Mwathirika mkuu wa ndoa kwa Sasa ni mwanamke! Tubadili Sheria tufunge ndoa za mikataba muolewaji alipwe pesa kulingana na mkataba!

Haswaa! Wawili mkikubaliana kuoana kwa mkataba iwe miaka tano,kumi itakuwa rahisi kuendelea na hiyo ndoa sababu mtakuwa mmejuana vilivyo na kama mtu ana kisirani atajuwa hapa baada ya huu mkataba basi ndoa inaisha, lakini mkihesshimiana baada ya miaka 5/10 basi mnaweza kuona uwezekano wa kuurudia mkataba mpya muongeze miaka mingine kama ile ya mwanzo lakini kwa tahadhari kubwa.
 
Hao unaowazungumzia ni wale wa manzese na tandale pale mtaa wa fisi Rudi nyuma fikiria kuhusu wadogo zako wa kike na watoto zako wa kike!
 
Wakiolewa kwa mikataba si ndo watakuwa vyombo rasmi vya starehe!?
#KATAANDOA
 
Wanawake wanajidhalilisha wenyewe kwa kuyageuza mahusiano chanzo Cha mapato ya kiuchumi
 
Watu kama hawa wanaowaza kama Wanawake ndio wanaotutungia sheria za ajabu ajabu.

Kwa hiyo wanaolelewa kwa maelezo yako wakifukuzwa, wakidhalilishwa, wakidhihakiwa ni sawa kisa ni Wanaume?

Ila Mwanamke ni sawa?
Ndio maana Vijana wanakataa Ndoa.
 
Huwez pata nguvu ya kudai mkataba wkt unachoofa kwny mahusiano Ni ngono TU.

Mwanamke productive kwny mahusiano hata kumuacha au kumnyanyasa lazima ujistukie Maana behind your success Kuna mkono wake.

Msitutafsiri vibaya,
Wanaume hatuna roho mbaya kiivyo
 
Hao unaowazungumzia ni wale wa manzese na tandale pale mtaa wa fisi Rudi nyuma fikiria kuhusu wadogo zako wa kike na watoto zako wa kike!

Huwezi pingana na nature, na hizi propaganda hazifiki popote, tutendaaa weee tutafika hapa

Isaya 4:1
"Na siku hiyo wanawake Saba watamshika mtu mume mmoja wakisema, tutakula chakula chetu na kuvaa nguo zetu wenyewe, lakini tuitwe tu Kwa jina lako, utuondoe aibu yetu"

Saizi mtasema ooh ndoa ni kifungo mara ooh ndoa inamgandamiza mwanamke lengo mkitaka wanaume waoane wao kwa wao na wanawake wao Kwa wao kwasababu mahusiano ya mwanaume na mwanamke ambayo ndio asili mnyapinga Kwa nguvu zote kwa kutoa changamoto zilizoko huko lakini kiuhalisia aibu ya mwanamke inafichwa na mwanaume utake usitake hakuna mwanamke ataridhika nje ya mwanaume hata angekuwa na uwezo wa namna gani tamaa yake iliwekwa Kwa mwanaume, mtaongeaa weeee lakini huo ndio ukweli na utabaki hivyo. Itafika kipindi wanawake Saba watahitaj kuolewa na mwanaume mmoja achana na hii ya wanawake wanne au mwanamke mmoja, Tena hawatahitaj mahar kwa mwanaume, hawatakimbilia mahakani kudai matumizi ya watoto,🤣🤣🤣 "ndoa is there to stay shauri la Mungu litasimama" save hiyo
 
Muoane wanaume kwa wanaume ili kukata mzizi wa fitina
Wanawake mmeumbwa Kwa ajili yetu waache hao kufaidi Yale Mungu aliyaweka Kwa mwanamke,waswahili wanasema "fuata nyuki ule asali" Kuna kawimbi ka vijana wa hovyo kameibuka wao wanataka asali tu maumivu ya nyuki hawataki haiko hivyo Sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…