Watu wanashindwa kuelewa kitu kimoja "Biashara ya Utalii sio kitu kinacholeta Faida kwa Nchi husika tuu,la hasha!"
Kwa Wakuu mnaofahamu sector hii mtakua mnajua Travel Agent,Ikiwa 90% ya watalii wote wanakuja kupitia Travel Agent basi ina maana mtalii anaanza kuacha hela kwao kwanza kabla ya kufika nchi husika...hapo hapo kuna Ajira,nk.
Secta ya anga inategemea utalii kwa kiasi kikubwa,leo hii mashirika makubwa ya ndege yako chini,Bei ya mafuta imepungua na uzalishwaji umepunguzwa..ili mashirika haya yainuke ni lazima Utalii Uamshwe....
Tusije tukajidanganya kwamba ni sisi tuu ndo wenye Kiu ya hyo pesa ya utalii ,Hata wao Wataimiza Wananchi wao Wafanye Spending ili kodi ipatikane,Na utalii ni spending inayoaminika kuwapa faraja watu wa Magharibi pindi watokapo kwenye matatizo.
Km unajua majira ya mwaka ya ulaya Utagundua ni Summer ndio iko mbioni kuingia na hapo huwa na joto kali sana,na msimu wa joto ni kitu cha kitamaduni kusafiri,na pia kutafuta ahueni ya ubaridi.
Wakuu it is matter of time Kigwangalla atakula mavuno yake...ulaya wanafungua mipaka yake 16/6...