Mwenye historia ya Nabii Mwamposa kabla ya kuanza huduma yake

Hahaha...hatari sana, nani hajawahi kumuona? kwa nini usimuone wakati anapanda hadharani? Mwamposa hubaki na watu anaowawekea mikono na kuwaombea na humzonga mpaka mlangoni anapoingia garini.
 
Lakini akiwa Mwanza alifafanua vyote hivyo kwa mistari ya biblia
Sio kufafanua anatafuta justification kupitia mistari ya biblia najua atakimbilia ule mstari unaosema waweke mafuta juu ya wagonjwa n.k

Lakini issue ni kwamba injili ya kweli ni Ile inyaoongelea mtu kwenda mbinguni. Haiwezekani mtu anaita mpagani anampa mafuta tu anamuacha aende bila kumfanyia Sala ya Toba, bila kumbatiza, Sasa kama sio faida yake kiuchumi unadhani ufalme wa Mungu una gain Nini kupitia huduma yake? Anaweza kweli kusema anasaidia Roho zifike mbinguni au anaacha watu waendelee kupotea gizani yeye anawapa mafuta tu imetosha.
 
Mkuu huduma ya uimbaji inaingia wapi ?
 
Nimetafakari kwa kina juu ya jibu lako, ila ni kipimo hicho tu pekee ndiyo kumpima na kuja na hoja ya kuwa si mtumishi wa Mungu?
Huo ni mfano tu basic wa kimwili ila kiroho zaidi mtumishi wa Mungu ana focus kuokoa Roho za watu kwenda mbinguni sio kupata magari na majumba huku Yuko gizani.

Ni lini umewahi ona Mwamposa anajombea watu wajazwe Roho Mtakatifu?

Lini Mwamposa amebatiza?

Lini Mwamposa ameongoza Sala ya Toba mpagani kabla ya kumuombea?

Nimemsikia anasema eti Yesu ni dhehebu zote, huo ni uongo na utapeli, Yesu anakutambua Pale unapookoka na kufuata mafundisho yake. Hauwezi ukawa unauza bangi alafu uende kwenye mafuta eti upokee muujiza then uendelee kuuza bangi!! Hii Sio sawa, Jesus is interested na way kuokoka sio kupata magari huku wameasi.
 
Kuna shuhuda nyingi ukifatilia vizuri niza uongo tena uongo mkubwa. Na wanao zitoa wako trained kabisa kwa ajili ya hiyo kazi.

Ukiwa na akili kama za bata huwezi elewa ila ukifatilia vizuri mtiririko wa shuhuda na matukio yaliyomo utaelewa.
Shuhuda nyingine za Mwamposa kweli zinatatiza. Nyingi ni physical na si spiritual.

Utasikia mtu katapika/kanya kufuli lililofungwa kumaanisha kuwa alifungwa na wachawi sasa kafunguliwa, mara katapika wembe, uzi, sindano.... Yaani kama mazingaombwe tu.
 
Nilichogundua kinachokusumbua ni wivu..pia unasikiliza sana story za vijiweni..mimi pia nilikua na mentality kama yako..ila niliamua kufuatiria mahubiri yake..kiukweli jamaa anahubiri watu waache dhambi.

#MaendeleoHayanaChama
Umewahi ona anajombea watu wajazwe Roho Mtakatifu? Ni lini amefundisha watu kuacha dhambi waende mbinguni? Umewahi ona anaenda kubatiza maelfu wanaokuja kwenye mikutano yake??

Yule ni tapeli tu anatafuta Hela kupitia madhabahu na hao walishaongelewa kwenye Mathayo 24 pamoja na Ufunuo na wathesalonike 2 so sio ajabu kuona mnachotwa na miujiza mkiamini ni Yesu..
 
Ila ingekuwa katoliki wangetangazwa kuwa watakatifu ili mradi wamefia kanisani. Hakuna kanisa lenye usanii Kama katoliki na mapadre wao walawiti
Mie sio mkatoliki so siwezi zungumzia mambo Yao ila nachozungumzia Mimi ni kwamba lile tukio la kusababisha mauti kwa maksudi kabisa lilitosha watu kumuona hafai.
 
