Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la CHADEMA aliyekamatwa Zanzibar, Hashimu Issa Juma apelekwa Kisutu

Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la CHADEMA aliyekamatwa Zanzibar, Hashimu Issa Juma apelekwa Kisutu

Bado wapinzani hawajaelewa namna ya kudili na nyakati.

Kosa kubwa la chadema ni kubeba mambo yote kwa pamoja na kurukia kila hoja.

Kigogo aliwashauri vizuri kuwa waandae watu . Mpaka anakamatwa na kupelekwa kusikojulikana wao hawana information toka ndani ya mifumo ya dola ni udhaifu mkubwa.

Chadema mpaka Mwenyekiti wao alikamatwa kibubusa bila taarifa ni ukolo.

Kigogo alijaribu kuwapa somo zuri sana la kujipanga lakini wakapotosha kuwa anawashauri kuandaa uasi. Mpaka sasa bado viongozi wanatekwa.

Sent from my TECNO L8 Lite using JamiiForums mobile app
Naona ukiwarushia lawama wapinzani na hasa Cdm kuhusu utendaji mbaya wa vyombo vyetu. Je inaisaidia nini nchi hii , ikiwa miaka 60 baada ya Uhuru Tanganyika bado ni masikini wa kusaidiwa sindano na nyembe ?!.

Kitengo hicho faida yake ni nini ?!
 
Hata Lissu akiwa rais watu watatekwa kama kawa, KUNA SYSTEM nyuma ya rais,Ndio maana tunaoijua hii nchi, tunajua Mbowe sio Gaidi ila SYSTEM imefanyabyake, angekuwepo JPM angetupiwa kila lawama...

SAMIA awali hakuijua Vzr SYSTEM..... akataka aendeshe nchi yeye kama yeye, ndipo SYSTEM ikamuambia kina mbowe watamzid kete...

Now Mbowe yupo korokoroni.....
Kweli sisi ni maamuma hatujui kinachoendelea inamaana System can do whatever they like bila kukubaliana na Rais? Basi haya ni makubwa.
 
Ameyataka mwenyewe mzee mzima ndio anashobokea siasa

USSR
Wewe uliathiriwa na vitendo vya uzalilishaji toka kwa "wajomba" zako,ndio maana upo hivyo ulivyo,robo taahira,robo msukule,robo maiti,robo mchawi.
 
hao huwa wapo miaka yote sema mitandao imesaidia kuwajua miaka ya karibuni hao ndio hujiona ndio serikali juzi walimyakua mchora katuni
wenggi hawajui hao watu wapo toka enz za nyerere, had kwa samia wanapiga kaz

ukiwa rais lazima uwaheshimu,wapo kwa manufaa mapana ya taifa,

JPM alikuwa anatoa hotuba akilalamika jinsi lissu anavyoshirikiana na wazungu kuhujumu nchi...

baada ya muda lissu alikiona cha mtema kuni....hawa jamaa huwa sio lazima wapate go ahead ya RAIS

Kwenye system lissu kamwe hawez kuwa rais...anajulikana kama MUHAINI
 
View attachment 1961683

Hii ndio Taarifa mpya kutoka Chadema kwa sasa, ambapo watu wasiofahamika wakiwa na bunduki wamemchukua Mzee Hashimu Issa nyumbani kwake Unguja na kuondoka naye, tena bila kusema wanampeleka wapi.

Taarifa zaidi zitaendelea kuwajia kwa kadri zitakavyotufikia.
Kuna Jambo watu wanalazimosha pasipo sababu , twende tu
 
HUIJUI HISTORIA YA HII NCHI

wana hoja,system iliwahi kumuondoa makamu wa raisi...

Alipotea makamu wa RAIS Abdallah Hanga huko Zanzibar Hadi leo hajapatikana

Muulize lissu,Roma mbona adui yao JPM hayupo, lkn wanaogopa kurudi...wanaogopa nn....hadi roma katelekeza familia...au JPM yupo
Hakuna cha system, nchi zaidi ya 35 za kiafrika kati ya 54 zimewahi kupinduliwa na jeshi sasa kwenye hizo nchi hamna hiyo system unayoiongelea.

Huyo Abdallah Hanga aliuwawa kwa amri ya Karume na hilo linafahamika vema. Hakuna kitu kinachoitwa system la sivyo mabadiliko ya utawala yasingekuwa yakifanyika.

Huu utawala wa ccm ni swala la muda tu hauatukuwepo, pale shinikizo ya kuwataka wafanye sweeping political reforms itakapoongezeka kwa siku zijazo kwani serikali haiwezi ku-survive bila kupata uungwaji mkono kutoka kwa mataifa tajiri.
 
ukisikia baridi kali - ujue kunakaribia kuchwa !!
 
Vijana hawaijui hii nchi... juzi tu alipoingia samia.... wametekwa wengi tu wenye kelele

kwa kikwete ULIMBOKA alitekwa hata JK hakujua.....amekuja kumuona muhimbili....

Roma alitekwa kwa makosa ya kipind cha JK, mwanzon mwa utawala wa JPM....
Acha uongo wewe. Roma alitekwa na bashite baada ya kutoa wimbo wenye maudhui ya kumponda JPM.
 
Hakuna system inaweza kufanya jambo bila mkuu wao kujua au kupewa taarifa ya operation hiyo na kuiridhia. Hiyo system inaongozwa na watu ambao kwa ukubwa wake ni wateule wa Rais.
Na kama utaicha system ifanye kazi bila kukutaarifu wewe ipo siku watakugambanisha na wananchi uwajibike wewe wakati wao wakila maisha kwa dhulma zao.
Rejea viongozi wengi wa hizi unazoita system walivyowajibishwa baada ya kufanya bila matakwa ya mkubwa wao.
Kwakifupi kila kitu kinachoendelea Samia anakibariki na kama analazimishwa basi ujue hatuna Rais na hii ni hatari kubwa sana.
Umenena vyema mkuu
 
Wanakamatwa sio kutekwa polisi hawateki wanakamata SEMA walikamatwa we anawahi kusema kutekwa ,ukifanya mgumu lazima ukalishwe


USSR
Hahaha PGOOOOOO,😂 wabongo washaisoma baada ya kutoifahamu kwa miaka dahar, sasa walishaichambua kuliko hata hao policcm 😀. Mlifanya makosa makubwa Sana kuiacha nje kibatala akapita nayo! sasa Mambo yote hadharani,wabongo wanajua Ni wakati gani wanakamatwa,wanabakwa au wanatekwa Ni kosa la PGO usilaumu mtu.
 
Wewe uliathiriwa na vitendo vya uzalilishaji toka kwa "wajomba" zako,ndio maana upo hivyo ulivyo,robo taahira,robo msukule,robo maiti,robo mchawi.
Ni mirengo tu wewee kushangiliae kifo cha jpm na mm kufurahia mwenyekiti wako kufungwa tofauti ninini?




USSR
 
View attachment 1961683

Hii ndio Taarifa mpya kutoka Chadema kwa sasa, ambapo watu wasiofahamika wakiwa na bunduki wamemchukua Mzee Hashimu Issa nyumbani kwake Unguja na kuondoka naye, tena bila kusema wanampeleka wapi.

Taarifa zaidi zitaendelea kuwajia kwa kadri zitakavyotufikia.
Haya ndio Mambo yaliyomkuta Moses Lijenje
 
Back
Top Bottom