Mwenge: Ni Mwanga Tu Au Kuna Uvumba Fulani Unafukizwa Ili Kupumbaza Watanzania? Is it Justified?.

Mwenge: Ni Mwanga Tu Au Kuna Uvumba Fulani Unafukizwa Ili Kupumbaza Watanzania? Is it Justified?.

Wanabodi,

Hili ni swali tuu najiuliza kuhusu hizi mbio za Mwenge wa Uhuru zinazoendelea sasa. Kwenye Mwenge kinachokimbizwa nchi nzima, jee kweli ni ule mwanga tuu ili kumulikia na kuangazia, au ni ule moshi mzito mweusi kana kwamba kuna dawa fulani za uvumba zinazonyunyuziwa kama ubani, kisha zinatumika na Mwenge kuwafukiza Watanzania ili kuendelea kuwapumbaza ili waendelee....(naomba nisimalizie).

Rais Magufuli alipoingia tuu madarakani na kufuta maadhimisho ya sherehe muhimu kama ya Uhuru kwa hoja kuwa hazi justify the cost for spending so much kwenye sherehe tuu huku hospitali zetu zikikosa madawa na wagonjwa wanalala chini kwa ukosefu wa fedha. Moja kwa moja nilidhania kuwa sasa huu ndio utakuwa mwisho wa kuzungusha kwa Mwenge wa Uhuru. Lakini hali haikuwa hivyo.

Hivyo hili ni swali kwa wenye ufahamu wa ndani kuhusu huu Mwenge, tuelezane ukweli jamani. Kinachozungushwa ni Mwenge lakini the essence ni ule mwanga tuu wa kumulikia au ni ule moshi unaofukizwa kama vile umetiwa mavumba fulani kuwapumbaza Watanzania?!.
.
Kama Tanzania tunataka maendeleo ya kweli ni lazima tuwe very serious kwa kuachana na kuendekeza matukio stereotype na kumaitains positions ambazo ni redundancies just to maintain a status quo, kwa vile zilikuwepo! .

When are we gonna change? . Yaani kwa Magufuli huyu aliyefuta sherehe za Uhuru lakini ana maintain mbio za Mwenge, huu Mwenge una nini haswa? . Tuelimishane jamani!.
Jumatano njema.
Paskali
update.
Forojo Ganze (Master), mchawi maarufu aliyeanzisha Mwenge wa Uhuru
Paskali huyu jamaa huwa anakurupuka kwenye maamuzi anayofanya sabb hapakuwa na ulazima wa kufuta sherehe ya uhuru wakati huo anahudhuria sherehe inayotuletea hasara WaTz. Mwenge kwa sasa hauna faida zaidi ya kutumia rasilimali fedha pasipo na ulazima na wakati huo ukichochea maambukizo ya ukimwi katika baadhi ya maeneo ambayo kunakuwa na mkesha. Vilevile una sura ya kichama hasa CCM na nakumbuka mwaka 1994 wakati nipo Shule moja ya sekondari huko Dar wanafunzi waligoma kuchangia mafuta kwa maelezo kuwa mwenge ni wa CCM ndipo ikatoka amri ya RC ambaye alikuwa kati ya Mary chipungahero almaaruuf Mama Chips au Hayati Mtoto wa hapa hapa Ukiwaona Ramadhani Mwinshehe Athmani Ditopile Mzuzuri ya walimu kutembeza viboko kwa wale wasiochangia wakidaiwa ni wapinzani. Kwa muktadha huu hakuna namna lazima Magu afikiri tena peke yake maana yeye ana akili kuliko watz wote kama kuna haja ya kuendelea na sherehe hizi za kuwapumbaza Watz
 
Wanabodi,

Hili ni swali tuu najiuliza kuhusu hizi mbio za Mwenge wa Uhuru zinazoendelea sasa. Kwenye Mwenge kinachokimbizwa nchi nzima, jee kweli ni ule mwanga tuu ili kumulikia na kuangazia, au ni ule moshi mzito mweusi kana kwamba kuna dawa fulani za uvumba zinazonyunyuziwa kama ubani, kisha zinatumika na Mwenge kuwafukiza Watanzania ili kuendelea kuwapumbaza ili waendelee....(naomba nisimalizie).

