Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe akutana na Rais Samia Ikulu leo Desemba 31, 2022

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe akutana na Rais Samia Ikulu leo Desemba 31, 2022

View attachment 2464661

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe pamoja na Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Abdulrahman Kinana mara baada ya kupokea taarifa ya Maendeleo ya mazungumzo ya mchakato wa maridhiano ya kisiasa, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 31 Desemba 2022.

View attachment 2464667
======

Hii ndio taarifa mpya iliyotufikia leo 31/12/2022

Taarifa zaidi zinadokeza kwamba huu ndio ule ule mwendelezo wa Majadiliano ya Maridhiano kuelekea Katiba Mpya na Tume huru ya Uchaguzi , ambapo Rais Samia amepokea Taarifa ya Maridhiano hayo

Mazungumzo hayo yalihudhuriwa pia na Makamu Mwenyekiti wa CCM Abdulrahman Kinana

Raisi Samia wengi hawajui sababu ya kumchagua kinana kuwa makamu na si mtu mwingine.

Sababu kubwa ni kwamba Kinana yuko tofauti kidogo kwenye utendaji wake. Kwanza amekulia Arusha na anaona vitu kama watu wengi wa Arusha kwa mtazamo wa biashara zaidi na sio siasa. Hivyo Kinana anaweza kabisa kuelewana na wakina Mbowe kwasababu hii. Yeye kinana anapima vitu na kuweka strategy na sio ushabiki. Anajua fika nchi hii asilimia 40-45 ni wapinzani ni bora kushinda kwa 50-55 kama majirani wa kenya na kuna na imani kuliko kushinda kwa feki kwa 80% na nchi ikawa kama Magu alivyo iacha kisiasa. Na sasa tunaona kumbe hata watu wengi walikuwa hawapendi zile chaguzi bila kujali chama. Kinana ni 70 years plus naye Mama ni muhula wa mwisho hivyo hana sababu ya kungangania vitu na watu ambao hata hawampendi na ni wa nafiki ndani ya CCM.
 
Hizi ndiyo siasa. Vyama vya upinzani viko kikatiba na wapinzani ni wananchi wenzetu.

Ila yule shetani wa Chato aliufanya upinzania ni uadui. Asante Mungu kwa kusikia maombi yetu hatimaye akasepeshwa jehanam mnamo 17/ 03/ 21
Samehe 7*70 mkuu...ametangulia ,tumuache apumzike..
 
Hizi picha wenzake wanazitumia vibaya. Bora akutanenao kimyakimkya tu na matokeo yakiwa mazuri, ndio ajitokeze hadharani kupiga nao picha.

Pia, Mbowe akumbuke kauli za Makamba na kikwete za hivi kariibuni kwenye Mkutano Mkuu wa CCM.
Wivu tu ndio umekujaa mpaka umekuwa Kama mtoto mdogo
 
Asali

Asali ya nyuki wadogo ina kauchungu kwa mbali, Lakini inafaa kwa kulamba

Mwenyekiti analamba asali

Nasikia bei ya asali haijaathiriwa na Vita vya Ukraine na Russia

Vita inaendelea lakini asali inalambika kama kawaida

Hivi ile vita ya ccm mpya na ccm asili ni nani aliyeamua ushindi, Na iliishia wapi

Tunashauriwa tusitumie vitu vyenye sukari ya kutengeneza lakini inaruhusiwa kutumia sukari ya asili kama asali

Tuendelee kulamba asali kabla mzinga haujabomoka

Mwenyekiti on Fire

Lamba asali mwenyekiti

Majungu. Na wewe kalambe asali.
 
View attachment 2464661

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe pamoja na Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Abdulrahman Kinana mara baada ya kupokea taarifa ya Maendeleo ya mazungumzo ya mchakato wa maridhiano ya kisiasa, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 31 Desemba 2022.

View attachment 2464667
======

Hii ndio taarifa mpya iliyotufikia leo 31/12/2022

Taarifa zaidi zinadokeza kwamba huu ndio ule ule mwendelezo wa Majadiliano ya Maridhiano kuelekea Katiba Mpya na Tume huru ya Uchaguzi , ambapo Rais Samia amepokea Taarifa ya Maridhiano hayo

Mazungumzo hayo yalihudhuriwa pia na Makamu Mwenyekiti wa CCM Abdulrahman Kinana
CHADEMA akili walizokuwa nazo wamepeleka wapi ?

Hivi bado hamjaelewa kuwa siasa za awamu hii ya Samia ni siasa za picha na vyama pinzani ???

Hivi hamjui kuwa mnahalalisha uvunjwaji wa katiba unaofanywa na wenzenu kwa matukio ya picha kama haya???

Hamkuona matokeo ya kikosi kazi ???

Mnadhani hizi picha zitawapa haki yenu ya kufanya mikutano ya hadhara??

Subirini muda utawapeni majibu ila mtakuwa mmeshachelewa sana.
 
Back
Top Bottom