Mwenge: Ni Mwanga Tu Au Kuna Uvumba Fulani Unafukizwa Ili Kupumbaza Watanzania? Is it Justified?.

Wakati tunatafakari hilo, tujiulize pia ile Fimbo ya Malkia na Mwenge wa Olympic ambavyo vyote hutembezwa sehemu mbalimbali Duniani na hapa kwetu vimeshafika mara kibao, je vina uvumba? Au malengo yake ni nini?
Yaleyale tu inabidi nayo tuyashangae kama wanavyoshangaa mwenge wetu
 
Wakati tunatafakari hilo, tujiulize pia ile Fimbo ya Malkia na Mwenge wa Olympic ambavyo vyote hutembezwa sehemu mbalimbali Duniani na hapa kwetu vimeshafika mara kibao, je vina uvumba? Au malengo yake ni nini?
Ukistaajabu ya Mussa utayaona ya Firauni. Vyote ni upuuzi na chanzo chake ni iman potofu
 
Mkuu Pascal,

Mwenge wa Uhuru ni ALAMA RASMI YA TAIFA ya UHURU kama ilivyo bendera.

Kiufundi ni sawa na uvumba wa kanisani maana ni lazima ufukizwe kuleta baraka kanisani na waumini na waso waumini.

Au pia ni sawa na UDI ufukapo mahala kuashiria faragha kubwa.

Lakini Mwenge wa UHURU ni alama rasmi na maalum kwa taifa kama ulivyo mwenge wa OLYPMPIC ambao ulianzia huko Ugiriki.

Hivyo kila mahala upitapo hufukiza na kukumbusha kwamba Tanzania ni nchi huru na itaendelea kuwa huru mpaka mwendawazimu mmoja atakapoamua kubadilisha hii desturi.

Na akifanya hivyo atakuwa amekiuka maadili na desturi yetu watanzania ya kuukimbiza MWENGE wa UHURU.

Tofauti haipo kwani sisi twtaumia mafuta kila mara na ule wa OLYMPIC watumia mafuta na kuwaka kwa muda wa dakika 10.
 
Sikuwahi kabla kushuhudia mwenge wa Uhuru hasa mkesha, mwaka huu nikasema nijisogeze nione kuna nini.

Tangu Siku ile najikuta nimeanza kuwa MTU wa hovyo hovyo tu.
Mi kwasababu najuaga ni nini,wamenishindwaga kunifanya bwege
 
Vitu vingi ambavyo vipo kimkakati huwa ni vigumu kuvielezea na ni vigumu kila kichwa kikaona umuhimu wake.
Ujumbe wa uliomo kwenye maelezo ya sababu za kuwashwa kwa mwnge huu kwa mara ya kwanza,ni sala adhimu kwa Watanzania kuwa wanaiadhimisha na kujitathimini kama nchi. Ujumbe wa mwenge hutoa ripoti tosherevu kwa serikali inayosaidia kuleta matumaini pale ambapo hakuna matumaini, upendo palipo na chuki, heshima palipo jaa dharau dharau, na umoja palipo na utengamano. Hayo yote ni mambo muhimu kwa usalama wa taifa letu.
Huku kuwa wamoja si bure ni kwa sababu ya hii sala yetu iayozidi kutuunganisha. Vijana wengi wanaobahatika kushiriki tukio hili kwa ngazi yoyote ile huwa wanapata hisia za kizalendo na kuwa hazina kwa taifa lao. Hapa taifa linakuwa kama limewaweka jandoni vijana wake. Huwa wanashirikiana na kupendana huku wakiimba nyimbo za hamaza za kulipenda taifa lao. Pia hotuba za viongozi husaidia kuamsha ari za wanachi kujikomboa kiuchumi, na kijamii.
Uliyoyafanya enzi hizo hukuanzia kwenye mwenge kutumia fursa hizo. Hata kwenye mbina mbalimbali huko kwenu maarufu kama chagulaga ndiko ulikojifunzia kutumia fursa hizi. Hilo ni athari za malezi yetu si kwasababu ya mwenge.
 
Msororo69, Uhuru wa mtu haupo kwenye kijingi cha moto...Uhuru ni hisia ndani ya mtu na uhalisia wa mazingira yanayomzunguka. Leo ndio nimesikia kuwa Mwenge upo kimakakati.

Mwenge unasaidia kuleta MATUMAINI pasipo MATUMAINI: Hakika ungenipa mfano wa matumaini ambayo Mwenge unaleta ungesaidia wengi sana. Neno tumaini si jepesi kulielewa mpaka ukutane na mtu aliyepoteza tumaini. Nikikupa mfano, yupo yule aliyetafuta uzazi kwa ujana wake wote, hadi sasa yu mtu mzima na ameingia kwenye ule umri ambao hatarajiwi tena kushika ujauzito. Kwake huyu, tumaini kwake ni kusikia kuwa yupo Mungu ambaye alimpa Sara mtoto akiwa Bibikizee. Je kuna ulinganisho wa hali hiyo kuhusu Mwenge?

