Uchaguzi 2020 Mwenyekiti wa CCM, Dkt. John Magufuli achukua fomu ya kugombea Urais wa Tanzania kwa muhula wa pili

Uchaguzi 2020 Mwenyekiti wa CCM, Dkt. John Magufuli achukua fomu ya kugombea Urais wa Tanzania kwa muhula wa pili

Ngoja na mimi nikachukue fomu!wasiojulikana wakini ua basi!!NAOMBENI MNICHANGIE JAMANI NISHINDANE NA MAGUFULI NDANI YA CHAMA!!
 
Hili linaitwa igizo la kukamilisha matakwa ya kikatiba.

Natamani kuona akijitokeza mtu mwingine achukue fomu ya kuombea nafasi ya urais

Lakini naambiwa mwenye ccm yao wanautamaduni wao, ukianza moja sharti uachiwe utimize mpaka kumi.

Ifike wakati wabadilishe huu utamaduni tufate katiba inavyotaka tuachane na utamaduni

Ukiwepo ushindani baada ya miaka mitano unatoa nafasi ya kiongozi kufanya kazi ufanisi zaidi
 
Hivi hakuna wanaopiga makofi akinywa maji?
Make MATAGA mnasifia hata visivyosifiwa.
 
Hili ni ONYO sasa ajitokeze mwanachama yeyote anaewashwa washwa na urais
 
Yes nimemuona live kupitia TBC rais Magufuli akichukua fomu ya kugombea urais kupitia CCM.

Kule tuu kuonyeshea live kupitia TBC ni kitu kizuri kwa kuonyeshea transparency ya zoezi hili zima, na kwa vile TBC ni public broadcasting station yaani TV ya umma, imetimiza wajibu wake kikamilifu kututangazia live, na natoa wito kwa vyama vyote vya siasa vitakavyo simamisha wagombea urais, kutoa ushirikiano kwa TBC ili TBC iwatangazie live Watanzania wagombea wao na kuwapa fursa Watanzania kuwaona wagombea wote wakipewa haki sawa kwenye vyombo vya habari vya umma.

Pili nimemnote rais Magufuli akitumia usafiri wa gari lenye number binafsi. This is very good thing kwasababu rais Magufuli ametenganisha shughuli za chama na shughuli za serikali. Rais Magufuli hakutumia gari za serikali, wala hakutembea na msafara ikiwemo battalion, rais Magufuli ametumia gari moja tuu yenye number za kiraia,
Hatua hii ni hatua yenye essence kubwa sana kwenye mustakabali wa usawa wa kidemokrasia na usawa wa uwanja wa mapambano kujenga uwanja sawa, the level playing field, hivyo ni hatua muhimu kuifuta ile dhana ya kugombea urais Tanzania kufananishwa na kugombea kisu cha makali kuwili huku mgombea mmoja ameshika mpini na kuwashikisha wapinzani wake upande wa makali kuwili
P
Kuna muda huwa sikuelewi kabisa Kaka Pascal Mayalla.
 
Kuna muda huwa sikuelewi kabisa Kaka Pascal Mayalla.
Mkuu Kalisheshe, pole kwa kutonielewa na hauko peke yako, ili unielewe ni lazima unisome huku umetulia, umetuliza akili na pia uwezo wako wa uelewa uwe ni wa level ya kiwango fulani cha uelewa kunielewa, hivyo ukijikuta hunielewi kabisa, naomba unisamehe tuu, hiyo ndio level yako.
P
 
Kuchukua fomu ni hiari sio lazima ukiona hakuna mwingine kachukua jua ni hiari .CCM tuko kidemokrasia mtu ana hiari ya kuchukua au kutochukua fomu.Hivyo ukiona hakuna aliyechukua zaidi Ya raisi Magufuli ujue wazi kuwa watu wametumia hiari yao kutochukua fomu sio kesi
Kama vile wabunge wa chadema wanavyompa mshahara wao Mbowe na wabunge wa CCM hawampi mshahara wao Magufuli. Ni utaratibu wa kila chama.
 
Hakuna hata mgombea mwingine wa kufanya maigizo ya kuchukua fomu huko ili aoneshe Mwenyekiti wenu sio dikteta, ameruhusu ushindani ndani ya chama chake?
Nyie chadema ongeleeni mgombea wenu wa CCM anawahusu Nini? Au wenu Hana ubavu wa kupambana na JPM? Ni wakati wenu kuchukua nchi chagueni wa kumbwaga JPM asubuhi mapemaa!
 
Back
Top Bottom