Nyie MATAGA mkipewa mbinu ya kupambana na majanga makubwa mnaleta jeuri na kibri siyo?
Haya kuna mwenzenu humu amekata tamaa japo alitoa hadi video na kuhamasisha.
View attachment 1469976
Halafu na nyie watu wa I.T ndiyo nini kutujazia mazagazaga hivyo mezani? Hamjui kuwa yanaonekana kwenye video?
View attachment 1469977
Mimi sioni kosa la waziri biashara ya Utalii ita pick up pole pole huwezi kutegemea kesho watalii wajae Tanzania dunia siyo Tanzania peke yake kuna nchi zingine pia zinaangalia soko hilo hilo.
Cha kufanya kwanza ni kuondoa hofu kwa watalii kwamba Tanzania si salama alafu ni kuwashawishi kupitia vivutio vyetu kwamba watafaidi kile wanachotarajia kutoka kwetu value for money.
Tusiogope mbuga zetu haziozi, fukwe tuzitunze, tamaduni tuzifufue ningependa kuona ikulu ya Dodoma ikiwa na jengo la Tembe jee unakumbuka nyumba za wagogo? Pale mlangoni askari wanaopokea wageni wavae zile shuka za wagogo na katambuga. Tuharakishe SGR ianze kazi na ikiwezekana tujenge SGR nyingine Dar, Tanga, Moshi, Arusha mpaka Musoma watalii watasafiri kwa urahisi na kwa bei nafuu, watakuja kwa wingi tu.
Tufufue utalii wa uvuvi deep sea fishing hasa Baracuda kule Mafia na Pemba, kuna soko kubwa sana hasa kutoka ujerumani na watalii wa deep sea fishing huwa wanakaa muda mrefu mpaka mwezi mmoja. Tungalie uwezekano wa kuanzisha utalii wa retired na senior citizens kule Lushoto kuna hali ya hewa nzuri, utulivu na usalama.
Ile kauli ya waziri Kigangwala kuweka Cable cars mlima Kilimanjaro ilikuwa kosa la jinai. Hizo cable cars apeleke Usambara Mountains kule aweke vivutio mlimani ajenge restaurants, Casinos, night clubs atavutia watalii wengi. Siwezi kuongea yote kwa leo.