Mwenye uwezo wa kufunga mipaka afunge chakula kinanunuliwa sana na majirani zetu na huu mwaka kutakuwa na njaa

Sawa mkuu. Samahani kama umejisikia vibaya kwamba ninakujibu ww as a person. Nia na mtizamo wangu ni kwamba humu Jf pia wamo watunga Sera na kwa kusoma comments za wadau wanaweza walau kupata cha kuwasaidia wanapotoa mwelekeo(Sera) katika masuala kama haya. i.e. wajue kwamba wapo watu tofauti na wao lakini wanafahamu kinachoendelea na wasidhani wananchi ni wa kuburuzwa tuu. Narudia tena kuomba samahani mkuu.
Upo sahihi mkuu kwa kua humu tunaenda kwa hoja. Ukiangalia kwenye ground jinsi mahindi as particular yanavyouzwa kwa tani na tani, tena export, utagundua wakulima wetu hawana elimu ya kutosha. Wanafurahia temporary comfort ya kua na hela bila kuwaza kesho kuna nini kitatokea. Tunahitajika kutoa elimu kubwa sana kwa jamii yetu. Sio tu kwa mahindi, hata mazao mengine. Trust me anayeuza mahindi leo in 6 months atapanga foleni ya mahindi ya msaada toka serikalini.

Tupo pamoja Chief!
 
Mkuu kwani bashe apate taarifa hayo mahindi ni mali yake?
Hivi nyinyi kila siku si ndo mnawaambia vijana wajiajili kwenye kilimo kwa hiyo unataka wajiajili kwenye kilimo alafu gunia la mahindi liuzwe 30000?
No. Ishu sio bei ya kuuza. Ishu wakulima wapate elimu ya kutosha, wanapouza wakumbuke na kusevu. Wakulima wetu wengi wanafurahia kumiliki pesa ambayo mwisho wa siku walio wengi huishia kwenye matumizi hovyo ru.
 
Moja ya kitu huwezi kuamini ni kuwa hao hao wakulima ndo ambao wanaliaa njaa sana msimu ukishamalizaka wote na mazao yote.

Alafu kwa bei hizo za kuuza hadi njee anae nufaika sio mkulima niDALALI.

Mtu anachukua gunia Kwa Elfu 30 anaenda kuliiuza elfu 95. Usafiri utakuta anatumia Elfu kumi tuu.. Hivyo anapata faida zaidi ya yule alosotea mazoa zaidi ya miezi mitatu.

Tumeweka urefu sana kati ya mlimaji na mnunuaji halisi hivyo hapo katikati wanufaika ni Madalali alafu mkulima anaumia.
Mkuu kama huo udalali ni rahisi si uhufanye ili na ww upige hela utajirike?

Sio kweli kuwa mkulima hanufaiki,mazao yakipanda bei sokoni automatically na mashambani kwa wakulima yanapanda.
Haiwezekani eti sokoni gunia la mahindi litakuwa linauzwa kwa 100,000 alafu ujidanganye eti utaenda kwa mkulima upate gunia kwa 30,000 au 40,000sahau kama ni hivyo wafanya biashara za mazao wote wangekuwa matajiri ,lakini ni sekita ambayo wafanya biashara wake wengi ni wanganga njaa.

Alafu kwenye biashara yeyote dalali hakwepeki maana ww hapo ulipo kila ulicho miliki umekipata kupitia wachuuzi na madalali haukwenda kukinunua mojakwamoja kiwandani.

Cheni ya biashara ni lazima iwepo ili watu wengi wapate ajira ukusema mkulima aende akauze mazao yake moja kwa moja kwa waliaji jua hapo katikati kuna maelfu kwa maelfu ya watu watakosa ajira hasa wafanya biashara wa mazao wenye mitaji midogo.
 
Mkuu kwani bashe apate taarifa hayo mahindi ni mali yake?
Hivi nyinyi kila siku si ndo mnawaambia vijana wajiajili kwenye kilimo kwa hiyo unataka wajiajili kwenye kilimo alafu gunia la mahindi liuzwe 30000?
Eti bei elekezi ya Serikali ni Tzs 540 kwa kg. Yan gunia la kgs 100 ni Tzs 54,000/= . Halafu Sasa anakuja Mkenya anakupa Tzs 85,000- 110,000/= kwa gunia la kg 100. Utakuwa mjinga kama hutoipokea hiyo 80,000 -110,000/= ukang'ang'ania bei elekezi. Ni bora usubiri kwa uvumilivu hadi bei igonge 150,000/= (na imeshawahi kutokea) ndipo uuze mahindi yako-japokuwa sio rahisi sana ukizingtia majukumu na mahitaji ya lazima nyumbani kwako.
 
