozi wengine waliokuwa naye.

Viongozi wengine walipelekwa Kituo cha Kati cha Polisi Mwanza,Ila Mwenyekiti Mbowe haijulikani alipelekwa wapi na mpaka Muda huu hakuna taarifa zozote za mahali alipo.
Waliokamatwa ni wafuatao;

1. Mhe .Freeman Mbow
2. Mhe.John Pambalu
3. Mhe. John Heche
4.Mhe. Rose mayemba
5. Masenya( Mwenyekiti Bavicha ilemela)
6. Steven Odipo
7.Dr. Azavel Lwaitama
8. Seti ( Dereva Kanda ya Victoria)
9. Apolinary Appolo (Afisa habari Taifa)
10. Frank Novatus (Chaso Mwanza)
11. Mwakiaba (Mwenyekiti Nyamagana)
12. Benjamin Kambarage ( M.kiti Bavicha kinondoni)

Tunalitaka Jeshi la Polisi kujitokeza na kusema alipo Mwenyekiti wa Taifa na sababu za kumkamata zilikuwa nini.

Tunalaani ukandamizaji huu wa Haki za Watanzania Kwa nguvu zote , na hizi NI dalili za wazi kuwa Udikteta uliokuwepo enzi za utawala wa Rais Magufuli bado unaendelea .

Tutatoa taarifa kadiri ya Muda na jinsi tutakavyozipokea .

====

UPDATES:

=====

Jeshi la polisi mkoani Mwanza limefunga barabara ya Bwiru maarufu kona ya Bwiru jirani na ukumbi uliopangwa kufanyia kongamano la Chadema la kudai Katiba, hakuna kinachoendelea kwa sasa polisi wametanda barabara nzima wakiwa na magari na silaha za moto
Ifahamike kuwa Mh Samia RJMT alisema mikutano ya ndani siyo marufuku...So kwa Imani take ya kidini alikuwa anadanganya?
 
Huu ujinga wenu, fanyieni huko moshi na arusha,

Kwenye raha watu wa Mwanza mnawaita watu wa mwendazake

Ikifika kwenye kuandamana eti twendeni Mwanza

Maanina zenu.
 
Shida Moja ya uongozi wa CCM kila anaewapinga Wao Wanataka kumuua..mtawaua wangapi?? hawachoki kumwaga damu na kufanya siasi safi za ukinzani wa hoja bila kuuwana? Katiba mpya n haki ya msingi kwa Faida ya Kila Mtanzania kwan katiba iliyo saivi ni ya kikoloni yaan Power ya Malkia Kutawala Makolin ndo hiyohiyo alipewa Raisi kutawala Tanganyika..hii sio sawa ili tupate maendelea inatakiwa Hoja za wanachi zisikilizwe kwa mujibu wa Sheria..I wonder Had uyu mama nae kaanza haya mambo hayatamfikisha popote..anaowatuma saivi wakateke badae watamsaliti na kuanza kuvujisha Taarifa muhimu kwa wapinzani Ajifunze kwa Late Jiwe.polen CDM wote
 
Huu ujinga wenu, fanyieni huko moshi na arusha,

Kwenye raha watu wa Mwanza mnawaita watu wa mwendazake

Ikifika kwenye kuandamana eti twendeni Mwanza

Maanina zenu.
Na pia wanataka katiba Mpya kwa tamaa zao za madaraka tu . Hawana muda na shida za wananchi . Japo katiba Mpya ni muhimu, ila kuja kuwapa nchi watu wa aina kama chadema hapana .
 
View attachment 1861764

View attachment 1861765
View attachment 1861766

Usiku majira ya saa tisa, Polisi walivamia Hoteli aliyokuwa amefikia Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa na wageni wengine pamoja na wenyeji wao.

Waliochukuliwa:
1. Freeman Mbowe
2. John Pambalu
3. John Heche
4. Rose Mayemba
5. Masenya(Mwenyekiti BAVICHA Ilemela)
6. Steven Odipo
7. Dr. Rwaitama
8. Seti (Dereva kanda ya Victoria)
9. Apollo (Afisa Habari Taifa)
10. Frank Novatus (CHASO)
11. Mwakiaba (Mwenyekiti Nyamagana)
12. Benja (BAVICHA Kinondoni)

Mpaka sasa haijajulikana wamechukuliwa kwa kosa gani.

=====

My Take.
Uonevu, uvunjifu wa haki za kiraia, kutoheshimu katiba ya nchi unaendelea kwa kasi katika serikali ya Samia Suluhu Hassan.
Anyway, Aluta continua, uonevu huu utaisha oneday, dawa tutaipata tu.

Nimkumbusha Samia kuwa alikuwepo mtu katika nchi hii anaitwa Magufuli, tulimuita Chuma, Jiwe—Leo yuko wapi?

====

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)

Taarifa Kwa UMMA

Mwenyekiti wa Chama Taifa Mhe..Freeman Mbowe alivamiwa na Jeshi la Polisi hotelini alipokuwa ( Kingdom Hotel) majira ya saa nane na nusu usiku na kumkamata pamoja na viongozi wengine waliokuwa naye.

