Mwenye historia ya Nabii Mwamposa kabla ya kuanza huduma yake

Kisha baada ya hayo Paulo akaanzisha biashara ya leso na nguo za upako ili ziwaponye watakaonunua.
 
Maelezo Yako yanafikirisha na yanaweza kuwa kweli.Ila ningetamani nabii asimwage baraka kama njugu Bali awatafutie watu njia ya kuingia ufalme wa Mungu ambalo ndio tatizo kubwa kwa wengi
Amen & Amen
 
Twende taratibu Yesu alisema Ufalme wa mbinguni ndio uanze mengine yafuate. So ilipaswa Mwamposa
1. Ahubiri watu waokoke
2. Awaombee Sala ya Toba
3. Awaombee wajazwe Roho Mtakatifu
4..Awafundishe waishi maisha ya kitakatifu na wajiandae na maisha baada ya kifo.

According to Yesu ukifanya hayo yote automatically mengine yote yanakufuata. Hivi ukiwa na Roho Mtakatifu utarogwa?? so Mwamposa akifanya yote hayo alafu ndio akaombea wapate magari sitokua na shida naye.
 
Kimsingi nimekuelewa sasa nini unamaanisha nashukuru kwa ufafanuzi wako huo ndiyo ukweli halisi.
 
Kuna jamaa alipeleka simu yake ikaombewe baada ya hapo ilianza kuingiza milioni kumi kumi kila siku na namba inayotuma haifahamu .Jamaa kajenga kanunua usafiri, Akafanikiwa kuoa mzungu kabisa. Napicha akaonesha. Watu makofi na vigelegele
 
Unajua sio kujilinganisha naYesu jomba .ni kufuata matendo ya Yesu kwa sababu ndie watu wanamwambia kwamba ni bwana na mwokozi wao..kwanini wasimfuate....hata bwana Yesu alisema kwamba tutafanya miujiza mingi zaidi ya aliyofanya yeye..unadhani ni vitu gani...ndio maana nasema tuwe waangalifu sana....shetani anatumia wakati mwingine bila kujijua..hivi niulize je wale wote wanaoshuhudia kwamba Mungu kawatendea miujiza huwa wanatengenezwa au ni matendo ya ukweli...Yale madudu, mijusi, manyau na vitu vingine ambavyo wachawi wanavitumia je ni kweli au uwongo
 
Anapokosea
1. Hajaombea watu Sala ya Toba
2. Hajawahi batiza
3. Hajawahi ombea watu wajazwe Roho Mtakatifu.
4. Hajawahi fundisha watu kuishi utakatifu na kwenda mbinguni.
5. Anasema Yesu ni WA dhehebu zote yaani hata ukiwa mpagani wewe pokea mafuta kaendelee na maisha Yako.

Je Kuna kipawa cha kupotosha injili?
 
Kuna jamaa alipeleka simu yake ikaombewe baada ya hapo ilianza kuingiza milioni kumi kumi kila siku na namba inayotuma haifahamu .Jamaa kajenga kanunua usafiri, Akafanikiwa kuoa mzungu kabisa. Napicha akaonesha. Watu makofi na vigelegele
Hahaha hiyo ni miujiza yake aliyopokea labda..au huamini Mungu hakuna linalomshinda...lisilo wezekana kwa binadamu kwa Mungu linawezekana...nadhan tusitake kum limit Mungu juu ya uwezo wake kabisa ..hivi umeshaona mwanamke Hana kizazi kimengolewa na anapata mimba na kuzaa...huyo ndio Mungu sasa
 
Ni lini Mwamposa atabatiza watu kama Yesu?
Ni lini atawaombea mjazwe Roho Mtakatifu
Ni lini atawafundisha kuhusu safari ya kwenda mbinguni?
 
Ni lini Mwamposa atabatiza watu kama Yesu?
Ni lini atawaombea mjazwe Roho Mtakatifu
Ni lini atawafundisha kuhusu safari ya kwenda mbinguni?
Jomba mi nadhani yote anafanya.. anabatiza, anaungamisha, anawafundisha maneno ya kwenda Mbinguni...lakini nimesema soma maneno kutoka Luka 9:49-50
 
Manabii wa kileo wana makando kando mengi sana miujiza hawana wengine wawavua chupi waumini mbele ya madhabahu na kuzinusa hadharani utasema ana kipawa?
Je yule alifumwa na mumini wake akijaribu kumtafuna mke mwenye ujauzito nyumbni kwa mwanakondoo wake huku amewqsha mishumaa na vibuyub?
 
