Pre GE2025 Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe akamatwa uwanja wa Ndege Songwe

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Uko sawa kabisa Kenya wanajijua na wanaendelea, huku kwetu maiti
 
Hawataacha kuwakamata kama,kuwateka ,kuwaua, kuwafunga na kuwapiga kama wanaofanya huo uovu wanapandishwa vyeo.

Mbowe alikosa maono akakimbilia Maridhiano ili tu afanye siasa za majukwaani bila kuona wazi hatari iliyokuwa mbele yake.

Yaani Mbowe aliona wazi kuwa Wambura a'eteuliwa kuwa GP, Kingai ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai,Awazi ameteuliwa kuwa Kalishina wa Oparation nchi nzima akiwa anatokea Kamishina wa Zanzibar ambapo aliwadhibiti ACT vilivyo kwenyeuchaguzi wa 2020. Leo watu hao amboa ni kwa vitendo walionekana wazi kuwaumiza Vilivyo wapinzani wakati wa awamu iliyopita. Walipoteuliwa tu Chadema walipaswa kuvunja makubaliano na kususia shughumi zote za kwenda kunywa chai Ikulu kwa Mkoloni wa Karne hii.

Na kama kuna Mpinzani anayedhani kuwa chaguzi zijazo zitakua za haki bila Katiba mpya anajidanganya sana.

Wabunge wa CCM na CCM na serikali yake wana pesa nyingi na nafasi nyingi za kuwahinga wakuu wa vyombo vya usimamizi wa uchaguzi vikiwemo vyombo vya kipolisi.

Wakubwa wengi wa vyombo vya Dola ni makada mapandikizi ya CCM. Hawajali umoja wa kitaifa wala ustawi wa Demokrasia wala wajibu wa serikali kwa wananchi. Wanachojali ni kupata vyeo na mali binafsi hata kama watavyeka watu kwa halaiki.


Wapinzani walekua wakilalamika tu bila kujua kuwa hakuna anayejali malalamiko yao na maulivu yao .
Dawa ingekua moja tu kuwafungulia kesi kwa majina yao mana wanayoyafanya hayana tija kwa taifa zaidi ya kusaka vyeo wao binafsi kwa gharama ya kujenga mpasuko na chuki kwenye jamii.


Mahita aliwahi kudaganya umma kuwa kuna Kontena la visu limeinguzwa na Chama cha CUF lakini mpaka leo CUF hawajamfungulia kesi ya kuchafua image ya Chama kwa taifa na kimataifa.

Kama wapinzani watabaki kumlia Rais aliyeweka safu yake ya kudhibiti uchaguzi na kuhakilisha anashinda mitano tena bila kudili na RPC au ocd mhusika basi itakua ni kucheza na akili za watu.
OCD anasema wazi kuwa wewe hushindi halafu watu wanabaki wanakenua meno wakati kuna mahakama na sheria zipo za namna jeshi la polisi linayopaswa kutenda wakati wa uchaguzi.

Mbona Mtikila aliwatetemesha sana watawala kwa kutumia mahakama japo hakuwa na wanachama wengi wala ruzuku kubwa.
 
Sisiemu INGIZA UPEPO ....tumieni akili wanachama wakiamua kuwafuata viongozi wao huko polisi KITANUKA MBAYA!!!!
 
Hili nalo neno.
 
Uko sahihi amejichafua zaidi hata waliokuwa hawamjui sasa ndio wameziona rangi zake. Kampeni za kumchafua zimeanzishwa rasmi na jeshi la polisi
Alikuwa anasubiria US warudishe msaada wa pesa ya MCC, akijinadi kuwa utawala wake unafuata haki na demokrasia. Hapa amekwishaifunga milango. Itabidi aendelee kukopa mpaka afikie ukomo wa kukopa.

Hakuna nchi iliyostaarabika inayofurahia kujishikamanisha na madikteta, na hasa madikteta wenyewe wawe ni ombaomba na kopakopa.

Idara ya uhusiano wa kimataifa ya CHADEMA ifanye kazi ya kumwelezea kiuhalisia huyu mama alivyo. Ili asuende kuyatia najisi mataifa yaliyostaarabika. Aende akazurule kwa madikteta wenzake, lakini siyo kwa watu wastaarabu.
 
Nchi imefika Patamu sana
 
Duuh! Huyu mama kaamua kuonesha kuwa yeye kweli siyo raia wa Tanganyika, kaja kutawala tu.
 
Sasa hii ni kuvuka mipaka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…