Unaposema ametumia muda wake mwingi kuwakaripia viongozi wenzake wa Chadema, nakushangaa, kama wewe ukiona mtu anakusema kwa kitu ambacho hujafanya, mtu anaendeshwa na hisia zake binafsi kukuhumu, na kukuchafua kwa wanachama wako, utakaa kimya?
Kwangu, alichofanya Mbowe ni sahihi kabisa, Lema na wenzake walitakiwa waje na uthibitisho wa vile Mbowe alilambishwa asali, lakini sio mtu upo Canada, kisa unaona mambo hayaendi vile ulivyozoea, ndio uanze kutengeneza hisia zako na kutoa shutuma kwa kiongozi wako, alikosea.
Mimi na wewe hatuwezi kujua secret behind ya kuruhusiwa hii mikutano ya siasa, lakini inawezekana kabisa, hekima na ukimya wa Mbowe, ndivyo vilichangia kumfanya Samia akubaliane nae, lakini kama mihemko ya kina Lema mnayoipenda ndio ingekuwa kwenye meza ya mazungumzo, basi inawezekana kabisa, mpaka leo mambo yangekuwa hayaeleweki...
Mbowe amejua kucheza na akili ya Samia na kushinda mchezo, tuliona vile ukimuendea Samia kwa mihemko nini atakufanya, - ukinipara nakuparua -, mwishowe Mbowe akaenda jela kwa kesi ya kutengenezewa, na hakuna mwanachama wala mpenzi yeyote wa Chadema, aliyefanya chochote ili kumtoa Mbowe gerezani, wakati mwingine acheni akili zifanye kazi, sio maguvu kila wakati!.