Mzee hao wawili waliokujibu mwanzo mwenye Id inayoanzia na J na mwingine M usiwe unawajibu ni wana chuki na uislamu kupindukia mpaka wanatia kinyaa,
Hao ndio ukiona mijadala ambayo itagusia uislamu hata kwa asilimia moja tu basi watakuja kutukana na kudhihaki uislamu au mtu anayeonekana kuwa na vinasaba vya kiislamu..ushauri wangu kwako usiwe unawajibu hao wanaonekana hata kwao hakuna heshima,imagine mtu umemoa hadi andiko kuthibitisha ulichomwambia then anakwambia ni muongo..tabia ya hovyo sana hii
Tadpole,
Ahsante sana kwa ushauri wako.
Hawa ndugu zetu wawili na wengine mfano wa hao wala wasikushughulishe.
Ukiona mtu anaegemea kwenye kejeli na matusi jua tayari ushamshinda.
Kichwa chenye hoja hakiwi na nafasi ya tusi au kejeli.
Muhimu ni kwenda na yeye hivyo atakavyo yeye bila ya wewe kurejesha tusi au kejeli dhidi yake.
Hapa ndipo penye ushindi.
Kejeli au matusi yake ndiyo kichocheo cha kusomesha zaidi historio ya kweli.
Kusomesha zaidi ndiyo kuelimisha zaidi.
Kuelimisha watu kuhusu ukweli wa historia ya uhuru wa Tanganyika na mchango wa Waislam ndicho kinachoniweka mimi hapa JF.
Tubakie kwenye kambi hii na hawa ndugu zetu.
Nimeweka hapa uzi mpya: ''Historia ya Kadi ya TANU.''
Tuwasubiri tuwasikie watakuja na yapi:
Wanamjua ni nani alisanifu kadi hii na kuchapisha kwa fedha zake?
Jina lake anaitwa Ally Kleist Sykes.
Kadi yake ya TANU No. 2.
Baba yake Kleist Sykes ni katibu muasisi wa African Association 1929.
Wanamjua aliyechukua kadi za TANU na kwenda nazo Rufiji kutafuta wanachama wa kwanza wa TANU?
Jina lake anaitwa Said Chamwenyewe.
Anajua nani alikuwa anaziuza kadi hizi misikitini?
Mufti Sheikh Hassan bin Ameir.
Kosa kuandika historia hii?
Tuchukulie kuwa wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika Kadinali Rugambwa angekuwa bega kwa bega na Nyerere kupigania uhuru na Kadinali Rugambwa angekuwa anauza kadi za TANU ndani ya St. Joseph's Cathedral wangekubali historia hiyo kufutwa?