Mwenezi Makonda Amtimua Mkurugenzi wa Nkasi Kwenye Mkutano Baada ya Wananchi Kumlalamikia

Mwenezi Makonda Amtimua Mkurugenzi wa Nkasi Kwenye Mkutano Baada ya Wananchi Kumlalamikia

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
66,537
Reaction score
75,687
Paul Mkaonda aendeleza moto wa kuwashughulikia Watendaji wababaishaji.

Zamu hii amemtimua kwenye Mkutano Mkurugenzi Mtendaji wa Nkasi Baada ya Wananchi wengi Kumlalamikia Kwa madai mbalimbali.

Makonda: Mwaka huu mtaota nywele 😆😆.

Kazi iendelee 👇👇

View: https://youtu.be/9xYY1I5CxU8?si=nQs8d_rgnMpEideN
 
Makonda amethibitisha tuhuma husika?, ok, amemfukuza mkutanoni na si kazi. Baada ya Makonda kupita ilistahili kuwe na kikosi kazi kinachothibitisha tuhuma na kupima mizania ili asionewe mtu, ccm tusishabikie tu alimradi tukaja kuonea baadhi ya watu.
KIDUMU CHAMA MAKINI CHAMA CHA MAPINDUZI.
 
Makonda amethibitisha tuhuma husika?, ok, amemfukuza mkutanoni na si kazi. Baada ya Makonda kupita ilistahili kuwe na kikosi kazi kinachothibitisha tuhuma na kupima mizania ili asionewe mtu, ccm tusishabikie tu alimradi tukaja kuonea baadhi ya watu.
KIDUMU CHAMA MAKINI CHAMA CHA MAPINDUZI.
Wao watatoa ripoti Kwa mamlaka husika na mapendekezo hivyo Kuna watu wataondoka alisema hata yeye juzi kule Mpanda.

Mwisho DED amesema madai anayajua ila Sasa Kwa nini hajalipa? Wao Wana Mapato ya Ndani Kwa nini wasitenge pesa za kuwalipa awamu kwa awamu kuliko kuwapiga chini mazima?

Na kumbuka pesa za Vituo vya Afya, Elimu nk zilikuja fixed. Kwanini majengo Yao yaishe ila pesa ya fundi isiwepo? Nina ushahidi wa watu wanayodai.

Ingekuwa ni madai ya Wakandarasi tungesema Serikali kuu inahusika ila Hawa local fundi ni Halmashauri.
 
Nimesoma hiyo clip ikihusu somo hilo hapo juu. Kwa kweli nimesikitika sana na kuhuzunika. Nchi hii inaendeshwa kisheria na kwa utawala bora kwa nini vitendo kama hivyo vinafanyika na Mamlaka imekaa kimya. Makonda ana mamlaka gani kumtimua Mkurugenzi kwenye kikao na kama alikuwa na kosa kwa nini uchunguzi usifanyike kwanza ndo hatua zikachukuliwa. Wananchi kulalamika ndicho cha kufukuzwa HAPANA. Hivi Mkurugenzi ni nswereable kwa Makonda?. Mhe. Waziri wa TAMISEMI lawama zote zitaelekezwa kwako. Nchi haiendeshwi hivyo.
 
• Watumbuliwe tu, CCM imeoza hiyo hakuna kiongozi wa maana,

• Ikiwezekana viongozi wa CCM wote wachomwe moto.
 
Huyu DED ana kigugumizi balaaa inaweza kuwa Ulemavu wake wa kutamka maneno umemponza. Lkn all in all ni kimeo sana huyu Mwalimu arudishwe akafundishe vidudu.
Huwa najiuliza Kada ya Ualimu ni Zoa Zoa hata kama huwezi kuongea una Kithembe au Kigugumizi wanazoa tuu mfano mzuri ni huyu.
 
Back
Top Bottom