2015 Magufuli hakuwa na nguvu kisiasa kakini alipitishwa na chama kugombea mbele ya vigogo na "huyu mwenzetu". Kwa sasa Magufuli siyo tu amejijengea jina kubwa nchini hata kimataifa kwa umahiri na umakini wake katika maamuzi, utawala, uongozi na uwajibika kwenye utendaji.
Itakuwa busara na ITAPENDEZA iwapo vyama vingine vya siasa, kama TLP, watamuunga mkono Magufuli kama mgombea wao. Wakifanya hivyo wananchi watawaelewa na angalau kuwapa kura kwa baadhi ya madiwani na wabunge.
MAENDELEO HAYANA CHAMA
-Ameshindwa kukuza uchumi na kugusa maisha ya watu moja kwa moja
- ameshindwa kutoa ajira ipasavyo hadi za zile kada za huduma za jamii mfano Elimu na afya yaani kwenye utawala wake watu wenye degree za udaktari,ufamasia,unesi,ualimu hawajaajiriwa vya kutosha ukilinganisha na 2015 kurudi nyuma
-jingine ni tatizo la ajira kwa ujumla wake limekuwa kubwa sana siyo degree wala wasio nazo,
-kingine ni hali ngumu kwa watumishi wa umma kutoongenezewa mshahara (nyongeza ya mwaka) hiyo imesababisha hali ngumu sana kwa watumishi wa umma na hivyo hilo limepelekea kushuka kwa purchasing power yao kwa sababu kipato kutokana na inflation.
-kingine watumishi hao hao wanalalamika kutokuwa na upandaji wa madaraja kwa wakati.
-kingine hali nzima ya utawala wa sheria imeshuka tumeona yeye mwenyewe akivunja katiba kwa kutoa msamaha kwa watuhumiwa rejea wale polisi wa madini,andengenye, kukiuka Sheria ya vyama vya siasa na katiba kwa kuweka masharti ya umri ya kuzuia siasa hadi 2020 na ile kusema ufanyie siasa ulipochaguliwa hilo ni kinyume kabisa na sheria, amevunja katiba kwa kuteua makada wa ccm kuwa majaji
-kutungwa kwa sheria zinazoashiria kutokuwa na utawala wa sheria mfano kufanyia marekebisho sheria ya judiciary administration act na kuwapa kinga makarani,wahasibu,na wafanyakazi wengine,
-kinga ya mashtaka kwa Jaji mkuu,waziri mkuu,spika,makamu wa rais.
-kuvurugwa kwa mfumo wa utetezi wa haki za binadamu kwa kuweka masharti kwenye sheria yanayotaka uonyeshe madhara uliyopata wewe binafsi na hivyo hilo linaathiri kesi za maslahi ya umma na kuathiri haki ya ulinzi wa katiba kama ilivyoelezwa kwenye katiba.
-Uhuru wa mahakama nyie wenyewe ni mashahidi mliona kaimu jaji mkuu, kwa nafasi ya jaji mkuu kumuweka mtu akaimu ni kutingisha na kuyumbisha muhimili wa mahakama dhidi ya matendo yasiyofaa ya executive
-Hali ya mahusiano ya kimataifa imetingishwa rejeeni matamko ya EU,USA embassy,dhidi ya mambo yanayofanyika nchini na rejea kuwekewa vikwazo kwa ofisa wa serikali kutoingia USA
-