Uchaguzi 2020 Mwanza: Shule zasitisha masomo, Wanafunzi waambiwa wakampokee na kumsikiliza Mgombea wa CCM Dkt. Magufuli Uwanja wa CCM Kirumba

Uchaguzi 2020 Mwanza: Shule zasitisha masomo, Wanafunzi waambiwa wakampokee na kumsikiliza Mgombea wa CCM Dkt. Magufuli Uwanja wa CCM Kirumba

Katika hali isiyo ya kawaida Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela amesitisha kufunguliwa kwa shule zote hapo kesho ili waalimu na wanafunzi washiriki kampeni za chama Cha CCM

Hali hiyo imesababishwa na chama hicho kukosa ushawishi wa watu kuhudhuria mikutano yake bila kulazimishwa na hali imejionyesha pamoja na kutumia wasanii haijasaidia kitu.

Mgombea wa Urais kupitia Chadema Tundu Lissu aliingia Mwanza kwa kishindo kikubwa wiki iliyopita na kuvuta umati wa watu ambao wachunguzi wa mambo wanasema huenda ukawa umati mkubwa zaidi kutokea jijini Mwanza.

Wazazi kadhaa wamelaani hatua ya kutumiwa ujumbe mfupi na wakuu wa shule kadhaa wa maandishi unaowataka wasipeleke watoto shule kesho.

Wazazi hao wamesema hiyo ni kinyume na kanuni za Tume ya Uchaguzi na inaonekana waziwazi CCM imeamua kukanyaga sheria hizo.
Jf imekuwa kijiwe cha kahawa maana habari hazina vyanzo ndio zinawekwa humu
 
Hawa jamaa kiukweli, waachie tu madaraka hawana jipya tena
 
Mikutano ya chadema imedoda kila Kona ya nchi hii.
 
Ile ya jana ndio mwanza tunayoijua , nyomi from kisesa mpaka town , watu walokuwepo igoma tu ni zaidi ya Lisu mbagala, segerea na kawe [emoji23]na hapo hapakua na wasanii, leo pale kirumba hapatoshi , huku Magu pale Diamond,
 
Acha uzwazwa watu tu waliokuwa wamemsuburi njiani ni zaidi ya waliohudhuria mkutano wa Lissu, subiri kesho dawa iwaingie.
Ni Bahati mbaya sehemu ambazo zinawatia moyo Jamaa akienda anapata watu mara tano ya Lissu, halafu sehemu ambazo Magufuli na CCM wana base, Lisu anaambulia watu wa level ya udiwani, juzi Dodoma uliona
Ni aibu kuzuia shule kufunguliwa ili wanafunzi waende kwenye kampeni.
 
Acha uzwazwa watu tu waliokuwa wamemsuburi njiani ni zaidi ya waliohudhuria mkutano wa Lissu, subiri kesho dawa iwaingie.
Ni Bahati mbaya sehemu ambazo zinawatia moyo Jamaa akienda anapata watu mara tano ya Lissu, halafu sehemu ambazo Magufuli na CCM wana base, Lisu anaambulia watu wa level ya udiwani, juzi Dodoma uliona
Nilijionea kwa macho yangu. Watu wanampenda sana Magufuli. Jana njiani hapakuwa na msanii wala mwanamaigizo lakini watu walikua wengi sana yaani sijui huko kirumba leo itakuaje.
Lissu kama alidhani pale furahisha alipata mafuriko leo aangalie gharika la Magufuli kirumba.
 
Niko wilaya ya Kwimba, takribani sungusungu 1300 kutoka vijiji mbali mbali wamekuwa recruited jana shule fulani ya Msingi, sasa hivi ninavyoongea mabasi yanawapeleka mjini.
 
Uwanja w kirumba hautatosha sijui itakuwaje. WATU TU WALIOJIPANGA KUMPOIKEA MAGUFULI NI MARA KUMI YA MIKUTANO YOTE LISU ALIYOFANYA NCHI NZIMA
 
Wakuu nilisikia jana lkn sikuamini mpaka asubuhi hii nilipoamua kupiga simu kwenye shule mbili za binafsi ambako watoto wangu wanasoma.
Wameagiza hakuna shule leo na watoto waruhusiwe kwenda kwenye mkutano bila uniform.

Wakuu hii maana yake nini?
Kwa nini kulazimisha kwa kiasi hiki?
Ni kweli mikutano ya magufuli ni Muhimu kuliko elimu ya watoto wetu?

Nimesikitika sn kuhusu amri hii haramu.
 
Hao wa njiani huwa wanaandaliwa kabisa. Ni kijiji gani kimaweza kuwa na watu wengi kiasi kile? Kama kweli anakunalika waache uchaguzi uwe wa haki tuone. Tegemeo lenu ccm ni tume yenu ya uchaguzi. Lakini kwenye sanduku la kura hamuwezi.
Acha uzwazwa watu tu waliokuwa wamemsuburi njiani ni zaidi ya waliohudhuria mkutano wa Lissu, subiri kesho dawa iwaingie.
Ni Bahati mbaya sehemu ambazo zinawatia moyo Jamaa akienda anapata watu mara tano ya Lissu, halafu sehemu ambazo Magufuli na CCM wana base, Lisu anaambulia watu wa level ya udiwani, juzi Dodoma uliona
 
Wambie wanao wasiende , na wewe endelea na shughuli zako , hakuna amri wala shuruti , wanaweza pia baki shule wskapiga prepo sku nzima
Daaa.... Nimetafakari sana bado sielewi.... Watoto walikosa masomo sababu ya Corona halafu anakuja mtu anawanyima elimu kirahisi kabisa
 
Wakuu nilisikia jana lkn sikuamini mpaka asubuhi hii nilipoamua kupiga simu kwenye shule mbili za binafsi ambako watoto wangu wanasoma.
Wameagiza hakuna shule leo na watoto waruhusiwe kwenda kwenye mkutano bila uniform.

Wakuu hii maana yake nini?
Kwa nini kulazimisha kwa kiasi hiki?
Ni kweli mikutano ya magufuli ni Muhimu kuliko elimu ya watoto wetu?

Nimesikitika sn kuhusu amri hii haramu.
Thibitisha, mm ni MWALIMU hapa Mbugani S/msingi madarasa yanaendelea.Lakini hazuiliwi MTU kwnd kumsikiliza mkuu wa nchi mahali aliko Karibu.
OVER..
 
Back
Top Bottom