Mzee Mohamed amejifunga kwenye simulizi za kidini tu. Na kueleza jinsi dini ilivyodhulumiwa na wajanja,..kumbe sio kweli walikuwa wajanja. Walikuwa wasomi wa miaka ile.
Ili story yake iwe na mashiko, angeweza klubalance, ili waja waiangalie vizuri
Rogo...
Naamini unakusudia historia ya Waislam unaposema "kidini."
Umesema kweli.
Nilipogundua kuwa historia ya uhuru wa Tanganyika imeandikwa sivyo niliamua lazima niitafiti na kuiandika ili isipotee.
Historia ya uhuru wa Tanganyika ni historia ya Waislam na Waislam.
Hakuna namna unaweza kuitenganisha historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika Waislam.
Ukithubutu kuwatoa Waislam katika historia hii utabakia huna historia ya ukombozi wa Tanganyika na utakuwa huna pia historia ya mashujaa waliopigania uhuru wa Tanganyika.
Ukiwaondoa Waislam utabakia na Julius Kambarage Nyerere peke yake.
Matokeo yake utakuwa huna majina ya waasisi wa African Association 1929.
Utakuwa huna majina ya waasisi wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) 1933.
Utakuwa huna majina ya TAA Political Subcommittee 1950.
Utakuwa huna jina la Mufti Sheikh Hassan bin Ameir kama kiongozi wa Waislam wa Tanganyika.
Utakuwa huna majina ya Abdulwahid na Ally Sykes, Hamza Mwapachu na Dossa Aziz.
Utakuwa kwa upande wa masheikh huna majina ya Sheikh Suleiman Takadir, Sheikh Mohamed Yusuf Badi, Sheikh Said Chaurembo, Sheikh Abdallah Rashid Sembe.
Kwa upande wa wanawake utakuwa huna majina ya Bi. Titi Mohamed, Bi. Tatu bint Mzee, Bi. Halima Khamis, Bi. Chiku bint Said Kisusa, Bi. Hawa bint Maftah, Bi. Sharifa bint Mzee, Bi. Halima Selengia, Bi. Amina Kinabo na wengine wengi.
Hawa wote niliowataja hapo juu walikuwa mstari wa mbele katika TANU.
Kabla sijaandika kitabu hiki: "The Life and Times of Abdulwahid Sykes, (1924 - 1968) The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism,"(1998) majina hayo hapo juu hayakuwamo katika historia ya TANU.
Historia ya TANU yote iligeuzwa kuwa historia ya Julius Nyerere.
Hivi ndivyo historia ya kweli ya TANU na historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika ilivyopotea.
Historia hii iliyopotea leo imepatikana.
Sasa historia ya uhuru wa Tanganyika na historia ya Nyerere inasomwa upya.
Kuwa kuna watu hawapendi historia kusomeshwa na kufahamika hii ni bahati mbaya kwao.