Viongozi wengine walipelekwa Kituo cha Kati cha Polisi Mwanza,Ila Mwenyekiti Mbowe haijulikani alipelekwa wapi na mpaka Muda huu hakuna taarifa zozote za mahali alipo.
Waliokamatwa ni wafuatao;

1. Mhe .Freeman Mbow
2. Mhe.John Pambalu
3. Mhe. John Heche
4.Mhe. Rose mayemba
5. Masenya( Mwenyekiti Bavicha ilemela)
6. Steven Odipo
7.Dr. Azavel Lwaitama
8. Seti ( Dereva Kanda ya Victoria)
9. Apolinary Appolo (Afisa habari Taifa)
10. Frank Novatus (Chaso Mwanza)
11. Mwakiaba (Mwenyekiti Nyamagana)
12. Benjamin Kambarage ( M.kiti Bavicha kinondoni)

Tunalitaka Jeshi la Polisi kujitokeza na kusema alipo Mwenyekiti wa Taifa na sababu za kumkamata zilikuwa nini.

Tunalaani ukandamizaji huu wa Haki za Watanzania Kwa nguvu zote , na hizi NI dalili za wazi kuwa Udikteta uliokuwepo enzi za utawala wa Rais Magufuli bado unaendelea .

Tutatoa taarifa kadiri ya Muda na jinsi tutakavyozipokea .

====

UPDATES:

=====

Jeshi la polisi mkoani Mwanza limefunga barabara ya Bwiru maarufu kona ya Bwiru jirani na ukumbi uliopangwa kufanyia kongamano la Chadema la kudai Katiba, hakuna kinachoendelea kwa sasa polisi wametanda barabara nzima wakiwa na magari na silaha za moto
Hivi wewe hujui mpaka sasa hao watu wamekamatwa kwa sababu gani? Unataka polisi wakufundishe kwa nini Mbowe na wenzake wamekamatwa?
Na hivi miamba Seifu sharifu, Ndesamburo, na mwamba Prof. Baregu wako wapi? Kifo ni yeyote hivyo hakiwezi kuwa adhabu maana kila mtu atakufa.
 
Wote tunapita, kwani huyo mwamba wenu ataishi milele?
Wenzio unaowatetea wanaishi maisha ya kifahar ww sindikiza hapa duniaan ss tunataka katiba mpya coz ni watu na pesa zetu hatutegemei ccm kuendesha maisha kma ww
 
waliokubali ni mataga maana kila alichosema marehemu kwao ilikuwa ni ndioooooooo
Basi kama wewe sio mnyonge,acha fanya kitu uwasaidie hao CHADEMA waliokamatwa na ikiwa huwezi kufanya hivyo basi wewe ni mnyonge tu hapa Tz, maana hata nilisema nizungumzie pesa bado ulikuwa unalia kuhusu tozo.
 
You fought JPM instead of fighting the system. Mambo ni yale yale, CCM itoke!

Mkuu miaka yote CHADEMA imekuwa ikipambana na mfumo wa chama dola (CCM). Bila shaka mwenyewe umeshuhudia madhila na dhahama iliyopitia CHADEMA katika harakati hizo. Kuanzia vipigo, vifungo, mateso, na hujuma kwa makada wake ikiwa ni pamoja na rushwa za pesa na vyeo zilizowahamisha baadhi toka kwenye chama.

Juhudi za kudai katiba mpya zilianza awamu ya nne baada ya kuonekana umuhimu wa kuwa na blueprint ya mfumo unaotakiwa kabla ya kuanza kudai kipengele kimoja kimoja.

Kupambana na JPM awamu ya tano lilikuwa ni suala maalum tu kwani bila simile wala haya alibana kabisa uhuru wa vyama vya siasa kufanya shughuli zao na kuigeuza nchi kuwa virtual dictatorship. Hata CCM kwenyewe mambo hayakuwa shwari. Kila kitu kilikuwa ni yeye tu. Alibomoa mifumo yote ya chama na serikali na kujiweka muamuzi wa kila kitu nchini personally.

Katika mazingira ya aina hiyo, mapambano yoyote ya kisiasa yalionekana kumlenga JPM zaidi. Alishakuwa kikwazo cha ziada.

Sasa wote tunashuhudia kuwa CCM is hell-bent on ensuring the status quo remains solidly. CCM hawataki mabadiliko kabisa. Katiba mpya ndio imekataliwa kabisa hivyo, Wananchi nao wameshatishwa kuangamizwa na vyombo vya dola wakijaribu kuunga mkono harakati za mabadiliko. Na wengi wanaamini katika “kutoboa one day” bila mabadiliko ya mazingira ya kisiasa. It’s a no-win situation for CHADEMA.

Najiuliza safari hii Mbowe na wenzake watakuja na hesabu zipi. I wish them all the best. Very courageous guys in a, unfortunately, terribly docile country.
 
Wqsiojulikana Tanzania wamejijulisha wazi ni wakina nani, poly ccm kwa kunyakua viongozi wa chama usiku wa manane kinyemela bila ya kutoa taarifa yeyote. Polisi wa Tanzania kwa vitendo hivi mnaonyesha wazi jinsi mnavyolinda maslahi ya ccm wazi wazi na kuchafua taaswira ya nchi kidemokrasia. Polisi wamekuwa watekaji sasa si walindaji wa usalama wa raia. Wanachama wa vyama nnje ya ccm hawana haki ya uraia kwenye nchi yao. Je hii ni mbinu ya makusudi ya kuchafua serekali ya awamu hii, ili ilaumiwe kama awamu iliopita? Kwa jinsi hii mheshimiwa Lisu na Lema bakini mlipo tz bado usalama wenu si shwari. Wanaojulikana bado wanaendeleza udhalimu wao.
Kukamata waharifu hadi wawape taarifa

USSR
 
Back
Top Bottom