Mwenye uwezo wa kufunga mipaka afunge chakula kinanunuliwa sana na majirani zetu na huu mwaka kutakuwa na njaa

ARGAN MARA

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2016
Posts
1,020
Reaction score
2,716
Habari za jumapili kwa mapenzi makubwa kwa taifa langu naomba taarifa hii imfikie mwenye uwezo wa kuzuia chakula kuuzwa Nnje ya nchi

Kutokana na majirani zetu ususani Kenya na Congo kwa kipindi hiki wanauitaji mkubwa wa chakula kupelekea kununua kwa wingi mazao yalipatikana katika msimu uliopita

Kutokuzuiya itapelekea chakula kotokututosheleza na sisi kwa kipindi cha mda mfupi tu na sisi tutakuwa na uitaji wa chakula kutokana na msimu huu mvua zimekuwa chache sehemu nyingi zenye jamii ya wakulima vyakula vimeungua mashambani kutokana na ukosefu wa mvua za kutosha

Mwisho kabisa nipende kuwasisitizia watanzania wenzangu kutunza chakula kwani njaa iko karibu kutufikia.
 
Unatakiwa kuishauru serikali kununua chakula cha kutosha kutoka kwa wakulima ili ije ikabiliane na njaa itakayo tokea na sio kushauri kuzuia wakulima kuuza mazao yao maana wakati wanalima hamkuwa changia gharama za kilimo.
 
Serikali ianze kununua chakula na kuhifadhi. Soon tutaanza kulia.

Lakini kwa upumbavu wa machawa, tutaambiwa serikali ina chakula cha kututosha mwaka mzima ghalani
 
Wakulima wasipige hela kisa nyie wa mjini. Fanya kazi ununue chakula mambo ya kuishi mjini kwa kumnyonya mkulima yamepitwa na wakati. Siku hata wasomi wanalima hivyo usitarajie unayowaza.
Moja ya kitu huwezi kuamini ni kuwa hao hao wakulima ndo ambao wanaliaa njaa sana msimu ukishamalizaka wote na mazao yote.

Alafu kwa bei hizo za kuuza hadi njee anae nufaika sio mkulima niDALALI.

Mtu anachukua gunia Kwa Elfu 30 anaenda kuliiuza elfu 95. Usafiri utakuta anatumia Elfu kumi tuu.. Hivyo anapata faida zaidi ya yule alosotea mazoa zaidi ya miezi mitatu.

Tumeweka urefu sana kati ya mlimaji na mnunuaji halisi hivyo hapo katikati wanufaika ni Madalali alafu mkulima anaumia.
 
Mkuu; Umesema na tumekusoma. Lakini katika sentensi ya mwisho ndipo umeongea vizuri zaidi -Ninainukuu hapa:
"Mwisho kabisa nipende kuwasisitizia watanzia wenzangu kutunza chakula kwani njaa iko karibu kutufikia".
Huko kwingine ulikokuwa unafumble eti kufunga mipaka; swali 1. Halafu mipaka ikifungwa hao jirani zetu ndo wanastahili kufa kwa njaa? 2. Wewe na familia yako mnahitaji tani ngapi za chakula kiasi kwamba bila kufunga mipaka hataweza kuzipata au kujitosheleza?
Kumbuka na uzingatie kwamba Wenye mazao/vyakula kwenye magodown ni kama wewe unavyoweka fedha yako CRDB au NMB. Je huna uhuru wa kutumia fedha yako kwa kutekeleza mipango yako uliyojiwekea?Unaonaje kama Serikali itafreez hiyo A/C yako kwa lengo la kukulazimisha ulipe kwanza ada na michango ya shule kwa wanao? Si utajisikia vibaya na kuona Serikali umingilia mno Mipango yako i.e. Serikali imekuwa ni Mbabe kwako.
Mimi naona ingekuwa ni sahihi zaidi Serikali ichukue jukumu la kuwahabarisha, kuwaonya na kuwahamasisha wale wenye vyakula/mazao yao ghalani wawe makini sana watumie kwa uangalifu mkubwa kile walichonacho ila kama kuna mwenye ziada aruhusiwe kuuza sokoni - kwanza hapa ndani lakini pia asizuiwe uhuru wake wa kuuza nje kwa kufunga mipaka. Unaonaje kesho ikawa ni upande wetu njaa ni kali lakini majirani wana chakula lakini Serikali imefunga mipaka -hatuwezi kwenda kuhemea huko.
 
Singida mahindi yanagombaniwa na wakenya, wanapanda bei kila uchwao mpaka wabongo wamekimbia kuwaachia soko..

Mheshimiwa Bashe sijui kama ana taarifa hizi
 
Kwa mantiki yako, kazi ya Serikali ingekuwa ni kumlinda Mkulima dhidi ya hao madalali (Mtu wa kati) na kudhibiti japokuwa kwa kiasi fulani matumizi ya chakula/mavuno yasiyo sahihi.
 
