Mwenye neno lolote aniambie japo kupoza akili yangu

Lakini ukweli ni kwamba watoto wanaweza kuwa mali wakitunzwa
Wasipotunzwa wanakuja kuwa mizigo na hata chanzo cha kuongezeka uhalifu
Hapa utunzwaji watoto sio tija mana fursa ni chache. Haya mambo yameelezwa na wasomi. Suluhu hapa ni kuwa na population ambayo ni CONTROLED tu. Sera inashindwa kuendana na idadi ya watu Kwa sabb ya kuzaana sana. Leo hii utasikia muhimbili haitoshi na nafasi ndogo wakati mwaka juzi ilitosha kabisa
 
Wala usiwe na wasiwasi, hivi ndio maana halisi ya maisha yaani ku Struggle, kila mmoja unaemuona mbele yako ana yake anapitia kama wewe lakini kubwa kuwa na tumaini, wakati mzuri upo mbele, wakati huu uliopo uwe ni wa maandalizi ya wakati mzuri unaokuja.
Maisha bila ya changamoto hayajawa maisha.
 
Sasa si hadi uwe na taaluma kidogo? Au mtu yoyote anaweza kufanya huo kazi bila kupata darasa
 
Usijiangaishe Kwa masuala ambayo yapo nje ya uwezo wako,hebu jiulize pamoja na kuwaza sanaaa kuhusu Hali ya uchumi wa familia Yako,Je Kuna mabadiliko yoyote? Jibu ni hamna. Muhimu ishi Leo maisha ni mafupi sana unapoishi Kwa stress muhimu zaidi hautaweza kumsaidia yoyote kuinuka kiuchumi kama wewe hujasimama sawa sawa,yaani inakuhitaji wewe kwanza ukae sawa kiuchumi ndipo unanze kumsaidia ndugu,jamaa. Umaskini upo na hautaweza kuumaliza kamwe pambania ndoto zako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukimaliza chuo,nenda veta kozi fupi ya ufundi yakukuweka mtaani,ukishindwa jifunze hata kupaka kucha na kubandika

Kama una kichwa kizuri ndani ya wiki moja ushajua,ukiongozana na wale chinga,na mtaji wake ni chini ya laki moja
Huu ni ushauri mzuri, anaweza hata akapangilia vizuri ratiba zake akaanza kujifunza ufundi kabla haja maliza chuo, fundi hajawahi kulala na njaa.
 
Pambana maisha ndo hayo. Kuna wenzio wanategemewa wakati hawana hata pa kupata mkopo wala nini. Usikate tamaa huenda ndo njia ya kufanikiwa hiyo.
 
Ila swala la uzazi, kuzaa na kuzaliwa lipo nje ya mamlaka binadamu

Seriously?? 😂

Kama una tatizo la ugumba,kuzaa inaweza kuwa nje ya uwezo wa binadamu...lakini kama kizazi kipo,control za kuzaa zipo
 
Oooyaaaaa wee! Mkurugenzi una zingua! Sasa stress za nini hapo? Wew wa MUNGU, wadogo zako wa MUNGU, yeye ndo anadili na matatizo ya binadam wake! Sasa saivi una sonona toka mzaliwe mbona mnakua tu freshi? Na usipo angalia na kua makini kama uko chuo tu una sema una stress ,wadogo zako wanakupa sonona,wazazi wanataka uwashike mkono.usipo badili mtazamo hasi huo bas ukija mtaan ujue wadogo zako na wazazi wewe ndo utawapa shida maana utachanganyikiwa
 
Yaani unajipa stress kisa watoto waliozaliwa na mtu mwingine? Come on

Ukweli ni kuwa bado wewe ni kapuku sana kuwa first born haikufanyi ubebe majukumu yasiyokuhusu jitafute wewe mwenyewe ukijipata ndiyo hangaika na hao nduguzo but mbali na hapo ipambanie future yako acha kiherehere kwenye mambo yasiyokuhusu .

Ni ushauri tu maana unajipa stress vitu vya kijingakijinga lakini kwenye orientation uliambiwa hela ya accomodation na meals ni ya kuwatumia wazazi ??

Acha ujinga stress unajitafutia ww mwenyewe kwani kabla ya kupata mkopo hao watoto na wazazi wako waliishije? Tafakari mdogo wangu .

Lakini vipi nasikia eti kipa wa Simba mbarazil haruhusiwi kucheza bongo hivi ni kweli kaka mkubwa ?

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
 
Usijisumbue kwa neno lolote, bali Kwa kila neno Kwa kufunga na kusali.
Haja zako na zijulikane kwa Mungu aliye hai.


Aonavyo mtu nafsini mwake ndivyo alivyo.
Na unavyokiri ndivyo unavyopokea.
 


Akili huwa inafikia mwisho wakati mwingine maana ina ukomo, ni logic, ndivyo ulivyoumbwa, kwa uliyoyasema nakuelewa sana.

Ila akili zinapofikia mwisho kuna matuamini, kuna Neema, ambayo inatoka na ahadi za Mungu na hizo ndo kimbilia.

Maisha utakayoishi kutoka sasa mpaka umalize chuo yataamua uendelee na sonona au uso utakate na ufanikiwe.

Mimi kama Mkristo, nikiwa na hali kama yako, tumaini langu huwa katika ukiri wa neno la Mungu tu na hivyo huona matokeo.

Imani ni jambo la Muhimu sana kwa mwanadamu, maana uwezo wake una mwisho, ila ana roho na access ya kuunganishwa na ulimwengo usio na mipaka.
 
Pambana na Hali yako Mzee baba,hao nane waliobaki waache wapambane na Hali zao Kwani ni walemavu au watoto?
Mambo ikikaa saw ndio ugeuke nyuma
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…