Mwenyekiti Mbowe, kweli Rais Samia amefanya mazuri ila sifa kwake zimezidi!

Mwenyekiti Mbowe, kweli Rais Samia amefanya mazuri ila sifa kwake zimezidi!

Amepoteza hii nafasi. Ametumia muda mrefu kuwakaripia viongozi wenzake wa Chadema kuliko kuikosoa CCM. Ametumia mrefu mno kulalamikia dhana kuwa amelamba asali kuliko kuwazungumzia wanachama wenzake ambao bado wako ndani. Mimi nilitegemea angetumia nafasi hii kuunganisha na kuwatia moyo wanachama wenzake lakini badala yake ametuonyesha kuwa kuna mpasuko ndani ya chama chake na hataki kukoselewa. Ameni disappoint sana. Angalau viongozi wenzake waliomtangulia walionyesha kuwa bado moto unawaka ndani ya matumbo yao.

Amandla...
Ninakusikiliza mkuu.
Sijamsikia Mbowe kwa leo, lakini nilimsikia wakati ule wa 'Diaspora', na hapo hapo nikahitimisha juu ya hatma ya Mbowe.

Kama hakuibua lolote jipya zaidi ya yale ya "Diaspora", CHADEMA itabidi waanze safari yao kivingine bila Mwenyekiti wao huyu.
 
Mwamba ana hangover ya maridhiano au anajaribu kucheza ndani ya mistari aliyochorewa na wenye nchi kumbuka ile kasi ya mchongo bado file lipo.
Kalamu
Duh!
Sijamsikia Mwenyekiti leo.

Ngoja kwanza niyapate aliyoyazungumzia leo, kama yana tofauti kubwa na yale aliyozungumzia wakati ule akiwa safarini kule Marekani.
 
Ninakusikiliza mkuu.
Sijamsikia Mbowe kwa leo, lakini nilimsikia wakati ule wa 'Diaspora', na hapo hapo nikahitimisha juu ya hatma ya Mbowe.

Kama hakuibua lolote jipya zaidi ya yale ya "Diaspora", CHADEMA itabidi waanze safari yao kivingine bila Mwenyekiti wao huyu.

Niwe mkweli, CHADEMA ikifuata trend ya Mbowe hatufiki mbali.
 
Niwe mkweli, CHADEMA ikifuata trend ya Mbowe hatufiki mbali.
Ukweli ni kwamba Mbowe alikwishanyang'anywa ajenda siku nyingi na Samia.

Mbowe hana ajenda yoyote iliyotofauti na ile anayoitekeleza Samia ndani ya CCM.

Sasa ataanzia wapi kupingana na Samia. Tatizo linaanzia hapo.

Samia atakapomaliza kazi ya kuwazima mabaki ya Magufuli, sina shaka yoyote akimkaribisha Mbowe kwenye boti lake kwenda mbele.
 
Yaani mwamba Hajasema Neno lolote linalogusa maisha ya Wananchi zaidi yakusifia watawala. Leo hii mbowe anawaambia Wananchi walipongeze jeshi la police[emoji848][emoji848]

Kwa polisi hata Mimi nawapongeza, wamesimamia msafara wa CHADEMA vizuri kuanzia Nyashishi mpaka mjini. Nadahani Mbowe ana nia nzuri ila mazingira yetu kwa Sasa hayaruhusu Hilo.
 
Nahisi Mwenyekiti Mbowe amelewa, hii sio sauti yake ya kawaida. Ametumia mkutano huu kujisafisha kuhusu kulamba asali.

Japo Rais Samia Suluhu anafanya vziuri lakini ametumia muda mrefu sana kumsifia.

Is MBOWE OKAY?
View attachment 2490283View attachment 2490284View attachment 2490285View attachment 2490286

Kuna mengi Raisi Samia anafanya vizuri. Kuhusu bei ni tatizo la kidunia sio Tanzania pekee. Kuanzia China, US , EU tatizo la bei ni kila mahali. Mimi nipo Texas na bei ni tatizo mpaka huku.
 
Kiwanga kazungumzia maumivu ya wakina mama. Pambalu kazungumzia maumivu ya vijana na kukumbusha kuwa bado kuna watu wao wengi wako ndani. Kuna waliozungumzia deni, kuna waliozungumzia waliotangulia mbele ya haki, kuna waliozungumzia maumivu waliyopata katika miaka hii ya zuio la mikutano. Mwenyekiti alitakiwa kujenga kwenye msingi walioweka waliomtangulia.

Amandla...

Kweli kabisa. Alitakiwa kitoa mwelekeo tunaendaje kutoka hapa. Angekuja hata na slogan. Nimependa Mama Kiwanga alivyosema miaka hii miwili kabla ya uchaguzi tutatebea nchi nzima kuwaelezea wananchi matatizo yao. At least Mwenyekiti angeto slogan hata MKATABA na WATANZANIA kihusu reforms mbalimbli. Lakini Mwenyekiti kaongea vitu vya ndani ya chama.
 
