Mwenyekiti Mbowe, kweli Rais Samia amefanya mazuri ila sifa kwake zimezidi!

Mwenyekiti Mbowe, kweli Rais Samia amefanya mazuri ila sifa kwake zimezidi!

Mbowe analazimisha chama kiende mrengo wake. Lissu na Heche ndio wanafaa kushika gurudumu. Kulikuwa na mengi ya kusema , mfumuko wa Bei, Deni la taifa.
Yaani mwamba Hajasema Neno lolote linalogusa maisha ya Wananchi zaidi yakusifia watawala. Leo hii mbowe anawaambia Wananchi walipongeze jeshi la police[emoji848][emoji848]
 
Mbowe analazimisha chama kiende mrengo wake. Lissu na Heche ndio wanafaa kushika gurudumu. Kulikuwa na mengi ya kusema , mfumuko wa Bei, Deni la taifa.
Kiwanga kazungumzia maumivu ya wakina mama. Pambalu kazungumzia maumivu ya vijana na kukumbusha kuwa bado kuna watu wao wengi wako ndani. Kuna waliozungumzia deni, kuna waliozungumzia waliotangulia mbele ya haki, kuna waliozungumzia maumivu waliyopata katika miaka hii ya zuio la mikutano. Mwenyekiti alitakiwa kujenga kwenye msingi walioweka waliomtangulia.

Amandla...
 
Mbowe analazimisha chama kiende mrengo wake. Lissu na Heche ndio wanafaa kushika gurudumu. Kulikuwa na mengi ya kusema , mfumuko wa Bei, Deni la taifa.

..Yote hayo yatasemwa.

..kabla ya Mbowe kuzungumza, Msigwa alipewa nafasi na akazungumzia ugumu wa maisha.

..Heche naye alipopewa nafasi alizungumzia hali mbaya ya uchumi inayowakabili wananchi.

..Cdm wakipanda jukwaani wanapiga hoja, hawana muda wa kumsujudia mwenyekiti.
 
Hapa hapakuwa mahali pake. Huu ni mkutano wa kwanza na angeweza kuutumia kusherehekea matunda ya juhudi zake bila kuwakaripia wanachama na viongozi wenzake ambao hawakukubaliana nae. Hii kuonyesha kukasirishwa sana na maneno ya baadhi ya wanachama imewaonyesha wapi udhaifu wake upo.

Mimi sijawahi kumsikia kiongozi mkuu yeyote wa CDM akimshutumu kuwa amelamba. Hata hivyo ni haki yao kuhoji gharama ya maridhiano hayo. Huyo Lema unaemsema nae amepitia magumu sana katika haya mapambano. Ingawa sio wote waliopoteza mabilioni kama alivyoteza Mbowe wako ambao kwa kiasi fulani wamepoteza kuliko yeye. Watu kama Heche aliyempoteza mdogo wake, watu kama Lissu aliyenusurika kupoteza maisha yake na vijana na wanachama wengi ambao wameumizwa, wamepoteza vibiashara vyao na wengine wametiwa ndani bila kuwa na uhakika wa kutoka mapema kwa sababu hawana majina kama Mbowe.

Unamsema Lema na wenzake na kumpa sifa Mbowe peke yake bila kujiuliza kama CCM wangekubali kuridhia kama pasingekuwa na sauti za wazi za wakina Lema kuwa hawana imani nao kabisa. Mbowe aliongezewa nguvu na uwepo wa wakina Lema kwa sababu CCM walijua dhati kuwa muafaka ungekuwa mgumu kupatikana kama Mbowe angesusa na wangebaki wakina Lema a Antipas. Ni kama vile Martin Luther King Jr. alisaidiwa sana na uwepo wa Malcolm X ambae hakutaka kabisa mazungumzo na mtu mweupe.

Mbowe anataka kuonekana kama Statesman lakini bila street fighters kama Lema, Lissu hata Mdude Chadema ari ya kuzungumza nae ingepungua.

Leo ilikuwa ni siku ya Chadema lakini yeye ameigeuza kwa kiasi fulani kuwa ya CCM. Hamna mtu anaemkataza kumshukuru Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa CCM. Ni jambo la busara kwa kweli. Lakini hapakuwa na haja ya kuwatupa wenzake chini ya basi.

Amandla...
- Unaposema hapakuwa mahali pake, sijui unataka pawe wapi pengine?, hii ni sawa na kumfunga mdomo Mbowe ashambuliwe tu na kukaa kimya, kwangu sio sawa.

- Lema kupitia magumu, hakumpi ruhusa ya kutoa shutuma kwa kiongozi wake zisizo na uthibitisho, alikosea, mbona hao kina Heche walikuwa kimya?

- Mbowe kutaka kuonekana statesman ni mtazamo wako hasi tu, muda wote aliokaa kimya mpaka anashutumiwa na Lema bila kujibu chochote ni uthibitisho tosha.