Mwambosa anajua kuhubiri sio mchezo. Anajua kuichambua biblia vizuri na mafundisho yake ni mazuri. Ila hapo kwenye shuhuda kuna tatizo mahali kuna baadhi sio za kweli wala haiitaji akili nyingi kujua hilo
 
Yes Yesu ni wa wote wenye dhambi na wasio na dhambi...lakini hakuna binadamu ambaye ni mtimilifu mbele ya Mungu..kweli au si kweli ..awe mpagani au nani wote wanaweza mpokea Yesu ..na pale anapokwenda kwenye ibada na kukiri kwa kinywa chake tayari amempokea...tusi complicate na taratibu zetu za kibinadamu...waacheni wote wanaoenda kwa Yesu wampokee ..Yesu alikuja kwa ajili ya kuwaokoa wale wenye dhambi na sio wale ambao wameshaokoka..sijui unaelewa..kama wewe umeokoka tayari ujue Yesu hayupo na wewe hapo...hahaha .
 
Mwambosa anajua kuhubiri sio mchezo. Anajua kuichambua biblia vizuri na mafundisho yake ni mazuri. Ila hapo kwenye shuhuda kuna tatizo mahali kuna baadhi sio za kweli wala haiitaji akili nyingi kujua hilo
Shuhuda kama ipi si utuambie tujifunze kitu
 
Mkuu, maandiko hayajawahi kupinga miujiza mikubwa mikubwa kutokea kwa watu, bali imeonya kuwa hata wasio wa Mungu wanatenda hayo. Maandiko yametuonya tuyapime yote na kama yametokana na Mungu. Ni kosa kubwa sana kujenga msingi wa imani yako kupitia miujiza, ziko sababu nzito tu za kimaandiko.

1. Miujiza ni lazima imbadili mtu imani yake. Hili ni kubwa zaidi, tunaona kwa hiki kizazi cha manabii Waislamu na wapagani wengine wakipokea miujiza na kurejea kwenye imani zao. Wengine wengi wamejenga imani zao kwa mwamposa na maji na mafuta anayotoa. Hii ni hila ya shetani kabisa.

2. Miujiza ya mbinguni imelenga kumpa Mungu utukufu kwa sababu Mungu wa mbinguni hashiriki utukufu wake na kiumbe. Licha ya kauli ya kisanii "nani mtenda miujiza? ", lakini ni ukweli usio shaka wafuasi wa Mwamposa humpa utukufu yeye.

3. Msikilize vema Mwamposa, ni mhubiri mzuri sana wa miujiza na mafanikio. HAHUBIRI INJILI YA UFALME WA MBINGUNI. Wafuasi wake WOTE ni genge la wasaka mafanikio na afya pekee, kwani huhubiri habari za uzima ujao na maisha baada ya kifo. Huyu ni mtu hatari mno kwa ufalme wa mbinguni kwani anawafungia watu mlango wa mbinguni kwakuwaahidi raha ya hapa duniani.

4. Baada ya kushuhudia miujiza wafuasi wake hutoka bila uwezo wala upeo wa kumhubiri Kristo badala yake wana nguvu na mamlaka ya kuhubiri uweza wa Mwamposa kuponya. Hii inasababishwa na kutofundishwa neno la uzima bali majigambo na majivuno ya mhubiri kuponya. Wafuasi wake bila kujua hujifanya mabalozi wakubwa wa Mwamposa kwa watu wengi huku wakimnadi ni jinsi gani anaweza kuponya na kukupatia mali nk. Hii ni hila ya shetani.

Yako mengi ambayo ningeweza kuyaandika hapa lakini naishia hapo nisikie unajibu vipi hoja hizi za kimaandiko.
 
Umepotoka wala kweli haimo ndani yako
 
Mwambosa anajua kuhubiri sio mchezo. Anajua kuichambua biblia vizuri na mafundisho yake ni mazuri. Ila hapo kwenye shuhuda kuna tatizo mahali kuna baadhi sio za kweli wala haiitaji akili nyingi kujua hilo
Sijawahi msikia akichambua Biblia hata mara moja. Huyu ni mhubiri wa miujiza pekee.
 
Anawatoto?Kama hana mke kwahiyo anazini tu?
 
Kuna mafuta wananunua misri,na uchawi sehemu mbalimbali...tumewaona tangu 90' akina kakobe nk,wanakula,wanachuma Mali,muda ukifika wanakaa pembeni,wanakuja wengine
Maombezi ya mafuta yameanza miaka ya 2010s huko Tisini ulimuona yupi anafanya kwa style hiyo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…