Katika hali isiyokuwa ya kawaida, mwenyekiti wa CCM huko Kilimanjaro (Chugga) amemrubuni mke wa mtu na kumuoa (bibi harusi). Kufuatia kadhia hiyo, wananchi wa eneo hilo wamecharuka vibaya sana wakimtaka mwenyekiti huyo awajibike kwa ukware wake wa kuchukua wake za watu mara kwa mara huku akijua kwamba kufanya hivyo ni kosa kisheria.
Imewalazimu wananchi hao kuandamana wakidai kuwa kama amemuona huyo mke wa mtu ni mwali, basi atoe mahari kwa mwenye mke, isiwe shida. Aidha, wananchi hao wamemtaka mwenyekiti wao kujiudhuru nafasi hiyo kwani amekuwa na tamaa na ulafi wa wake za watu kwa kiwango cha kutisha. Hawataki tena aendelee kuwa mwenyekiti wao abadani.
Wakuu sitaki kuwapotezea muda. Hebu wasikilize nyinyi wenyewe hapo chini wananchi wenye hasira kali wanavyosema:
MAONI YANGU
CCM siku zote wamekuwa wakipora rasilimali za taifa bila huruma na sasa wamehamia kwenye uporaji wa wake za watu.
Hivi hawa walafi ni lini wataacha kufakamia rasilimali za taifa pamoja na kupora wake za watu? Inauma na inahudhunisha sana!