No. Ishu sio bei ya kuuza. Ishu wakulima wapate elimu ya kutosha, wanapouza wakumbuke na kusevu. Wakulima wetu wengi wanafurahia kumiliki pesa ambayo mwisho wa siku walio wengi huishia kwenye matumizi hovyo ru.
:HYPERCLAPHD: :HYPERCLAPHD: Hii iko poa kabisa.
 
Mtoa mada apuuzwe sisi wakulima ndio neema yetu.
 
No. Ishu sio bei ya kuuza. Ishu wakulima wapate elimu ya kutosha, wanapouza wakumbuke na kusevu. Wakulima wetu wengi wanafurahia kumiliki pesa ambayo mwisho wa siku walio wengi huishia kwenye matumizi hovyo ru.
Hili ndo tatizo la waafirika kujiendekeza yaani mtu una akili ya kwenda kuoa mpaka ukazaa watoto watano ila huna akili ya kutunza chakula kwa ajili ya hao watoto mpaka uje ufundishwe na serikali?
Mbona kwenye kuoa na kuzaa hukufundishwa na serikali?kwanini mnapenda kuibebesha serikali mizigo isiyo wahusu?
Mwaka 2017 Magufuri alinifurahisha alivyo wachanaga wafugaji wa kule manyara,mtu ana miliki ngombe 400 ila watoto wake wanateseka kwa njaa huku akisubiri msaada kutoka serikalini badala auze ngombe anunue chakula.
 
Eti bei elekezi ya Serikali ni Tzs 540 kwa kg. Yan gunia la kgs 100 ni Tzs 54,000/= . Halafu Sasa anakuja Mkenya anakupa Tzs 85,000- 110,000/= kwa gunia la kg 100. Utakuwa mjinga kama hutoipokea hiyo 80,000 -110,000/= ukang'ang'ania bei elekezi. Ni bora usubiri kwa uvumilivu hadi bei igonge 150,000/= (na imeshawahi kutokea) ndipo uuze mahindi yako-japokuwa sio rahisi sana ukizingtia majukumu na mahitaji ya lazima nyumbani kwako.
Hilo ndo ambayo hatutaki serikali inaweka bei elekezi hayo mazao ni ya serikali au ni ya wakulima?
Mkulima amelima kwa nguvu zake kwa jasho lake muache auze atavyo taka.
Serikali haitakiwi kuingilia bei ya mazao bali bei za mazao zinatakiwa kuamuliwa na wakati uliopo na sio Serikali imetakaje.

Magufuri chini ya Utawala wake aliingilia biashara ya kilimo mwisho wa siku mazao yalikuwa yana ozea shambani kwa kukosa wanunuzi.
 
Wakulima wasipige hela kisa nyie wa mjini. Fanya kazi ununue chakula mambo ya kuishi mjini kwa kumnyonya mkulima yamepitwa na wakati. Siku hata wasomi wanalima hivyo usitarajie unayowaza.
Unavuna gunia chini ya 20 unajiita mkulima,unauza zote baada ya miezi michache unataka kununua chakula unashindwa
 
Upo sahihi mkuu kwa kua humu tunaenda kwa hoja. Ukiangalia kwenye ground jinsi mahindi as particular yanavyouzwa kwa tani na tani, tena export, utagundua wakulima wetu hawana elimu ya kutosha. Wanafurahia temporary comfort ya kua na hela bila kuwaza kesho kuna nini kitatokea. Tunahitajika kutoa elimu kubwa sana kwa jamii yetu. Sio tu kwa mahindi, hata mazao mengine. Trust me anayeuza mahindi leo in 6 months atapanga foleni ya mahindi ya msaada toka serikalini.

