Mwenye jengo akamatwe, eneo liuzwe, mali zake zifilisiwe, halafu hela zote wapewe majeruhi na waliofiwa

Hio siku ni lini ambayo mahakama itatenda haki? Na hapo unataka kusemaje kwamba mahakama ikamkamate mwenye Jengo na kumfungulia kesi?
Mimi sijasema leo Kesho au keshokutwa lakini ipo siku haki itapatikana

Usichoelewa ni nini Mkuu au ni kukaza ubongo bila sababu.
 
Haya kamkamate basi mwenye Jengo haki ipatikane kesho Serikali yenyewe itakushangaa unachokifanya
 
Kariakoo wange-replan upya hilo eneo matathalani hilo lingebaki eneo la wauzaji wa nguo pekee, maeneo mengine yaanzishwe kuweka watu wa bulding materials, stationeries simu na vifaa vyake ili mwisho wa siku maeneo muhimu mfano ya assembly point na disaster rescue access point ziwepo.

serikali ianzishe maeneo mengine ambayo yata serve kama Kariakoo lkn kwa bidhaa ambazo pekee zitakuwa zinapatikana maeneo hayo, so hata population itapungua maana wahitaji watakuwa wanaenda eneo specific kwa ajili ya kufuata huduma/ bidhaa zinazopatikana mahali hapo, Shida ss Kariakoo inayotokea ni kwa sababu eneo limekuwa centralised kwa bidhaa zozote wenyewe wanasema karikaoo kila kitu kinapatikana...u
Hiyo Kariakoo tayari imejigawanya. Kuna maeneo/ mitaa ina stationeries, mitaa yenye pharmacy na medical equipment, mitaa ya vifaa vya ujenzi na mitaa yenye vifaa vya magari kule gerezani. Sema kwa kuwa njia wanazopita ni zile zile, hiyo misongamano itakuwepo TU.
 
Babu Serikali hata kumzungumzia haijathubutu ndio ujue yeye ni dude kubwa kiasi gani
Sikatai mkuu, ila nyuma ya pazia ni lazima ujue jamaa ana kadi ya kijani na pengine ni miongoni mwa wafadhili wakubwa wa chama chao ndomaana wanamkalia kimya. Kinyume na hapo jamaa ni sisimizi tu mbele ya serikali. Anaweza kupotezwa katika mazingira ambayo hata yeye mwenyewe hatoweza kujua amepoteaje poteaje.

Unakumbuka wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, mzee Lowasa alitauminisha kwamba yeye anaijua serikali kindaki ndaki, kwamba ni mtu aliekulia na kuishi kwenye mfumo wa serikali kwa miaka mingi, hivyo hakuna anaweza kumtisha wala kuthubutu kumuibia kura yake hata moja.

Kilichotokea baada ya uchaguzi kila mtu ikiwemo wewe mwenyewe unakijua. Mhe aliishia kuongelea chini chini tu yakaisha bila kuthubutu kufanya lolote. Hii inamaana kuwa serikali ndio inayoamua kukuacha kwa sababu ya faida yao wenyewe, ila wakiamua kukunyea unaweza kutamani bora ungekuwa raia wa Burundi au Congo.
 
Kwa hio hapo unataka kusemaje? labda utuweke sawa kiongozi unataka kusema nini labda maana kila kitu nimeshakwambia
 
Mbona Mabasi yanaua Kila siku sijawahi sikia mwenye basi akikamatwa na Mali zake kuuzwa kugawiwa waliopata ajali?
Kuna ajali ya kutokea kwa bahati mbaya na ajali ya kusababishwa na uzembe wa mtu kwa tamaa zake mwenyewe mkuu.
 
Kwamba Jamaa ni dude kubwa kiasi kwamba Serikali inamhanya kumsemasema kwamba amefanya vibaya?
Namaanisha kuwa jamaa ni sisimizi tu mbele ya serikali. Ila kadi ya chama na ufadhili wa chama ndio vinavyoweza kumfanya jamaa aendelee kusavaivu na kuonekana kuwa ni dude kubwa mbele ya wananchi wa kawaida.

Siku akijichanganya akajifanya kufadhili upinzani au kwenda kinyume na kile kinachompa jeuri basi anaweza kujikuta yeye ni sisimizi tu kama walivyo raia wengine wa kawaida.
 
Sawa mkuu ndio nimekwambia yeye ni dude kubwa ndio maana Serikali imekula ganzi nilitaka nibwatuke ila mdomo koma
 
Kama ni sheria na itekelezwe, kama ni emotions tu tujitafakari wote tumechangia nini kwenye muktadha huu wote!
 
Sawa mkuu ndio nimekwambia yeye ni dude kubwa ndio maana Serikali imekula ganzi nilitaka nibwatuke ila mdomo koma
Kwanini uogope mkuu na wakati hata ukiongea hakuna wa kumchukulia hatua!!

Wenye kuogopa kuongelewa ni wale ambao wanajua ukimtaja tu au kumuongelea saa hizi, basi usiku ashaenda kupigiwa hodi na wasiojulikana.

Lakini huyu kwa mujibu wako hata ukimsema hakuna wa kumgusa maana tayari anajulikana.
 
Mkuu usiniset nikiwa napiga makelele nitakua pekeyangu hautakuwepo
 
Back
Top Bottom