Duuh nakoaea kubishana na wewe.
Mimi ninaongelea kutotumia vitu wewe unasema neno.
Baki na Mwamposa wako mkuu tafadhali
Jamaa hajakuelewa anapenda ubishi bila tafakuli maana yako nimeielewa kama sijakosea kwamba Sawa Yesu na mitume walitenda miujiza ila ilikuwa haijirudii maana funuo huwa zinabadilika leo yaweza kuwa ya maji kesho majivu au chumvi ila sio mazoea na miujiza haifanyiki kila siku maana ni ukuu wa Mungu usio zoeleka...
Nikosoe au Nielekeze nisipoelewa please.
 
Ndugu upo vizuri sana, asieelewa ni mkaidi tu
 
Hayo ni kweli lakini Yale SIO mafuta ya upako ni mafuta yanayotengenezwa kwa formula za kushirikina.
Na zinajukana . MTU yeyote anaweza kuyanunua Kwa maustadhi na yanafanya KAZI Kwa Hiyo SIO upako Wa Kikristo Bali ni mchanganyiko Wa mitishamba kama Dawa nyingine za kisuna. KUWADANGANYA watu Kuwa ni upako Wa Roho Wa MUNGU ni kupotosha na kumwandolea MUNGU sifa za Upekee.

Natamani kuwaambia ukweli Wakristo wenzangu mana wamepotoka sana. Uliona Mashekhena ubwabwa wameenda kumuunga mkono Nabii Mkuu . Ni Muislam Gani anayekubali Kuwa kuna Nabii mwingine baada ya Nabii Mohamad (SAW)? Wale ni wataalam Wa Dawa za Kisuna wanajua Kuwa zipo Dawa za Kisuna na za majini zinazotumiwa kutibu Kwa uwezo Wa Allah MTU akapona mana Kila kitu alikiumba yeye na akaumba Dawa za Kila Ugonjwa Katika miti aliyoiumba ?


Nikuulize Swali ?

Hiví Unaonaje kama Madaktari Wa Muhimbili wangesema Kuwa tunatibu Kwa Jina la Yesu ! Njooni Juma Pili mlete wagonjwa wenu WOTE waliovuniika miguu ,wenye matatizo ya macho tuna macho ya KIROHO,macho ya upako Yaani miwani. Wakati huo binadam wawe hawajapata elimu Juu ya sayansi rasmi ya tiba ? Je, watu wasingefurika Muhimbili nakujua Kuwa ni Imani ya Kikristo kutibu Kumbe ni sayansi ya Kigiriki na Kirumi ?

Kwa Sasa Imani zimegubikwa na Sayansi ya Kale ya MISRI .
Wayahudi wamegubikwa na Sayansi ya Kimisri ikiwemo Mussa Aliyekulia Kwa Faraoh kama Mtoto Wa Mfalme. Mussa alijua sayansi na ushirikina WOTE mana alikulia NDANI ya Ikulu ya Faraónh Lakini aliuacha akamwamini MUNGU Mmoja na Kupinga Imani za kishirikina . Waisraeli wengi walijua mbinu za wamisri za kishirikina lakini walikua wanaamrishwa waepukane nazo na wakawa wanatungiwa Sheria Kali sana kuachana nazo.
Musa alichelewa kurudi Toka mlimani Siku 40 tu Waisraeli wakaanza ibada za Sanamu Kwa kuchonga Sanamu ya Ng'ombe na kuiabudu.

MANABII WENGI WANATAMANI MIUJIZA LAKINI HAWATAIPEWA KAMWE NA MUNGU ANAACHA MAKUSUDI ILI KUWAJUA WATU WAKE HALISI. SASA WENGI WANAPOONA MUNGU ANACHELEWA KUJIBU MAOMBI YAO YA MIUJIZA WANAAMUA KUCHONGA SANAMU ZA NG'OMBE YAANI VITAMBAA ,MAFUTA ,KEKI, CHUMBI N.K. HIZI NI IBADA ZA WAMISRI. NA MPAKA LEO KULE MISRI KUNAVYUO VYA KICHAWI LAKINI KWA SABABU WANAFUNDISHA KWA KIARABU BASI WATU WANAJUA KUWA NI VYA KIDINI HIVYO KUNA WATU WENGI WANASOMEA KULE NA WANAJUA FOMRULA NYINGI ZA DAWA ZA KUONA ,KUFUGA NA KUTOA MAJINI. NDIZO WANAZOWAPA MANABII NA MAKRISTO WA UONGO WALIOCHOKA KUOMBEA KWA JINA LA YESU BILA MAFUTA NA KUONA KUWA WANATUMIA NGUVU KUBWA SANA KUOMBA NA HAKUNA MUUJUZA WALA NINI.
MAFUTA ni Ibada ya Sanamu.