- Hilo la mwisho nalo la siku ya leo kuwa ya CCM ni mtazamo wako mwingine hasi tu, kwasababu umeamua kubeba kujitetea kwa Mbowe dhidi ya shutuma za Lema kama ndio ajenda yako kuu, mnapenda kumshambulia Mbowe ila yeye asijitetee!.
 
Angeenda bila kulewa asingekuwa huru kuyataja mazuri ya Mama Samia. Kafanya vyema sana. Inahitaji kujitoa ufahamu kwanza mbele ya BAVICHA ili uweze kuzungumzia mazuri ya CCM. Mbowe ni mtaalamu wa siasa za nchi hii.
Nahisi Mwenyekiti kuhutubia akiwa CHAKALI ina maanisha kuvaa miwani ya mbao kufisha tuhuma za yeye kulamba asali.

Ila tulisoma CUBA tunajua na yeye mwenyewe anajua hana jinsi maana ile kesi ya ugaidi umewekwa PENDING akienda tofauti wana review imekuwa fimbo ya kumchapia na kuwanyamazisha.

Sawa maridhiano ni mazuri lakini awaoni gharama za maisha kusababishwa na mfumuko wa bei,na ufisadi etc
 
Unaposema hapakuwa mahali pake, sijui unataka pawe wapi pengine?, hii ni sawa na kumfunga mdomo Mbowe ashambuliwe tu na kukaa kimya, hii sio sawa.
Huo ndio ukubwa. Hata Lissu walimshutumu mengi alipokutana na Rais Ubelgiji na kueleza wazi kuwa ameahidiwa kulipwa madai yake. Mbowe ni Mwenyekiti na alipaswa kumalizana na viongozi wenzake kwenye vikao vyao vya ndani. Hapa palikuwa mahali pa kuthibitisha umoja wa chama chake na utayari wake wa kumpambania mtanzania. Si mahali pa kujibishana na vijana wa kwenye mitandao (ambao inawezekana wengine ni wa upande wa pili na nia yao ilikuwa ni kuleta ufa). Njia pekee ya kuthibitisha kuwa yeye hakulamba asali ni kuonyesha kwa vitendo kuwa ari yake ya kupigania haki iko pale pale. Watu wanaingia wasiwasi wanapomuona amekuwa kimya sana na anapoibuka ni kummwagia sifa Mwenyekiti wa chama pinzani. Wenzake wanazungumzia ugumu wa maisha yeye anasifia kukua kwa uchumi! Kwa kweli amekua tone deaf.

Amandla...
 
Mbowe safi kabisa, ila ujue tu CHADEMA wenzako unaowaongoza watakuchukia, sababu walitaka utukane, utoe maneno makali ya kumkashifu Mh. Rais Samia etc, hongera Mh. Mbowe
 
Kupata nafasi ya kujitetea na kuacha kufanya hivyo hakuwezi kuwa ukubwa, ni mtazamo wako mwingine hasi tu, usiingilie maamuzi ya Mbowe, huo ni udikteta, hata kama akiwa kiongozi, coz hakuna anayeingilia yako.

Lissu kufanya yalikuwa maamuzi yake, lakini hiyo haikuwa sheria, kila mtu aifuate!.
 
Mbowe safi kabisa, ila ujue tu CHADEMA wenzako unaowaongoza watakuchukia, sababu walitaka utukane, utoe maneno makali ya kumkashifu Mh. Rais Samia etc, hongera Mh. Mbowe
Kufutiwa kesi sio mchezo
 
Kupata nafasi ya kujitetea na kuacha kufanya hivyo hakuwezi kuwa ukubwa, ni mtazamo wako mwingine hasi t, usiingilie maamuzi ya Mbowe, hata kaa akiwa kiongozi, coz hakuna anayeingilia yako.
Hakuanza leo kujitetea. Hata Washington ilikuwa hivyo hivyo. Another lost opportunity.
Lakini hatugombani. Ni mtazamo wangu. Sio lazima ukubaliane nao.

Amandla...
 
Hakuanza leo kujitetea. Hata Washington ilikuwa hivyo hivyo. Another lost opportunity.
Lakini hatugombani. Ni mtazamo wangu. Sio lazima ukubaliane nao.

Amandla...
Tunaelekezana I know, usiogope!.

Mtazamo hauwezi kujenga chuki.
 
Ile kesi ya kupika ilitumika vizuri sana kummaliza na unayoyaona huenda ni masharti ya maridhiano kwamba kuna mipaka imewekwa ni marufuku kuvuka.......poor Mbowe....Poor Tz democracy...[emoji17][emoji17][emoji17].

denooJ zitto junior
"Huenda"

Ajabu ndio unamhukumu Mbowe kupitia neno hilo.
 
Yaani mwamba Hajasema Neno lolote linalogusa maisha ya Wananchi zaidi yakusifia watawala. Leo hii mbowe anawaambia Wananchi walipongeze jeshi la police[emoji848][emoji848]
Mwamba ana hangover ya maridhiano au anajaribu kucheza ndani ya mistari aliyochorewa na wenye nchi kumbuka ile kesi ya mchongo bado file lipo.
Kalamu
 
Back
Top Bottom