Mwanza: Yaliyojiri Mkutano wa Hadhara wa CHADEMA baada ya kuondolewa zuio la mikutano

Mwanza: Yaliyojiri Mkutano wa Hadhara wa CHADEMA baada ya kuondolewa zuio la mikutano

Muktasari:
Chadema wanafanya mkutano wa kwanza wa hadhara baada ya takriban miaka saba kutokana na zuio la mikutano ya kisiasa iliyowekwa na Rais wa Awamu ya Tano, Hayati John Magufuli mwaka 2016. Zuio hilo limeondolewa karibuni na Rais Samia Suluhu Hassan.
Mwanza. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeipa kongole Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza kwa kukipa ushirikiano kufanikisha mkutano wa hadhara wa chama hicho unaofanyika jijini Mwanza leo.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumamosi Januari 21, 2023, Katibu wa Chadema Kanda ya Victoria, Zakaria Obadi amesema chama hicho kimepokea kwa furaha jinsi uongozi wa Jeshi la Polisi Wilaya za Nyamagana na Ilemela mkoani Mwanza ulivyosaidia kufanikisha mkutano huo unaofanyika viwanja vya Furahisha.

"Kusema ukweli tunawapongeza na kuwashukuru Jeshi la Polisi Mwanza; wametoa ushirikiano unaostahili kwa mujibu wa sheria ikiwemo kuwapokea na kuwapa ukinzi viongozi wetu wa kitaifa wakiongozwa na Mwenyekiti wetu Freeman Mbowe," amesema Obadi

Ameongeza; "Tunaamini viongozi wa Jeshi la Polisi katika mikoa mingine wataiga mfano bora ulioonyeshwa na wenzao wa Mwanza kwa kutimiza wajibu na jukumu la ulinzi na usalama katika mikutano na shughuli za kisasa za vyama vyote kwa haki na usawa kwa mujibu wa sheria,"

Jeshi la Polisi limeimarisha ulinzi kuanzia katika hoteli la kitalii iliyoko katikati ya jiji la Mwanza walikofikia viongozi wa kitaifa na makada wa Chadema.

Pamoja na ulinzi hotelini, askari polisi wakiwa katika magari matatu wameonekana wakiimarisha ulinzi katika msafara wa viongozi wa Chadema wakiongozwa na Mbowe uliokuwa ukielekea eneo la Buhongwa, nje kidogo la jiji la Mwanza yanakofanyika mapokezi rasmi kabla ya kwenda viwanja vya Furahisha kuhutubia mkutano wa hadhara.

Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika ameiambia Mwananchi kuwa pamoja uzinduzi wa mikutano mingine itayaofanyika maeneo mbalinbali nchini, mkutano wa leo pia ni sehemu ya kumbukizi ya miaka 30 tangu Chadema iliposajiliwa rasmi mwaka 1993.

Picha zaidi
View attachment 2490192
20230121_162517.jpg
 
Watu wanabidi kuwa , Wachache ili tusibanane mtoa Mada hauna hoja f*c*y
 
gongo ndio imekulea hadi leo umekuwa polisi
na umpeleki segerea life is not fair
Polisi mnamaisha gani? mnakufa masikini kwa kuwatetea wanyang'anyi!
Chorus
Peperusha bendera
ViVa ROMA ViVa
Bendera x4

verse III

Hakuna mtoto asiye na mzazi yupi wa serikali ya tatu?
mikataba iweke wazi demokrasia ni watu,
ona sasa kila msomi anaikimbilia siasa,
nchi itajengwa na nani? ajira imekuwa serious!
Wanafanya biashara haramu bado hawalipi kodi
nani atahoji na hao ndio wadhamini wa bodi?
Jasho analila mzungu wachimbaji wadogo wa migodi
au mnataka Ivan aje awe mfuasi wa panyaroad?
Pesa starehe za Muungano hamzingatii itifaki
wanafunzi mnawachoma jua na shule hawana madawati
mnalipa mishahara hewa, na hamlipi mafao walimu
na mlimpiga Warioba alivyowaletea Rasimu!
Nchi inalima pamba nyinyi mmeua viwanda
tunauzia wawekezaji ona dola inapanda
Tunageuka waagizaji kisha wanatuuzia mitumba
uchumi unayumba leta fujo upigwe kama Lipumba!
Nakutabiri nani afuate? Karibu Tanga kunani...
Huku hatuitaji kakakuona wala pweza wa ujerumani
Round hii kombe linaenda Monduli?(Masai yelo subhai...
Au kombe ni la Magufuli?
Kama kawa kama dawa, Je kombe linabaki Ukawa?!
Mmarekani anataka wese(we hakuna atakaye pona)
na Mchina akifuata gesi? mwambie Nangwanda sijaona.

Tunataka picha mdogo wangu. Kuanza kuangalia Youtube nzima ni matumizi mabovu ya bando
 
Back
Top Bottom