YESU alimpaka MTU matope machoni kama Dawa lakini na kumwambia Kuwa Imani yake imemponya. Ile ilikuwa ni Dawa tu kama Panadol . Hakusema Kuwa ni matope ya upako.
Someni Vitabu .
 
Wewe inaonekana una mihemko,. Na hujui maandiko....bwana Yesu wanasema alitumia hata tope kumuondolea mtu upofu..hata mafuta eti..sijui unaelewa
Ni lini alirudia hayo ya kupaka tope? Kwamba ikawa ni utaratibu wa "kupaka tope" watu Ili wapone! He did it once.

Kingine injili ya Yesu ilikua ya watu kwenda mbinguni sio ya watu kupata mafanikio ya kimwili. Alitubisha watu waache dhambi, alibatiza n.k ila huyo Mwamposa ni lini kabatiza? Ni lini amejaza watu Roho Mtakatifu? Ni lini kamuambia mtu akiponywa asifanye dhambi Tena kama alivyokua anasema Yesu?!

Then acheni kumfananisha Mwamposa na Yesu maana Kila mtu akikosoa huduma yake mnakimbilia "Hata Yesu"..... As if Yesu alikua anaombea watu wapate magari na utajiri!!
 
Hivi unadhani Mungu Ana formula...unajua taratibu za Mungu wewe labda kama ni msaidizi wake...kama Bwana Yesu aliwaambia wale majambazi waliongikwa msalabani pamoja nae hapohapo kwamba jioni Ile wataenda wote Mbinguni, unadhani aliwabatizaje, au aliwapakaje mafuta...wale walipata ticket ya moja kwa moja...kwa hiyo msidhani taratibu zenu za kibinadamu sikuzote ndizo zitawafikisha Mbinguni.. sisi tukeshe na kuomba sikuzote kwa maana hatujui siku Wala saa tutakayotwaliwa. Unaweza kuta hao unaita wapagani wakawah kuingia Mbinguni na wewe unaenda motoni
 
Kwani lazima kuoa??

#MaendeleoHayanaChama
Kuoa ni lazima maana yule ni rijali, je mihemko yake ya kihisia anapeleka wapi?

Kwa maslahi ya waumini wake ilitakiwa amsamehe mkewe wawe pamoja
 
Nadhan usikariri jomba..bwana Yesu alikuja kuwaokoa wanadam kwa Hali zote..alisema Mali na vitu vyote tulivyonavyo duniani ni vyake..au hakusema...Sasa utatenganishaje hivi vitu wewe..Mali zote zinapatikana kwa uweza wake na kila kitu kinachoendesha chumi na maisha yetu..Sasa wapi walikataza usiuombee kupata Mali kama magari na vinginevyo...Jenga hoja vizuri jomba...tunahitaji kupanua mawazo yetu sana...shetani anajaribu kutufungafunga ili tusiweze kupambanua mbivu na mbichi..tusiwe na uelewa kwa maana anajua kabisa hapo ndio Siri yake ya ushindi
 
Yesu alimpa shortcut jambazi siku Moja tu wapi kwingine alitoa shortcut? Tatizo mnapenda kulinganisha na Yesu what the hell? Yesu hakurudia chochote alichofanya eti apake matope Kila siku mara atumie mafuta Kila siku nope Kila muujiza alifanya kwa mafunuo aliyokuwa nayo sio "formula" Moja kama Mwamposa.

Then Yesu alibatiza na kutubisha watu, na pia kuhubiri kuhusu maisha baada ya kifo. Je ni kipi hapo Mwamposa amewahi hubiri zaidi ya watu kupata pesa na kuponywa uchawi!!
 
Yote hayo yamekuwa substituted na DAMU YA YESU.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…