Rais Magufuli alipoingia tuu madarakani na kufuta maadhimisho ya sherehe muhimu kama ya Uhuru kwa hoja kuwa hazi justify the cost for spending so much kwenye sherehe tuu huku hospitali zetu zikikosa madawa na wagonjwa wanalala chini kwa ukosefu wa fedha. Moja kwa moja nilidhania kuwa sasa huu ndio utakuwa mwisho wa kuzungusha kwa Mwenge wa Uhuru. Lakini hali haikuwa hivyo.

Hivyo hili ni swali kwa wenye ufahamu wa ndani kuhusu huu Mwenge, tuelezane ukweli jamani. Kinachozungushwa ni Mwenge lakini the essence ni ule mwanga tuu wa kumulikia au ni ule moshi unaofukizwa kama vile umetiwa mavumba fulani kuwapumbaza Watanzania?!.
.
Kama Tanzania tunataka maendeleo ya kweli ni lazima tuwe very serious kwa kuachana na kuendekeza matukio stereotype na kumaitains positions ambazo ni redundancies just to maintain a status quo, kwa vile zilikuwepo! .

When are we gonna change? . Yaani kwa Magufuli huyu aliyefuta sherehe za Uhuru lakini ana maintain mbio za Mwenge, huu Mwenge una nini haswa? . Tuelimishane jamani!.
Jumatano njema.
Paskali
update.
Forojo Ganze (Master), mchawi maarufu aliyeanzisha Mwenge wa Uhuru
Dhamira ilikuwa ni Njema ya kuzimulika sehemu zote za Tanzania Kimaendeleo nadhani kwasasa wamesha Imulika Tanzania nzima huu Mwenge Hautakiwi ikimbizwe kila mwaka ni Matumizi mabaya ya Peza za Walipa Kodi
 
Tambiko hilo ,ndio maana una miiko..yake
Kwanza wakimbiza mwenge hutafutwa kwa makini..na huapa.

Wakati wa kulaza mwenge lazima...ufunikwe na wahusika ni wakimbiza mwenge kitaifa
Wakati wa kuongeza mafuta pia wanaufunika na.wahusika ni hao tu
 
Mkuu Pascal,

Mwenge wa Uhuru ni ALAMA RASMI YA TAIFA ya UHURU kama ilivyo bendera.

Kiufundi ni sawa na uvumba wa kanisani maana ni lazima ufukizwe kuleta baraka kanisani na waumini na waso waumini.

Au pia ni sawa na UDI ufukapo mahala kuashiria faragha kubwa.

Lakini Mwenge wa UHURU ni alama rasmi na maalum kwa taifa kama ulivyo mwenge wa OLYPMPIC ambao ulianzia huko Ugiriki.

Hivyo kila mahala upitapo hufukiza na kukumbusha kwamba Tanzania ni nchi huru na itaendelea kuwa huru mpaka mwendawazimu mmoja atakapoamua kubadilisha hii desturi.

Na akifanya hivyo atakuwa amekiuka maadili na desturi yetu watanzania ya kuukimbiza MWENGE wa UHURU.

Tofauti haipo kwani sisi twtaumia mafuta kila mara na ule wa OLYMPIC watumia mafuta na kuwaka kwa muda wa dakika 10.
Kuna...ukweli kuwa ipo siri inawezekana ..hata wapinzani siku wakishika dola wataendelea .baada ya kujua hayo maagano

Kuna rafik zangu wamepata kuniambia...uwepo...wa..siri fulani na matambiko ya kitaifa ambayo kila rais anayeingia anatakiwa kufanya

Inadaiwa Mkapa alikuwa mgumu kidogo ..na kilichomtokea yeye mwenyewe akapatwa na mstuko...ndani ya muda mfupi...alipata majanga mfululizo kama mv bukoba na msafara wake kuingiliwa na...lori bovu ambalo hata sweepers hawakuliona.....yule dereva hakuwahi shitakiwa...kwa uhaini kama..ilivyo kwa kuingilia msafara wa rais na..kutaka kimgonga.....

