Uchaguzi 2020 Mwenyekiti wa CCM, Dkt. John Magufuli achukua fomu ya kugombea Urais wa Tanzania kwa muhula wa pili

Mtu mmoja tu anachukua fomu. Anaenda kushindana na nani. Demokrasia ya kiprimitive hiyo.
 
2015 Magufuli hakuwa na nguvu kisiasa kakini alipitishwa na chama kugombea mbele ya vigogo na "huyu mwenzetu". Kwa sasa Magufuli siyo tu amejijengea jina kubwa nchini hata kimataifa kwa umahiri na umakini wake katika maamuzi, utawala, uongozi na uwajibika kwenye utendaji.

Itakuwa busara na ITAPENDEZA iwapo vyama vingine vya siasa, kama TLP, watamuunga mkono Magufuli kama mgombea wao. Wakifanya hivyo wananchi watawaelewa na angalau kuwapa kura kwa baadhi ya madiwani na wabunge.

MAENDELEO HAYANA CHAMA
-Ameshindwa kukuza uchumi na kugusa maisha ya watu moja kwa moja
- ameshindwa kutoa ajira ipasavyo hadi za zile kada za huduma za jamii mfano Elimu na afya yaani kwenye utawala wake watu wenye degree za udaktari,ufamasia,unesi,ualimu hawajaajiriwa vya kutosha ukilinganisha na 2015 kurudi nyuma
-jingine ni tatizo la ajira kwa ujumla wake limekuwa kubwa sana siyo degree wala wasio nazo,
-kingine ni hali ngumu kwa watumishi wa umma kutoongenezewa mshahara (nyongeza ya mwaka) hiyo imesababisha hali ngumu sana kwa watumishi wa umma na hivyo hilo limepelekea kushuka kwa purchasing power yao kwa sababu kipato kutokana na inflation.
-kingine watumishi hao hao wanalalamika kutokuwa na upandaji wa madaraja kwa wakati.
-kingine hali nzima ya utawala wa sheria imeshuka tumeona yeye mwenyewe akivunja katiba kwa kutoa msamaha kwa watuhumiwa rejea wale polisi wa madini,andengenye, kukiuka Sheria ya vyama vya siasa na katiba kwa kuweka masharti ya umri ya kuzuia siasa hadi 2020 na ile kusema ufanyie siasa ulipochaguliwa hilo ni kinyume kabisa na sheria, amevunja katiba kwa kuteua makada wa ccm kuwa majaji
-kutungwa kwa sheria zinazoashiria kutokuwa na utawala wa sheria mfano kufanyia marekebisho sheria ya judiciary administration act na kuwapa kinga makarani,wahasibu,na wafanyakazi wengine,
-kinga ya mashtaka kwa Jaji mkuu,waziri mkuu,spika,makamu wa rais.
-kuvurugwa kwa mfumo wa utetezi wa haki za binadamu kwa kuweka masharti kwenye sheria yanayotaka uonyeshe madhara uliyopata wewe binafsi na hivyo hilo linaathiri kesi za maslahi ya umma na kuathiri haki ya ulinzi wa katiba kama ilivyoelezwa kwenye katiba.
-Uhuru wa mahakama nyie wenyewe ni mashahidi mliona kaimu jaji mkuu, kwa nafasi ya jaji mkuu kumuweka mtu akaimu ni kutingisha na kuyumbisha muhimili wa mahakama dhidi ya matendo yasiyofaa ya executive
-Hali ya mahusiano ya kimataifa imetingishwa rejeeni matamko ya EU,USA embassy,dhidi ya mambo yanayofanyika nchini na rejea kuwekewa vikwazo kwa ofisa wa serikali kutoingia USA
-
 
Ndo kishachukua form, hakuna kuwaachia upenyo Mabeberu na vibaraka wao. Rais bora wa Afrika, nchi zote zinamtamani
 
Ni rahisi zaidi ngamia kupenya tundu ya sindano, kuliko mwanasiasa kuingia katika ufamle wa Mungu!
 
Muda ni miaka 5. Usipotaka kuendelea unaruhusiwa, na pia unaruhusiwa kugombea vipindi viwili tu.
Kama alikuwa analalamika amebebeshwa mzigo, angeweza kukaa pembeni walafi wengine wakaingia kwenye ulaji.

Sent from my LM-Q710(FGN) using JamiiForums mobile app
Naunga mkono hoja!!
 