UPENDO PALIPO NA CHUKI: Hapa tunahitaji mifano na sio ngonjera za kale na mashairi. Nchi hii imejaa migongano na mikwaruzano. Mwenge unapita kila mwaka, nyuma yake ng'ombe wanakula mazao ya mkulima na kadhalika na kadhalika.

Mchelea mwana kulia, hulia mwenyewe. Vijana wa leo sio wa mwaka 47. Hotuba ya kiongozi ni 'hotuba ya kisiasa', hakuna hotuba iletayo ari ya kujikomboa kiuchumi bila kuwapo na mipango. Mwenge haufanyi mipango. Mwenge unazindua yaliyopangwa na kutekelezwa.

Ukitaka kujua kuwa Mwenge hauna mipango, jiulize kwa nini hatukuuona Mwenge ukizindua FLYOVERS za Dar es Salaam au SGR
 
mbio za mwenge wa Uhuru zimekuwa zikijalalisha upigaji wa Mali ya umma na pia kupiga kampeni zisizo rasmi na ndio maana JPM anasita kuzifuta.
 
Asante sana ndugu Pascal kwa andiko lako, limenifanya nifikirie zaidi kuhusu umuhimu wa mwenge karne hii. Hata kama kweli una umuhimu "sijui kuunganisha makabila 128 ya Tanzania", nadhan kutumia gesi kuwasha mwenge ni moja ya kutangaza rasilimali zetu, na kuhamasisha matumizi ya health and environmental friendly resources.
Watafiti waje, je twaweza kuwasha mwenge kwa gesi??
 
Miradi inayofunguliwa na mwenge ni ile iliyoibuliwa na wananchi na kuichangia kisha kuongezewa na kumaliziwa na halmashauri zao. Kijiji au mtaa ambao mradi wake ukichaguliwa kuzinduliwa na mwenge hufurahi sana kwa kuwa mradi wake utakamilika kwa wakati.
Mengine niheshimu maoni yako kwakuwa hiyo ndio imani yako na hayo ndio wewe yanakupa matumaini na amani.
 
Miradi inayofunguliwa na mwenge ni ile iliyoibuliwa na wananchi na kuichangia kisha kuongezewa na kumaliziwa na halmashauri zao. Kijiji au mtaa ambao mradi wake ukichaguliwa kuzinduliwa na mwenge hufurahi sana kwa kuwa mradi wake utakamilika kwa wakati.
Mengine niheshimu maoni yako kwakuwa hiyo ndio imani yako na hayo ndio wewe yanakupa matumaini na amani.
 
Ni Maushirikina (Imani isiyo na Tija)
Yenye Asili ya sehemu moja ya Nchi,
Kwa nguvu ya Mtu fulani akamua kuya-'practice'
Na kuyarithisha kama sehemu muhimu ya
Ya Utamaduni wa Nchi.
Madaraka bwana....
 
Vyema kwa ufafanuzi.
Ila hayo ni yatokanayo na mnazodai ni matunda ya Hilo li-dude lenu,
Umewahi kuchimba na kujua Asili yake?
Sio mwanzo mlipoambiwa utawekwa juu kuangaza? Na kama hoja ni kuangaza Kwanini sasa unarandaranda? Tujiongezage jamani.
 
Mwenge ni kichocheo cha maendeleo na miradi iliyolala kwa muda mrefu katika maeneo yetu hapa Tanzania, Mwenge unaweza kuhamasisha na kuchochea ukarabati wa barabara ambayo ili sahaulika miaka hata mitano iliyopita.

Swali la kujiuliza hapa ni je bajeti ya uendeshaji wa Mwenge inatoka wapi? binafsi sijawahi sikia Bunge linapitisha bajeti ya ukimbizaji mwenge, hili ni swali ambalo uwa hatulipi ufafanuzi wa kutosha.
Hakika na kubaliana na Paskali kuwa Mwenge ni kichocheo kikubwa cha maambukizi mapya ya VVU, niliwahi kufanya coverage ya mwenge wakati fulani nilichokiona ni kufuru, tunahitaji mbinu mpya za kuenzi kitu kinachoitwa mwenge, nadhani hayo yalikuwa ni mawazo ya Mwl. Nyerere kwa nyakati hizo, lakini kufanya mabadiliko kwa zama hizi wala si dhambi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…