Baada ya pale...inadaiwa...alikubali kufanya...tambiko na toka hapo hakupata tena misukosuko....


Wakati wa..MV BUKOBA...marais wastaafu Nyerere na Mwinyi walimfuata Mkapa kuteta naye ..ikulu ya Mwanza.
 
Nasisitiza CCM ifanye utafiti, wakimbiza mwenge wa uhuru ni wangapi wako hai mpaka hii leo na hali za afya zao zikoje, kama waliugua, waliugua nini, na walianza kuugua muda gani tangu wamalize mbio za mwenge?.

Bila utafiti wa kina, people may think this is joke, tulifundishwa kuhusu kuvuta hewa ya carbon, au kuvuta moshi wowote tuu, ndio maana kuvuta sigara kwenye public, kumepigwa marufuku maeneo mengi duniani ili wasiovuta sigara, wasiathiriwe na ule moshi wa wanaovuta sigara, sasa just imagine, kama moshi tuu wa sigara, unamdhuru yule wa jirani asiyevuta, vipi kuhusu huu moshi mnene, mzito wa mwenge, hao wanaovuta kila siku hali zao zikoje?.

Kwenye somo la baiyolojia tuliwahi kufundishwa kuvuta moshi wowote, una hewa ya carbon iliyochanganyika na carbon monoxide ambayo ina sumu inayoua taratibu.

Nimeukumbuka uzi huu, baada ya kupokea taarifa za kifo cha kiongozi huyu

View attachment 636895

TAARIFA YA AWALI:


Wadau nimepata taarifa muda huu zinasema mbunge wa Songea mjini Mh. Leonidas Gama hatunaye tena....

UPDATE:

JamiiForums imepata uthibitisho wa taarifa za kifo cha Mhe. Gama ambacho kinadaiwa kutokea muda wa Saa 6 kuelekea Saa 7 usiku wa kuamkia leo.

Amefariki akiwa mbunge wa Songea Mjini na amefariki dunia usiku wa kuamkia leo hii Songea katika Hospitali ya Peramiho.

Gama amewahi kuwa mkuu wa wilaya ya Muheza, Nachingwea, Newala, Mbeya na Ilala. Vilevile amewahi kuwa mkuu wa mkoa Kilimanjaro.

Inadaiwa marehemu Gama alianguka nyumbani kwake saa saba usiku juzi huko Likuyu; akapooza upande wa kushoto akawa hajitambui kabisa na akapelekwa Hospitali ya Peramiho ambako aliwekewa mashine za kumsaidia kupumua.

Mungu ailaze roho ya Marehemu Mahali pema peponi.
Alikuwa ni kiongozi wa mbio za mwenge miaka ya nyuma.

RIP Leonidas Gama.

Paskali
 
Wakati tunatafakari hilo, tujiulize pia ile Fimbo ya Malkia na Mwenge wa Olympic ambavyo vyote hutembezwa sehemu mbalimbali Duniani na hapa kwetu vimeshafika mara kibao, je vina uvumba? Au malengo yake ni nini?
Wenzako wanajitosheleza wao kwanza kwa mambo muhimu halafu mwenge ndo unafuata kama kujifurahisha tu.
 
