Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ninakusikiliza mkuu.Amepoteza hii nafasi. Ametumia muda mrefu kuwakaripia viongozi wenzake wa Chadema kuliko kuikosoa CCM. Ametumia mrefu mno kulalamikia dhana kuwa amelamba asali kuliko kuwazungumzia wanachama wenzake ambao bado wako ndani. Mimi nilitegemea angetumia nafasi hii kuunganisha na kuwatia moyo wanachama wenzake lakini badala yake ametuonyesha kuwa kuna mpasuko ndani ya chama chake na hataki kukoselewa. Ameni disappoint sana. Angalau viongozi wenzake waliomtangulia walionyesha kuwa bado moto unawaka ndani ya matumbo yao.
Amandla...
Duh!Mwamba ana hangover ya maridhiano au anajaribu kucheza ndani ya mistari aliyochorewa na wenye nchi kumbuka ile kasi ya mchongo bado file lipo.
Kalamu
Ninakusikiliza mkuu.
Sijamsikia Mbowe kwa leo, lakini nilimsikia wakati ule wa 'Diaspora', na hapo hapo nikahitimisha juu ya hatma ya Mbowe.
Kama hakuibua lolote jipya zaidi ya yale ya "Diaspora", CHADEMA itabidi waanze safari yao kivingine bila Mwenyekiti wao huyu.
Mbowe leo aliwanywea pombe chadema- k vant oyeee
Ukweli ni kwamba Mbowe alikwishanyang'anywa ajenda siku nyingi na Samia.Niwe mkweli, CHADEMA ikifuata trend ya Mbowe hatufiki mbali.
Yaani mwamba Hajasema Neno lolote linalogusa maisha ya Wananchi zaidi yakusifia watawala. Leo hii mbowe anawaambia Wananchi walipongeze jeshi la police[emoji848][emoji848]
Nahisi Mwenyekiti Mbowe amelewa, hii sio sauti yake ya kawaida. Ametumia mkutano huu kujisafisha kuhusu kulamba asali.
Japo Rais Samia Suluhu anafanya vziuri lakini ametumia muda mrefu sana kumsifia.
Is MBOWE OKAY?
View attachment 2490283View attachment 2490284View attachment 2490285View attachment 2490286
Naunga mkono hoja hii......Cdm waanze kumuandaa mrithi wa Mbowe sasa hivi mapema kwa faida yao na nchi kwa ujumla.Niwe mkweli, CHADEMA ikifuata trend ya Mbowe hatufiki mbali.
Kiwanga kazungumzia maumivu ya wakina mama. Pambalu kazungumzia maumivu ya vijana na kukumbusha kuwa bado kuna watu wao wengi wako ndani. Kuna waliozungumzia deni, kuna waliozungumzia waliotangulia mbele ya haki, kuna waliozungumzia maumivu waliyopata katika miaka hii ya zuio la mikutano. Mwenyekiti alitakiwa kujenga kwenye msingi walioweka waliomtangulia.
Amandla...
..Yote hayo yatasemwa.
..kabla ya Mbowe kuzungumza, Msigwa alipewa nafasi na akazungumzia ugumu wa maisha.
..Heche naye alipopewa nafasi alizungumzia hali mbaya ya uchumi inayowakabili wananchi.
..Cdm wakipanda jukwaani wanapiga hoja, hawana muda wa kumsujudia mwenyekiti.
Hawa walevi na hiyo saccos yao ya kikabila ndio wanataka tuwape nchi yetu nzuri?
Kuna kiongozi gani leo wa CDM ametukana? Kiongozi gani kamkashifu Mh. Rais Samia? Sugu amemsifia sana Mheshimiwa Rais. Mbona wote hawasemwi? Mimi namlaumu zaidi Mbowe kwa kuwasema vibaya viongozi wenzake jukwaani. Angemsifia Mheshimiwa Rais pamoja na kuzungumzia kwa kina challenges zinazokabili chama chake na wananchi kwa ujumla wala nisingepiga kelele. Aidha, ningemdharau sana kama angemtukana na kumkashifu Mheshimiwa Rais.Mbowe safi kabisa, ila ujue tu CHADEMA wenzako unaowaongoza watakuchukia, sababu walitaka utukane, utoe maneno makali ya kumkashifu Mh. Rais Samia etc, hongera Mh. Mbowe
Nahisi Mwenyekiti kuhutubia akiwa CHAKALI ina maanisha kuvaa miwani ya mbao kufisha tuhuma za yeye kulamba asali.
Ila tulisoma CUBA tunajua na yeye mwenyewe anajua hana jinsi maana ile kesi ya ugaidi umewekwa PENDING akienda tofauti wana review imekuwa fimbo ya kumchapia na kuwanyamazisha.
Sawa maridhiano ni mazuri lakini awaoni gharama za maisha kusababishwa na mfumuko wa bei,na ufisadi etc
Mbowe safi kabisa, ila ujue tu CHADEMA wenzako unaowaongoza watakuchukia, sababu walitaka utukane, utoe maneno makali ya kumkashifu Mh. Rais Samia etc, hongera Mh. Mbowe
Huo ndio ukubwa. Hata Lissu walimshutumu mengi alipokutana na Rais Ubelgiji na kueleza wazi kuwa ameahidiwa kulipwa madai yake. Mbowe ni Mwenyekiti na alipaswa kumalizana na viongozi wenzake kwenye vikao vyao vya ndani. Hapa palikuwa mahali pa kuthibitisha umoja wa chama chake na utayari wake wa kumpambania mtanzania. Si mahali pa kujibishana na vijana wa kwenye mitandao (ambao inawezekana wengine ni wa upande wa pili na nia yao ilikuwa ni kuleta ufa). Njia pekee ya kuthibitisha kuwa yeye hakulamba asali ni kuonyesha kwa vitendo kuwa ari yake ya kupigania haki iko pale pale. Watu wanaingia wasiwasi wanapomuona amekuwa kimya sana na anapoibuka ni kummwagia sifa Mwenyekiti wa chama pinzani. Wenzake wanazungumzia ugumu wa maisha yeye anasifia kukua kwa uchumi! Kwa kweli amekua tone deaf.
Amandla...