Nionavyo mimi.
Kazi ya Mwenyekiti Mbowe, iliyokuwa imebakia ili kusimika uongozi wake imara katika historia ya nchi hii, baada ya misukosuko yote ile aliyopitia, na kusimama kidete hadi CHADEMA kufikia hapa ilipo sasa, ilikuwa ni KATIBA MPYA.

Hii ndiyo kazi pekee iliyosalia, na ajenda kuu aliyopaswa kuisimamia bila kutetereka.
Angetimiza kazi hii kwa ufanisi mkubwa, hakuna mtu ambaye angetokea tena kuhoji uongozi wa Mbowe katika historia ya nchi yetu.

Sasa sijui tena kama bado hili analikumbuka.
 
..Yote hayo yatasemwa.

..kabla ya Mbowe kuzungumza, Msigwa alipewa nafasi na akazungumzia ugumu wa maisha.

..Heche naye alipopewa nafasi alizungumzia hali mbaya ya uchumi inayowakabili wananchi.

..Cdm wakipanda jukwaani wanapiga hoja, hawana muda wa kumsujudia mwenyekiti.

Mimi niliyemwelewa Ni Susan Kiwanga na Catherine Ruge. Wao wamesema miaka hii miwili watatembeaa nchi nzima kuelezea shida za wanachi. Nadhani CHADEMA tujikite happy na kuelezea tutafanya Nini kuhusu Hilo au reformations , tuachane na mambo ya kusutana kuhusu kulamba asali.
 
Mbowe safi kabisa, ila ujue tu CHADEMA wenzako unaowaongoza watakuchukia, sababu walitaka utukane, utoe maneno makali ya kumkashifu Mh. Rais Samia etc, hongera Mh. Mbowe
Kuna kiongozi gani leo wa CDM ametukana? Kiongozi gani kamkashifu Mh. Rais Samia? Sugu amemsifia sana Mheshimiwa Rais. Mbona wote hawasemwi? Mimi namlaumu zaidi Mbowe kwa kuwasema vibaya viongozi wenzake jukwaani. Angemsifia Mheshimiwa Rais pamoja na kuzungumzia kwa kina challenges zinazokabili chama chake na wananchi kwa ujumla wala nisingepiga kelele. Aidha, ningemdharau sana kama angemtukana na kumkashifu Mheshimiwa Rais.

Amandla...
 
Nahisi Mwenyekiti kuhutubia akiwa CHAKALI ina maanisha kuvaa miwani ya mbao kufisha tuhuma za yeye kulamba asali.

Ila tulisoma CUBA tunajua na yeye mwenyewe anajua hana jinsi maana ile kesi ya ugaidi umewekwa PENDING akienda tofauti wana review imekuwa fimbo ya kumchapia na kuwanyamazisha.

Sawa maridhiano ni mazuri lakini awaoni gharama za maisha kusababishwa na mfumuko wa bei,na ufisadi etc

Umaelewa maana ya pending case?. Ni kesi ambayo bado haijatolewa maamuzi. Sasa kesi ya Mbowe imefutwa, ikirudishwa inaanza upya kabisa.
 
Mbowe safi kabisa, ila ujue tu CHADEMA wenzako unaowaongoza watakuchukia, sababu walitaka utukane, utoe maneno makali ya kumkashifu Mh. Rais Samia etc, hongera Mh. Mbowe

Sio kutoa maneno makali au matusi. Acha kupotosha.
 
Huo ndio ukubwa. Hata Lissu walimshutumu mengi alipokutana na Rais Ubelgiji na kueleza wazi kuwa ameahidiwa kulipwa madai yake. Mbowe ni Mwenyekiti na alipaswa kumalizana na viongozi wenzake kwenye vikao vyao vya ndani. Hapa palikuwa mahali pa kuthibitisha umoja wa chama chake na utayari wake wa kumpambania mtanzania. Si mahali pa kujibishana na vijana wa kwenye mitandao (ambao inawezekana wengine ni wa upande wa pili na nia yao ilikuwa ni kuleta ufa). Njia pekee ya kuthibitisha kuwa yeye hakulamba asali ni kuonyesha kwa vitendo kuwa ari yake ya kupigania haki iko pale pale. Watu wanaingia wasiwasi wanapomuona amekuwa kimya sana na anapoibuka ni kummwagia sifa Mwenyekiti wa chama pinzani. Wenzake wanazungumzia ugumu wa maisha yeye anasifia kukua kwa uchumi! Kwa kweli amekua tone deaf.

Amandla...

Ni muda wa Mbowe kustaafu, la sivyo anachojaribu kufanya matokeo yake sio mazuri. Viongozi wote walioongea wamekuwa tofauti naye.
 
Nadhani hujasijiliza hotuba za Viongozi wote. Wameongelea issue zote za wananchi. Sema mwenyekiti ndio kaharibu.
 
Back
Top Bottom