-Ameshindwa kukuza uchumi na kugusa maisha ya watu moja kwa moja
- ameshindwa kutoa ajira ipasavyo hadi za zile kada za huduma za jamii mfano Elimu na afya yaani kwenye utawala wake watu wenye degree za udaktari,ufamasia,unesi,ualimu hawajaajiriwa vya kutosha ukilinganisha na 2015 kurudi nyuma
-jingine ni tatizo la ajira kwa ujumla wake limekuwa kubwa sana siyo degree wala wasio nazo,
-kingine ni hali ngumu kwa watumishi wa umma kutoongenezewa mshahara (nyongeza ya mwaka) hiyo imesababisha hali ngumu sana kwa watumishi wa umma na hivyo hilo limepelekea kushuka kwa purchasing power yao kwa sababu kipato kutokana na inflation.
-kingine watumishi hao hao wanalalamika kutokuwa na upandaji wa madaraja kwa wakati.
-kingine hali nzima ya utawala wa sheria imeshuka tumeona yeye mwenyewe akivunja katiba kwa kutoa msamaha kwa watuhumiwa rejea wale polisi wa madini,andengenye, kukiuka Sheria ya vyama vya siasa na katiba kwa kuweka masharti ya umri ya kuzuia siasa hadi 2020 na ile kusema ufanyie siasa ulipochaguliwa hilo ni kinyume kabisa na sheria, amevunja katiba kwa kuteua makada wa ccm kuwa majaji
-kutungwa kwa sheria zinazoashiria kutokuwa na utawala wa sheria mfano kufanyia marekebisho sheria ya judiciary administration act na kuwapa kinga makarani,wahasibu,na wafanyakazi wengine,
-kinga ya mashtaka kwa Jaji mkuu,waziri mkuu,spika,makamu wa rais.
-kuvurugwa kwa mfumo wa utetezi wa haki za binadamu kwa kuweka masharti kwenye sheria yanayotaka uonyeshe madhara uliyopata wewe binafsi na hivyo hilo linaathiri kesi za maslahi ya umma na kuathiri haki ya ulinzi wa katiba kama ilivyoelezwa kwenye katiba.
-Uhuru wa mahakama nyie wenyewe ni mashahidi mliona kaimu jaji mkuu, kwa nafasi ya jaji mkuu kumuweka mtu akaimu ni kutingisha na kuyumbisha muhimili wa mahakama dhidi ya matendo yasiyofaa ya executive
-Hali ya mahusiano ya kimataifa imetingishwa rejeeni matamko ya EU,USA embassy,dhidi ya mambo yanayofanyika nchini na rejea kuwekewa vikwazo kwa ofisa wa serikali kutoingia USA
-
Hongera kwa kuorodhesha mapungufu katika utawala wake. Kule kuyatambua, na ukayaorodhesha, ni dhahiri kuwa unajua ni kwa kiwango gani amefanikiwa katika maeneo hayo. Kwa ufupi unakubali aliyoyaanisha katika hotuba yake ya kuvunja bunge, iliyosheheni takwimu (zinajibu maswali yako yote), tofauti na mtia nia ya Urais kama huyu.
 
Hongera kwa kuorodhesha mapungufu katika utawala wake. Kule kuyatambua, na ukayaorodhesha, ni dhahiri kuwa unajua ni kwa kiwango gani amefanikiwa katika maeneo hayo. Kwa ufupi unakubali aliyoyaanisha katika hotuba yake ya kuvunja bunge, iliyosheheni takwimu (zinajibu maswali yako yote), tofauti na mtia nia ya Urais kama huyu.View attachment 1481821
Wapi nimesema nayakubali aliyoyasema?
 
Mkuu Kalisheshe, pole kwa kutonielewa na hauko peke yako, ili unielewe ni lazima unisome huku umetulia, umetuliza akili na pia uwe wako wa uelewa uwe ni wa level fulani ya kiwango cha uelewa!, hivyo ukijikuta hunielewi kabisa, naomba unisamehe tuu, hiyo ndio level yako.
P
Mheshimiwa, ni kazi pia kwa watu wazima kuwaelewa watoto wachanga wanachomaanisha wanapojaribu kutoa sauti zao za kitoto.
 
Tupo pamoja Mh. Rais na Mwenyekiti wa CCM, unapoanza safari yako ya kuingia katika awamu ya pili ya uongozi wako kwa Taifa.

Tutakuwa hapa kuonesha support yetu kwako.

Kila la heri Mkuu.
 
Back
Top Bottom