Tupo pamoja Chief!
Kuna kipengele ni kama umekipuuzia mkuu. Ujue wakulima wale wanaolima Ha 1-5 ie. ekari 2-10 ndo wengi. Lakini wale wanaolima Ekari 50-300 au hadi 600 ni wachache lakini hutumia mikopo ya Benki.
Hao wanaozalisha kwa kutumia mikopo, kama wakivuna hawana namna. Marejesho ni lazima-vinginevyo nyumba inapigwa bei. Halafu cjui (uelewa wako) kama ulisha wahi kufanya Cost -benefit Analysis ya maize production. Uzalishaji wa mahindi kibiashara ni HASARA kamili.( I stand to be corrected, na ikiwapendeza wasomaji wa komenti yangu nitaweka hapa Uchambuzi wa Uhalisia kuonesha kwa nini nimesema ni HASARA kamili).
Biashara ya mahindi humnufaisha mtu wa kati (middle man) na hao ndo unaowaona wakipakia, wakijaza masemitela na kusafirisha kuelekea Himo, Dar n.k. Wao kama wao sio wazalishaji - sio wakulima.
Umesema ukweli usiopingika kwamba Elimu kwa wakulima ni muhimu sana. Wasidanganywe kwa bei ndogo na pia wakumbuke Akiba. Jambo hili limewahi kufanyika kwa kutoa elimu ya Food Budgeting at household level lakini dah! Wakulima hawakuzingatia na ikawa ni "back to square One" Wakuma wakivuna ndo kipindi cha kuoa, kulipa mahari , "kucheza ngoma" na starehe nyinginezo kwa kutumia kile kilichopatikana shambani.
Na inakuwa hivyo kwa sababu fedha wanapelekewa hard cash huko-huko mashambani kusikokuwa na Bank au Financial Services za kueleweka.
 
Hilo ndo ambayo hatutaki serikali inaweka bei elekezi hayo mazao ni ya serikali au ni ya wakulima?
Mkulima amelima kwa nguvu zake kwa jasho lake muache auze atavyo taka.
Serikali haitakiwi kuingilia bei ya mazao bali bei za mazao zinatakiwa kuamuliwa na wakati uliopo na sio Serikali imetakaje.

Magufuri chini ya Utawala wake aliingilia biashara ya kilimo mwisho wa siku mazao yalikuwa yana ozea shambani kwa kukosa wanunuzi.
Exactly yes Nakubaliana na ww 100%. Labda sana sana kazi ya Serikali ibaki kuwa ni kutoa Ushauri na kama tujuavyo ushauri unaweza kukubaliwa au kukataliwa (kutupwa kule).
Yan inafaa Serikali itambue na ikubali ukweli kwamba mazao ni mali ya wakulima baas. Serikali isimtendee mkulima ubabe na izingatie kwamba mkulima anapitia changamoto nyingi na kazi yake ni kazi ya sulba i.e. jua lake, mvua yake, anapambana na wafugaji ref. migogoro ya kulishiwa mazao shambani, anatembea parefu kwa miguu n.k. halafu at the end of the day anapata hicho alichopata, then Serikali inaingila mchakato wa uuzaji. Hilo sio sawa. Serikali imwache mkulima anufaike na jasho lake.
 
Hili ndo tatizo la waafirika kujiendekeza yaani mtu una akili ya kwenda kuoa mpaka ukazaa watoto watano ila huna akili ya kutunza chakula kwa ajili ya hao watoto mpaka uje ufundishwe na serikali?
Mbona kwenye kuoa na kuzaa hukufundishwa na serikali?kwanini mnapenda kuibebesha serikali mizigo isiyo wahusu?
Mwaka 2017 Magufuri alinifurahisha alivyo wachanaga wafugaji wa kule manyara,mtu ana miliki ngombe 400 ila watoto wake wanateseka kwa njaa huku akisubiri msaada kutoka serikalini badala auze ngombe anunue chakula.
Nachangia swali hili: "kwanini mnapenda kuibebesha serikali mizigo isiyo wahusu?
Jibu: Serikali inawajibika kwa wananchi kwa sababu inachukua kodi za wananchi hao.
 
Unavuna gunia chini ya 20 unajiita mkulima,unauza zote baada ya miezi michache unataka kununua chakula unashindwa
Kwani mkuu mipaka ikifungwa hayo mahindi ndo hatauza?
 
Nachangia swali hili: "kwanini mnapenda kuibebesha serikali mizigo isiyo wahusu?
Jibu: Serikali inawajibika kwa wananchi kwa sababu inachukua kodi za wananchi hao.
Kama ndo hivyo basi serikali ilitakiwa iwe inatutunzia mpaka watoto.
 
