Mwanza: Wawili wauawa kwa kushukiwa Majambazi

Dalton elijah

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2022
Posts
373
Reaction score
829
JESHI la Polisi mkoani Mwanza limethibitisha kuua watu wawili wanaodaiwa kuwa ni majambazi, katika jaribio la kuiba nyumbani kwa mfanyabiashara, wakiwa wamevalia mavazi ya kike kuficha jinsia na mwonekano wao.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Naibu Kamishna (DCP) Wilbrod Mutafungwa, alithibitisha jana kuwa watu hao ambao ni wanaume, waliuawa kwa risasi na polisi waliokuwa katika doria juzi saa 2:45 usiku.
DCP Mutafungwa alisema tukio hilo lilitokea katika Mtaa wa Kabambo, Kata ya Kiseke wilayani Ilemela na watu hao walikuwa wamevalia magauni na vilemba.

Alisema walivamia nyumbani kwa Flora Sungura Abdallah (42) na kuingia ndani wakati mfanyabiashara huyo anafunguliwa geti akitoka kwenye shughuli zake za kibiashara.
“Watu hao walikuwa na bunduki aina ya Shotgun moja iliyotengenezwa kienyeji ikiwa na risasi mbili na mapanga mawili. Baada ya hali hiyo, wakazi wa eneo hilo walipiga kelele za kuomba msaada na taarifa hizo kufika kwa askari polisi waliokuwa doria eneo hilo,” alisema.
Kamanda Mutafungwa alisema baada ya askari kufika eneo la tukio kwa ajili ya kutoa msaada na kuwataka watu hao kujisalimisha, walikaidi amri na kutaka kuwadhuru wakazi wa nyumba hiyo pamoja na askari.
“Ndipo askari walifyatua risasi, hivyo kusababisha watu wawili ambao mmoja alishika bunduki na mwingine akiwa na panga kujeruhiwa kwa risasi hizo na kupoteza maisha papo hapo,” alisema.

Kamanda Mutafungwa alisema miili ya watu hao ambayo haijatambuliwa imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufani ya Kanda Bugando ikisubiri utaratibu wa utambuzi na uchunguzi wa kitaalamu.

Alisema katika tukio hilo hakuna mali iliyoibwa na kuwa jeshi hilo likakamata silaha aina ya shotgun moja, mapanga mawili na begi la mgongoni likiwa na suruali, shati, bisibisi na viatu.

Kadhalika, alisema watu wawili wa jinsia ya kiume wanaodhaniwa pia kuwa majambazi walitoroka kwa kutumia usafiri wa pikipiki ambayo namba za usajili hazijafahamika.
“Tunaendelea na msako mkali wa kuwatafuta watu hao waliokimbia na watu wengine ambao walipanga na kuratibu tukio hilo la kihalifu unaendelea ili kukamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria,” alisema DCP Mutafungwa.
 
Yaani watu wanahisiwa tu kuwa majambazi na kuuawa na polisi.Tunajeshi la polisi la hovyo sana ambalo halifanyi uthibitisho kuwa anayekamatwa kafanya kosa au hajafanya.Jeshi linaongozwa na washamba sana
Uwe unasoma habari kikamilifu na kuielewa na kabla ya kuandika maoni fikiria kwanza,, sio unajiandikia tu....
 
Polisi hawana weledi wa kuthibitisha kuwa watuhumiwa ni majambazi... Most of stories ni fabrications kutoka kwao. Mafunzo ya polisi siku hizi ni kuua na siyo kuzuia na kudhibiti.

Ninawaombea kwa Mungu awapatilize kila askari na kizazi chake kwa kunyofoa roho za watu kila wanapotaka kufanya hivyo
 
Sasa jeshi la polisi litaua wangapi,ujue ukimkamata mshukiwa Kwanza inakurahisishia kiupelelezi,wanaweza kutajanq na kusaidia kupata zaidi ile chain ya hao Criminals.

Pia kila binadamu ana haki ya kuishi kikatiba,iweje jeshi liue?

Tuna watu waoga Sana kwenye majeshi yetu wasio na uwezo wa kuarrest mtu,yeye wepesi wake ni kuua tu
 
Yaani watu wanahisiwa tu kuwa majambazi na kuuawa na polisi.Tunajeshi la polisi la hovyo sana ambalo halifanyi uthibitisho kuwa anayekamatwa kafanya kosa au hajafanya.Jeshi linaongozwa na washamba sana
Duuh!! Umarekani mwingi sana, maelezo hayo yanaridhisha kabisa kuwa walikuwa majambazi bado unalaumu jeshi la polisi. Watanzania tuna kasoro si bure
 
Sasa jeshi la polisi litaua wangapi,ujue ukimkamata mshukiwa Kwanza inakurahisishia kiupelelezi,wanaweza kutajanq na kusaidia kupata zaidi ile chain ya hao Criminals.

Pia kila binadamu ana haki ya kuishi kikatiba,iweje jeshi liue?

Tuna watu waoga Sana kwenye majeshi yetu wasio na uwezo wa kuarrest mtu,yeye wepesi wake ni kuua tu
Nikuache uniue kisa mimi nataka nikukamate ukiwa hai? Au hujasoma vizuri kuwa walichukua hatua gani walipotakiwa kujisalimisha?
 
Yaani watu wanahisiwa tu kuwa majambazi na kuuawa na polisi.Tunajeshi la polisi la hovyo sana ambalo halifanyi uthibitisho kuwa anayekamatwa kafanya kosa au hajafanya.Jeshi linaongozwa na washamba sana
We inaonekana ni ndugu yao unafaidika na huo ujambazi. Sijaona mtu wa hovyo km wewe. Wananchi wapige kelele baada ya kuingia kwa nguvu getini wakiwa na silaha bado badala upongeze jeshi unaandika huu utumbo?
 
Polisi hawana weledi wa kuthibitisha kuwa watuhumiwa ni majambazi... Most of stories ni fabrications kutoka kwao. Mafunzo ya polisi siku hizi ni kuua na siyo kuzuia na kudhibiti.

Ninawaombea kwa Mungu awapatilize kila askari na kizazi chake kwa kunyofoa roho za watu kila wanapotaka kufanya
We ni aibu kwa Taifa
 
Back
Top Bottom