Mwasisi wa TANU, Shushushu anayetajwa kufanya kazi na mashirika 8 ya Kijasusi duniani

Huyo jamaa alikuwa jasusi kama Ali Tambwe ?
 
Hongera sana
 
Mzee Mohamed amejifunga kwenye simulizi za kidini tu. Na kueleza jinsi dini ilivyodhulumiwa na wajanja,..kumbe sio kweli walikuwa wajanja. Walikuwa wasomi wa miaka ile.
Ili story yake iwe na mashiko, angeweza klubalance, ili waja waiangalie vizuri
 
Pole kaka,kuna watu hawajui kuwa hoja hujibiwa na hoja ni sio mitusi
 
Kuna wahuni humu Mzee.
Usitumie nguvu kushindana nao.
 
Sikua namjua mzee said mpaka leo hii.Nyuz zake hapa jF sikuwahi muwa nazichukulia kwa uzito kabisaa hasa kwakua zimejifunga kwenye dini zaidi kitu ambacho sionagi mantik yake nut honestly umeni impress sana kwa hiyo brief history yako ya maisha binafsi
 
Date...
Hakuna dini kama mafunzo (doctrine).

Naeleza historia ya jamii yangu na sisi ni Waislam vipi tuliathirika na ukoloni wa Mjerumani na Mwingereza.

Naeleza tuliyofanya katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

Historia hii haikuwapo kabisa.
Ndiyo nikaamua kuitafiti na kuiandika.

Ikiwa wewe unajihisi vibaya kusoma historia ya African Association iliyojaa waasisi Waislam au historia ya Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika ilivyotoa viongozi wa TANU na wanachama wake hii ni bahati mbaya kwako.

Swali la wewe kujiuliza ni kwa nini historia hii ilifutwa historia ya TANU ikageuzwa kuwa historia ya Julius Nyerere peke yake?
 
Uko sahihi mzee wangu na wala sina shida na historia ya jamii yako naomba usinielewe vibaya ila tu nasema sijawahi kuwa napendelea kuzifuatilia kwa kuzisoma kwakua hazijawa zikinihusu sana (na nadhani sio kosa kutokua interested na some stuffs)..
Hapo kwenye Tanu kuwa Nyerere pia sina comment pia.

All in all kazi nzuri
 
Mzee Mohamed amejifunga kwenye simulizi za kidini tu. Na kueleza jinsi dini ilivyodhulumiwa na wajanja,..kumbe sio kweli walikuwa wajanja. Walikuwa wasomi wa miaka ile.
Ili story yake iwe na mashiko, angeweza klubalance, ili waja waiangalie vizuri
Rogo...
Naamini unakusudia historia ya Waislam unaposema "kidini."

Umesema kweli.

Nilipogundua kuwa historia ya uhuru wa Tanganyika imeandikwa sivyo niliamua lazima niitafiti na kuiandika ili isipotee.

Historia ya uhuru wa Tanganyika ni historia ya Waislam na Waislam.

Hakuna namna unaweza kuitenganisha historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika Waislam.

Ukithubutu kuwatoa Waislam katika historia hii utabakia huna historia ya ukombozi wa Tanganyika na utakuwa huna pia historia ya mashujaa waliopigania uhuru wa Tanganyika.

Ukiwaondoa Waislam utabakia na Julius Kambarage Nyerere peke yake.

Matokeo yake utakuwa huna majina ya waasisi wa African Association 1929.

Utakuwa huna majina ya waasisi wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) 1933.

Utakuwa huna majina ya TAA Political Subcommittee 1950.

Utakuwa huna jina la Mufti Sheikh Hassan bin Ameir kama kiongozi wa Waislam wa Tanganyika.

Utakuwa huna majina ya Abdulwahid na Ally Sykes, Hamza Mwapachu na Dossa Aziz.

Utakuwa kwa upande wa masheikh huna majina ya Sheikh Suleiman Takadir, Sheikh Mohamed Yusuf Badi, Sheikh Said Chaurembo, Sheikh Abdallah Rashid Sembe.

Kwa upande wa wanawake utakuwa huna majina ya Bi. Titi Mohamed, Bi. Tatu bint Mzee, Bi. Halima Khamis, Bi. Chiku bint Said Kisusa, Bi. Hawa bint Maftah, Bi. Sharifa bint Mzee, Bi. Halima Selengia, Bi. Amina Kinabo na wengine wengi.

Hawa wote niliowataja hapo juu walikuwa mstari wa mbele katika TANU.

Kabla sijaandika kitabu hiki: "The Life and Times of Abdulwahid Sykes, (1924 - 1968) The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism,"(1998) majina hayo hapo juu hayakuwamo katika historia ya TANU.

Historia ya TANU yote iligeuzwa kuwa historia ya Julius Nyerere.

Hivi ndivyo historia ya kweli ya TANU na historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika ilivyopotea.

Historia hii iliyopotea leo imepatikana.

Sasa historia ya uhuru wa Tanganyika na historia ya Nyerere inasomwa upya.

Kuwa kuna watu hawapendi historia kusomeshwa na kufahamika hii ni bahati mbaya kwao.
 
Faana,
Makala hiyo inatokana na paper aliyoandika James Brennan msomi maarufu wa historia na mjuzi wa historia ya Tanzania.

Toa shaka kuwa alichaondika hakina ithibati:





Articles

“The Secret Lives of Dennis Phombeah: Decolonization, the Cold War, and African Political Intelligence, 1953–1974”​

James R. Brennan
Pages 153-169 | Published online: 16 Jun 2020
 
Inahitaji iwe na kitabu chake kabisa hii
 
Kwa udini alionao…. Hatakusaidia sana kwasababu ‘star’ wa habari yako anaitwa Denis

Angeitwa ally or Abdul ungepata mengi
 
Mpe heshima yake jasusi wetu

Achana na perepete za Yvonne mzee wangu
 
Mzee anza na ziara za Uarabuni Sasa. Picha na makfiri wa kizungu zimetosha Sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…