Habari za jumapili kwa mapenzi makubwa kwa taifa langu naomba taarifa hii imfikie mwenye uwezo wa kuzuia chakula kuuzwa Nnje ya nchi

Kutokana na majirani zetu ususani Kenya na Congo kwa kipindi hiki wanauitaji mkubwa wa chakula kupelekea kununua kwa wingi mazao yalipatikana katika msimu uliopita

Kutokuzuiya itapelekea chakula kotokututosheleza na sisi kwa kipindi cha mda mfupi tu na sisi tutakuwa na uitaji wa chakula kutokana na msimu huu mvua zimekuwa chache sehemu nyingi zenye jamii ya wakulima vyakula vimeungua mashambani kutokana na ukosefu wa mvua za kutosha

Mwisho kabisa nipende kuwasisitizia watanzania wenzangu kutunza chakula kwani njaa iko karibu kutufikia.
aliye lima ale nini sasa, kama mmeona fursa nunueni chote njaa ikija mtuuzie,
 
Kama ndo hivyo basi serikali ilitakiwa iwe inatutunzia mpaka watoto.
Naam! Ndiyo. Mbona inafanya hivyo tayari?
1. Usipompeleka mtoto wako shule, Hospitali, usipompa chakula na mavazi, Serikali inakuwajibisha.
2. Ukimwadabisha/Ukimchapa mtoto wako kupitiliza, Serikali utaiona mbele yako chaap'
3. ...........
4. ..............
Kwa mantiki hiyo, ww mzazi unatoa huduma ya kuwatunza watoto uliowazaa ww mwenyewe lakini ni kwa niaba ya Serikali.
 
Exactly yes Nakubaliana na ww 100%. Labda sana sana kazi ya Serikali ibaki kuwa ni kutoa Ushauri na kama tujuavyo ushauri unaweza kukubaliwa au kukataliwa (kutupwa kule).
Yan inafaa Serikali itambue na ikubali ukweli kwamba mazao ni mali ya wakulima baas. Serikali isimtendee mkulima ubabe na izingatie kwamba mkulima anapitia changamoto nyingi na kazi yake ni kazi ya sulba i.e. jua lake, mvua yake, anapambana na wafugaji ref. migogoro ya kulishiwa mazao shambani, anatembea parefu kwa miguu n.k. halafu at the end of the day anapata hicho alichopata, then Serikali inaingila mchakato wa uuzaji. Hilo sio sawa. Serikali imwache mkulima anufaike na jasho lake.
Hilo ndo linalo takiwa, jukumu la kurahisisha maisha ya wana nchi ni la serikali na sio jasho la wakulima.
Serikali inunue chakula kutoka kwa wakulima kwa bei wanayo itaka ili njaa ikitokea serikali iweze kuhudumia raia wake.
Kipindi cha Magufuri mazao ya kilimo yaligeuka kama mavi kwa kukosa thamani kwa sababu ya upumbavu wa serikali kuingilia soko.
Mtu ana kuambia vijana waache uzembe waende wakalime alafu wakati huo anataka gunia la mahindi liuzwe 30,000 ili maisha yake yawe rahisi.
 
Moja ya kitu huwezi kuamini ni kuwa hao hao wakulima ndo ambao wanaliaa njaa sana msimu ukishamalizaka wote na mazao yote.

Alafu kwa bei hizo za kuuza hadi njee anae nufaika sio mkulima niDALALI.

Mtu anachukua gunia Kwa Elfu 30 anaenda kuliiuza elfu 95. Usafiri utakuta anatumia Elfu kumi tuu.. Hivyo anapata faida zaidi ya yule alosotea mazoa zaidi ya miezi mitatu.

Tumeweka urefu sana kati ya mlimaji na mnunuaji halisi hivyo hapo katikati wanufaika ni Madalali alafu mkulima anaumia.
Kuna wakulima wanalima heka mpaka 200. Usifikirie tu mkulima wa heka 3,5,10. Kwa hio ukifunga mipaka unaua nguvu ya mkulima kutoboa. Wakulima ndio wanaoumia sio wanaiasa au wafanyabiashara. Kuna mwaka magu alifunga mipaka aisee viazi viliozea shambani, wakenya hawakuja kununua,wapemba nao hawakuja. Debe la viazi liliuzwa sh elf 7000 dsm kule shamba hata bure watu walikuwa hawavitaki. Magu aliua mtaji wangu niliouhangaikia . Yaani watu wa mjini wanataka mazao yawe chini ili waishi na kustarehe mijini kwa jasho la mkulima.
 
Back
Top Bottom