Nipe Elim Kuhusu Hili Ili Nielimike Na Mim
Huyu Forojo Ganze,alikuwa ni mmoja kati ya wazee waliotumwa kufanya zindiko la nchi baada ya uhuru kule bagamoyo, walipewa kazi ya kuhakikisha rais aliye madarakani hapingwi na mtu yeyote(Mwl.Nyerere), zindiko hilo lilifanyika bagamoyo ktk moja ya mashimo yanayopatikana wilayani hapo,zoezi hilo lilienda sambamba na kumuuliza shetani na malaika zake ni jambo gani lifanyike ili Tanzania iendelee.
Forojo Ganze ndiye mtu pekee aliyeingia ktk hilo shimo kwaajili ya kuuliza, alikaa huko kwa muda wa siku 10 huku akiwa amewaacha wenzake nje wakimgoja atakuja na jibu gani ili wakampatie rais na wazee wa Dar es salaam,kilichoshangaza siku ya kumi na moja alitoka akiwa hoi hajiwezi akiwa kama mtu aliyepigwa na alikuwa anaongea lugha isiyofahamika,wenzake wakiwa wanaongozwa na Yahaya Hussien walimbeba hadi ikulu Dar es salaam na walipomfikisha mbele ya mwalimu Nyerere alitamka maneno hayo yanayohusu mwenge kwa kiswahili kisha akanyoosha juu mkono wake wa kulia ambao tayari ulikuwa umeandikwa namba hii 115,kisha akakata roho.
Baada ya mazishi mwalimu aliyafanyia kazi maneno ya Forojo Ganze akaanzisha mwenge wa uhuru bila kujua ulikuwa na maana gani, baada ya hapo aliwagiza yahya Hussein atafasiri maana ya ile namba 115, kama kawaida ya shehe Yahaya alitafasiri akamwambia kuwa namba hiyo inamaanisha "utakufa ukiwa na umri wa miaka 77 na taifa la Tanzania kwa kipindi hicho litakuwa na umri wa miaka 38.
Hii inamanisha ukichukua 77 umri wa mwalimu jumlisha 38 umri wa taifa utapata 115, na hii ndivyo ilivyokuwa, mwaka 1999 mwalimu alikufa akiwa na miaka 77 na taifa lilikuwa na miaka 38 ya uhuru (77+38=115) pia utamaduni wa rais kuongea na wazee wa Dar es salaam unaendelea hadi sasa na wamekuwa na maamuzi ya kitaifa na husikilizwa sana wanachokisema,mbona haijawahi kutokea rais akaongea na wazee wa bukoba jambo la kitaifa?,zindiko la bagamoyo linafanya kazi.
Safu hii ilikuwa ya watu 5 ambao ni.
1. Mzee Ramadhan, alizaliwa mwaka 1920,
2. Ally Tarazo(1929),
3. Komwe wa Komwe(1918),
4. Sheihe Yahya Hussein(1925),na
5. Forojo Ganze (1902)
 
wakati fulani nikiwa bukoba niliwahi kukutana na mkimbiza mwenge mmoja mkongwe.

nilimuuliza maswali kadhaa ya ndani kabisa kuhusu mwenge. hakuwa na hiyana, alinipa majibu.

katika majibu yake aliniambia kuna mchanganyiko fulani wa madawa ya kishirikina ambayo yanawekwa katikati ya ule mwenge.

hakutaka kuendelea sana...ila niligundua mwenge una uhusiano mkubwa sana na ushirikina, matambiko na makafara makafara mbalimbali.

kuna siri kubwa katika mwenge.
 
Nasisitiza CCM ifanye utafiti, wakimbiza mwenge wa uhuru ni wangapi wako hai mpaka hii leo na hali za afya zao zikoje, kama waliugua, waliugua nini, na walianza kuugua muda gani tangu wamalize mbio za mwenge?.

Bila utafiti wa kina, people may think this is joke, tulifundishwa kuhusu kuvuta hewa ya carbon, au kuvuta moshi wowote tuu, ndio maana kuvuta sigara kwenye public, kumepigwa marufuku maeneo mengi duniani ili wasiovuta sigara, wasiathiriwe na ule moshi wa wanaovuta sigara, sasa just imagine, kama moshi tuu wa sigara, unamdhuru yule wa jirani asiyevuta, vipi kuhusu huu moshi mnene, mzito wa mwenge, hao wanaovuta kila siku hali zao zikoje?.

Kwenye somo la baiyolojia tuliwahi kufundishwa kuvuta moshi wowote, una hewa ya carbon iliyochanganyika na carbon monoxide ambayo ina sumu inayoua taratibu.

Nimeukumbuka uzi huu, baada ya kupokea taarifa za kifo cha kiongozi huyu


Alikuwa ni kiongozi wa mbio za mwenge miaka ya nyuma.

RIP Leonidas Gama.

Paskali
Swali hili bado ni valid.
P.
 
Back
Top Bottom