Kwa mantiki yako, kazi ya Serikali ingekuwa ni kumlinda Mkulima dhidi ya hao madalali (Mtu wa kati) na kudhibiti japokuwa kwa kiasi fulani matumizi ya chakula/mavuno yasiyo sahihi.
Yaaah Huwa serikali zetu bwana zina focus na maswala sa ingine hayana maana ila ya muhimu yanaachwa..
Ukweli ulimaji kwa watu wakawaida unawatesa wakulima sana..
Wanao lima na kunufaika ni watu wenye uwezo kwasababu kumfikia mteja au mnunuzi ni rahisi kwao hawana haja ya dalali.

Mtu analima hata gari au kirikuu ya kupeleka mazao sokoni hana.. Dalalali anakuja na kumshawishi na hela kwa mazao yote .. anaona ahuni kumbe anaumia sana.. anauza kila kitu msimu ukiisha ana njaa balaaa
 
Acha wakulima wajipigie pesa bhana....maswala ya njaa na blah blah zingine, tutajua cha kufanya hiyo njaa itakapofika
 
Labla itakuwa ndo mwisho wa dunia 😎
 
Singida mahindi yanagombaniwa na wakenya, wanapanda bei kila uchwao mpaka wabongo wamekimbia kuwaachia soko..

Mheshimiwa Bashe sijui kama ana taarifa hizi
Umeanza vizuri lakini tena umekuja kuhoyanga hapo mwishoni kwa kumwita Mh. Bashe. Je; Unataka Bashe aingilie kati i.e. akukingie kifua kwenye ushindani wa soko??? Adhibiti nguvu ya soko kwa kuwa wewe kiwango cha uwezo wako kimepitwa na nguvu ya soko-Umeshindwa kumudu hali ya mapambano ya soko? Hapana. Acha nguvu ya soko itende sawia i.e. Demand & Supply iamue bei (Price)itakuwaje. Mbona bei kwa mkulima ikishuka hamlalamiki? au ni ile kanuni yenu kwamba Mfanya Biashara anataka /anapenda anunue at the lowest possible price halafu akauze at the highest possible (maximum) price.
 
Hii ndo dhambi kubwa mno Serikali inafanya. Mkulima mdogo ndo anaibeba Serikali na Hatma ya nchi katika mustakabali mzima wa Upatikanaji wa chakula hapa nchini. Hao wakulima wakubwa ni wafanya biashara na wanataratibu za Kisheria zinazowalinda. Mkulima mdogo ameachwa ajipambanie mwenyewe. Hiyo sio sawa.
Kwani Serikali ingepoteza nini au inashindwaje kuwadhibiti madalali? Inauma sana kwa mfano huku Umasaini, mfugaji akipeleka ng'ombe wake mnadani, njiani just some few meters from the auction mart, atakutana na mtu wa kati almaarufu kama Galagaja. Huyo galagaja atatumia kila mbinu ya ushawishi hadi atanunua ng'ombe huyo tena kwa bei ndogo e.g. 500K(Laki tano) lakini baada ya nusu saa tu, galagaja atakuwa amemfikisha mnadani huyo ng'ombe na ataweza kumuuza kwa 800-900K (almost a million) na ametengeneza faida ya 60-80% kwa ng'ombe mmoja ndani ya saa moja tu. Je, akinunua ng'ombe wengi intakuwaje ,vipi na akiongezapo na mbuzi?
 
Mkuu asilimia kubwa JF hatujizungumzii sisi. Sisi tayari kuwepo humu tuna exposure ya mambo mengi. Humu kuna mada kama hizi tunazungumzia jamii kubwa ya watanzania ambao hawana access na mitandao ya kijamii kupata taarifa ikiwemo hii JF. So usipende kujibu on personal attack basis... Jibu kwa consideration ya jamik nzima..
 
Nimelima nayajua mateso ya kilimo, nimesimamia taasisi inayonunua chakula na kuona shida zake. Ushauri tu kila mtu ajiwekee chakula chake mwenyewe. Mwacheni mkulima afaidi, hujui mateso wanayopotia mpaka wanavuna. Kazana ujiwekee akiba wewe, usizuie baraka ya mwingine.
 
Serikali ianze kununua chakula na kuhifadhi. Soon tutaanza kulia.

Lakini kwa upumbavu wa machawa, tutaambiwa serikali ina chakula cha kututosha mwaka mzima ghalani
Ww ndo umesema jambo la maana na sio kufunga mipaka.
 
Sawa mkuu. Samahani kama umejisikia vibaya kwamba ninakujibu ww as a person. Nia na mtizamo wangu ni kwamba humu Jf pia wamo watunga Sera na kwa kusoma comments za wadau wanaweza walau kupata cha kuwasaidia wanapotoa mwelekeo(Sera) katika masuala kama haya. i.e. wajue kwamba wapo watu tofauti na wao lakini wanafahamu kinachoendelea na wasidhani wananchi ni wa kuburuzwa tuu. Narudia tena kuomba samahani mkuu.
 
Singida mahindi yanagombaniwa na wakenya, wanapanda bei kila uchwao mpaka wabongo wamekimbia kuwaachia soko..

Mheshimiwa Bashe sijui kama ana taarifa hizi
Mkuu kwani bashe apate taarifa hayo mahindi ni mali yake?
Hivi nyinyi kila siku si ndo mnawaambia vijana wajiajili kwenye kilimo kwa hiyo unataka wajiajili kwenye kilimo alafu gunia la mahindi liuzwe 30000?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…